Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-17 16:37:49    
Chimbuko la utengenezaji wa taa za kisanaa za jadi ya China

cri

Tarehe 15 mwezi Januari kwa kalenda ya kilimo ya China, ilikuwa siku kuu ya Yuanxiao ya jadi ya China, ambayo inachukuliwa na wachina kuwa ni mwisho wa wakati wa sikukuu ya Spring. Sikukuu ya Yuanxiao pia inaitwa sikukuu ya taa, katika siku hiyo licha ya wachina kula Yuanxiao, ambacho ni aina ya chakula cha wachina kinachotengenezwa kwa donge la unga wa mchele laini na unaonata, na ndani yake vinawekwa vijazo vya aina mbalimbali, shughuli nyingine muhimu ni kuangalia taa za kisanaa za jadi ya China. Wakati wa sikukuu hiyo, taa za kisanaa za rangi nyekundu pamoja na za rangi mbalimbali zinatundikwa kwenye mitaa yote mikubwa na midogo, ambazo zinaongeza shamrashamra ya sikukuu. Katika mji wa Gao, mkoani Hebei, kuna sehemu moja ambayo ni chimbuko la utengenezaji wa taa za kisanaa za jadi ya China, kumbukumbu zilizoandikwa kwenye vitabu vya historia zinasema, utengenezaji wa taa za jadi nchini China ulianza katika enzi ya Han ya nchini China ya kabla ya miaka zaidi ya 2,000 iliyopita. Taa zinazotengenezwa na mji wa Gao pia zinaitwa taa za kifalme, ambazo zilitumika katika majumba ya wafalme. Bw. Shi Youquan kutoka kituo cha utafiti na utengenezaji wa taa za kifalme, alisema,

"Mfalme Qian Long wa enzi ya Qing alipofanya matembezi ya kwenda sehemu ya kusini ya China, alifika kwenye mji wa Gao, wakati ule ulikuwa tarehe 15 mwezi Januari ya kalenda ya kilimo ya China, aliona kote zilitundikwa taa za sanaa za rangi nyekundu za kupendeza, baada ya kurejea alichagua taa kadhaa na kuzitundika katika jumba la kifalme, hivyo taa za sanaa za mji wa Gao zikaitwa taa za kifalme."

Tangu taa za mji wa Gao zichaguliwe kutumika katika jumba la mfalme, taa za huko zikawa na sifa kubwa, na zilienea mbali. Mji wa Gao nao umekuta sehemu ya jadi inayotengeneza taa za sanaa za jadi ya China. Katika zaidi ya miaka 200 iliyopita, ufundi wa kutengeneza taa za kifalme wa mji wa Gao uliendelezwa na wasanii kwa enzi mbalimbali mfululizo, taa za sanaa za kifalme zimekuwa na umaalumu wake na kutengenezwa kwa wingi, hivi sasa taa za aina hiyo zimeenea hadi kwenye sehemu nyingi za nchini na nchi nyingi za nje.

Kijiji cha Tuntou cha tarafa ya Plum kimekuwa maarufu zaidi kwa utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme kati ya vijiji vingi vinavyotengeneza taa za aina hiyo vya mji wa Gao. Mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, kijiji hicho kilikuwa kijiji kikubwa maalumu kinachoshughulikia utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme cha nchini China. Utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme umekuwa njia muhimu ya kuongeza pato kwa wanakijiji wa kijiji cha Tuntou, wanakijiji wanasema kwa furaha kuwa wao wanakimbilia jamii yenye maisha bora ya "Xiaokang" wakiwa na taa mikononi.

Kijiji cha Tuntou kiko kwenye sehemu ya kusini mashariki ya mji wa Shijiazhuang, mji mkuu wa mkoa wa Hebei, umbali kati ya sehemu hizo mbili ni kilomita 100 hivi. Unapokaribia kwenye kijiji hicho, utaona viwanda vingi vya utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme kwenye kando mbili za barabara. Mkurugenzi wa kamati ya kijiji cha Tuntou, Bw. Su Zhenguo alipozungumzia utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme, alisema,

"Hivi sasa kijiji hicho kina familia 1,400 za wakulima, na karibu nusu ya idadi ya familia hizo zinashughulikia utengenezaji wa taa za sanaa za kifalme, na karakana kubwa ni zaidi ya 30, kwa uchache kabisa kijiji hicho kinatengeneza taa 4,000 kwa mwaka, ambazo thamani yake ni zaidi ya Yuan milioni 100. Taa hizo licha ya kuuzwa kwenye sehemu mbalimbali za nchini, zinasafirishwa kwa nchi za Asia ya kusini mashariki na kwenye sehemu ya mashariki ya kati."

