Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-17 15:34:33    
Mwigizaji mwanamke wa China Chen Xiaoyi

cri

Chen Xiaoyi ni mwigizaji mwanamke ambaye katika miaka ya hivi karibuni amekuwa anaonekana mara kwa mara kwenye televisheni kutokana na michezo yake ya kuigiza kuoneshwa, yeye ni mwigizaji wa Jumba la Michezo ya Kuigiza la Beijing. Hivi karibuni amerudi tena kwenye jumba hilo na kuwa mwigizaji mkuu katika mchezo wa kuigiza uitwao "Lianhua".

Mchezo wa kuigiza wa "Lianhua" ni hadithi iliyotokea mjini Beijing inayomwelezea bwana Tianhe na mke wake Lianhua ambao mwanzoni walikuwa maskini sana, katika miaka yao ya kujitafutia utajiri hatua kwa hatua walikuwa wakielekea kwenye mambo mabaya. Kitu kimoja cha kale walichopata chenye thamani kubwa kilikuwa ni tumaini lao la kuondoka kwenye umaskini, lakini ni kitu hicho kilichoharibu mapenzi yao waliyopalilia kwa miaka mingi. Mchezo huo ulianza kuoneshwa kutoka mwisho wa hadithi, kwamba mke Lianhua alimuua mumewe kwa bastola aliyebadilisha mapenzi yake, kisha alijiua mwenyewe. Kuonesha hadithi kutoka mwisho hadi mwanzo ni mtihani kwa uhodari wa mwigizaji. Bi Chen Xiaoyi alisema,

"Mchezo huo unapoanza tu mara unafikia mwishoni na kisha unaanza kushuka pole pole, ambapo si kama michezo mingine ambayo inaeleza pole pole kutoka mwanzo hadi mwisho, kwa hiyo kuigiza namna hiyo ni vigumu sana kuwavutia watazamaji baada ya kufahamu mwisho wa hadithi na kuelezwa kutoka mwisho huo hadi mwanzo."

Mchezo wa "Lianhua" ni mchezo wa kwanza wa jukwaani kwa Chen Xiaoyi baada ya kuachana na michezo ya kuigiza kwa miaka mitano. Kwenye mchezo huo wa "Lianhua" aliigiza kuwa ni mhusika mkuu aitwaye Lianhua, ni mwanamke anayejali sana mapenzi yake kwa mumewe, lakini mwishowe alikufa kutokana na mapenzi yake. Mwigizaji Chen Xiaoyi aliigiza kwa kina sana. Alisema, katika Jumba la Michezo ya Kuigiza la Beijing wahusika wakuu huwa ni waigizaji wanaume, lakini kwa bahati katika mchezo huo mhusika mkuu alikuwa mwanamke. Alisema kuigiza mchezo wa jukwaani ni vigumu zaidi kuliko michezo ya filamu, kwa sababu mwigizaji anaigiza kwa hisia mfululizo toka mwanzo hadi mwisho. Alisema ni furaha yake kupata nafasi ya kuigiza mwanamke kama Lianhua anayethubutu kupenda na kuchukia.

Bi. Chen Xiaoyi mwenye umri wa karibu miaka 40, alizaliwa mkoani Sichuan. Miaka zaidi ya kumi iliyopita alipokuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uigizaji cha Beijing alipata nafasi ya kuigiza filamu iitwayo "Kibarua msichana Aliyetoka kijijini". Katika mchezo huo aliigiza kuwa kibarua msichana aitwaye Zhao Xiaoyun, uigizaji wake ulikuwa halisi uliwavutia sana watizamaji wengi kuliko michezo mingine iliyooneshwa wakati huo kwenye televisheni, na kutokana na uhodari wa kuigiza alijulikana sana. Tokea hapo alikuwa mara kwa mara akitokea kwenye michezo ya televisheni, na aliwahi kuigiza kwenye michezo ya "Mke wa Mwanajeshi", "Mama Mzazi" aliyehangaika kwa ajili ya mtoto wake. Katika michezo yote aliyoigiza alikuwa "mwanamke mzuri", Bi. Chen Xiaoyi alisema amechoka na nafasi kama hiyo na anataka kuigiza wanawake wa aina nyingine kabisa katika michezo ya kuigiza. Alisema,

"Wanawake niliowaigiza katika filamu wote walikuwa ni wanawake wanaosikitisha, nimechoka kuigiza wanawake kama hao, nataka kuigiza wanawake wa aina nyingine, naona kwamba mwigizaji anatakiwa awe na uwezo wa kuigiza watu wa aina mbalimbali."

Bi. Chen Xiaoyi ana sifa nzuri miongoni mwa waigizaji wenzake. Uigizaji wake unaolingana na hali halisi unawaingiza watazamaji ndani ya mazingira halisi. Yeye ni mtu mnyoofu na yuko makini kwa kila jambo, hata kama dogo. Alisema uigizaji wake ni kama yeye mwenyewe kwamba lazima aigize kwa makini sana. Alisema,

"Mimi siwezi kuigiza michezo kwa sura tu, kama moyoni mwangu sikuwa na hisia za kweli au nikishindwa kupata hisia hizo siwezi kulia machozi kwa kelele tu na kuigiza kwa kuonesha sura. Hii ni kanuni yangu ya uigizaji."

Ingawa miongoni mwa waigizaji wengi Bi. Chen Xiaoyi hakujitokeza mbele sana, lakini anavutia watazamaji kutokana na jinsi anavyoigiza kwa undani. Alisema baada ya kuolewa na kuwa mama mazazi mambo ya kimaisha yanasaidia zaidi uigizaji wake.

Idhaa ya kiswahili 2008-03-17