Watalii wanapotembelea sehemu hiyo, wanaweza kutengeneza taa za sanaa wao wenyewe. Kama wanashindwa kutengeneza taa kubwa, wanaweza kutengeneza taa rahisi, tena wanaweza kubuni picha wanazopenda.

Kwanza kabisa vijiti vya mianzi vinavyotumiwa kutengeneza taa za sanaa vinapaswa kupashwa moto juu ya majiko ili kuvipinda hadi viwe na umbo kama herufi T, vijiti vinne vilivyopindwa namna hiyo, vikiunganishwa pamoja vikawa mraba, miraba hiyo ikiunganishwa pamoja vikawa fremu za taa.

Halafu aina ya karatasi nyembamba maalumu ya Xuan inafunikwa nje ya fremu za taa, karatasi za Xuan ni nyembamba sana, hivyo mwangaza wa mshumaa uliowekwa ndani unaweza kuangaza sehemu ya nje. Baada ya kufunika karatasi ya Xuan, watu wanachora michoro ya aina mbalimbali juu yake, kwani ufundi na mali-ghafi zinazotumika kutengeneza taa za sanaa za jadi ya China, hivyo karatasi hizo zichorwe kwa brashi yenye wino, ili zionekane kuwa na umaalumu wa utamaduni wa jadi ya China. Kazi ya mwisho ni kuweka kitako cha taa kwenye sehemu ya chini ya taa, kisha kuchomeka mshumaa mmoja kwenye kitako cha taa, basi kufika hapo taa moja rahisi inakuwa imekamilika.

Ni dhahiri kuwa kutengeneza taa moja rasmi ya sanaa ya kifalme siyo kazi rahisi. Inahitaji kazi za aina 5 na 6 hivi, tena kazi zote zinafanywa kwa mikono. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mji wa Gao imeongeza uungaji mkono kwa shughuli za kutengeneza taa za sanaa za kifalme, na inatekeleza sera zenye nafuu kwa uvumbuzi wa taa za sanaa za kifalme, zikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku ya utafiti wa sayansi na kupunguza kodi, tena imeanzisha kampuni moja ya utafiti wa taa za sanaa za kifalme ya mji wa Gao ili kushughulikia mahususi utafiti na usanifu wa taa za aina hiyo. Aidha, ina kiunga mkono kijiji cha Tuntou kuunda jumuiya ya utafiti wa taa za sanaa za kifalme, na kushirikisha familia za wakulima kufanya uvumbuzi. Jumuiya ya utafiti wa taa za sanaa za kifalme, imewakaribisha baadhi ya wataalamu wa utafiti wa vitu vya sanaa waende huko kuwa waelekezaji wa kazi za ufundi kijijini mwao, na kufanya utafiti ili kuvumbua aina mpya za taa za sanaa kwa kuunganisha umaalumu wa taa zinazotengenezwa kijijini. Sasa wanatengeneza zaidi ya aina 200 za taa, zikiwemo zenye maumbo ya pembe nane, tufe, tikiti maji, taa ndogo zinazotengenezwa nao ni kama machungwa, na zile kubwa ni kama nyumba. Wanakijiji wa kijiji cha Tuntou ni hodari sana, wamevumbua baadhi ya mitambo maalumu kwa ajili ya utengenezaji wa taa za sanaa, hivi sasa ufanisi wa kazi zao umeinuka kwa mara kumi kadhaa.

Mwandishi wetu wa habari alifika nyumbani kwa mwanakijiji Zhang Xizhong kwenye kijiji cha Tuntou, kati ya watu watatu wa familia hiyo, watu wawili wanafanya kazi za kutengeneza taa za sanaa za kifalme, na zinawaletea ongezeko la pato la zaidi ya Yuan elfu 20 kwa mwaka, na wanaishi maisha ya furaha. Alisema,

"Maisha yetu yameinuka sana kuliko wakati nilipokuwa mtoto. Tumenunua magari mawili pamoja na vyombo vyote vya umeme vya nyumbani. Hali hiyo ni ya kawaida kabisa katika kijiji chetu."

Idhaa ya kiswahili 2008-03-17