Mkutano wa nne wa mawaziri wa kundi la nchi 20 kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, nishati isiyo na uchafuzi na maendeleo endelevu, ulifanyika kwa siku 2 na kufungwa tarehe 16 katika Chiba, Japan. Mkutano huo ni sawa na mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa wa mwaka uliopita, japokuwa pande mbalimbali zilizoshiriki kwenye mkutano huo zilithibitisha tena lengo la pamoja la kuhifadhi mazingira, lakini zimeshindwa kuondoa tofauti zao katika hatua halisi za utekelezaji.
Mkutano wa mwaka huu wa kundi la nchi 20 ulifanya majadiliano kuhusu mada tatu za kanuni mpya, ambazo ni teknolojia ya kupunguza na kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia, kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea na kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani baada ya mwaka 2013. Katika suala la kuhimiza na uvumbuzi wa teknolojia, kuna mgongano dhahiri kati ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea hasa kuhusu namna ya kuthibitisha sekta muhimu, teknolojia muhimu na uwekaji wa kiwango cha kuinua ufanisi wa matumizi ya nishati. Katika eneo la utoaji misaada ya fedha, nchi zilizoendelea zinasisitiza kutegemea umuhimu wa masoko, wakati nchi zinazoendelea zinasisitiza kuunganisha kazi mbili za uelekezaji wa serikali na masoko.
Namna ya kudhibiti ongezeko la joto la dunia kwa kuchukua hatua zenye ufanisi ni changamoto inayowakabili binadamu wote. Kwenye mkutano wa wakuu wa nchi nane uliofanyika nchini Japan mwaka jana, lilitolewa wazo la kupunguza kwa nusu ya utaoji hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani. Lakini wachambuzi wanasema, tangu "Mkataba wa Kyoto" usainiwe, baadhi ya nchi zilizosaini mkataba huo licha ya kutotenda vitendo halisi katika kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani, bali zilikwenda kinyume na mkataba huo. Marekani, nchi inayotoa hewa nyingi inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani, bado inakataa kusaini mkataba huo.
Kwenye mkutano huo, wazo lililotolewa na baadhi ya nchi zilizoendelea la kuthibitisha nchi zinazotoa kwa wingi hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani kwa kigezo cha jumla ya utoaji wa hewa ya kuongezeka kwa joto, linapingwa na nchi nyingi. Ofisa mmoja wa uhifadhi ya mazingira wa India alisema, wastani wa utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani wa kila mtu wa India ni tani moja tu, lakini ule wa Marekani umezidi tani 20, alisema hajui ni kwa nini nchi kama ya India imeorodheshwa katika kundi la nchi zinazotoa kwa wingi hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
Waziri wa mazingira na utalii wa Afrika ya Kusini alisema, Afrika ya Kusini inapinga kuwekwa kwenye orodha ya nchi zinazotoa hewa nyingi zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Bw. Tony Blair alipotoa hotuba tarehe 15 alisema, nchi zilizoendelea zimekuwa na viwanda vingi, na zilisababisha mgogoro wa hali ya hewa katika mchakato huo. Sasa nchi zinazoendelea zinajenga jamii yenye viwanda, ambapo bidhaa nyingi zinazozalishwa na bidhaa hizo zinasafirishwa kwa nchi zilizoendelea na kutumiwa na watu wa nchi hizo. Hivyo si haki kuweka matarajio kubwa kuhusu nchi zinazoendelea katika suala la kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
Kwenye mkutano wa tarehe 16, naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China aliyeshiriki kwenye mkutano huo Bw. Xie Zhenhua alisema, kujenga kanuni kuhusu hali ya kila nchi ni tofauti na ya nchi nyingine, na iko katika kipindi tofauti cha maendeleo, na zinazopaswa kuchukuliwa nazo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, pia zinatakiwa kuwa tofauti. Kila nchi inatakiwa kutafuta mpango mwafaka wa utatuzi kwa msimamo wa kuaminiana na makini. Bw. Xie Zhenhua alisema nchi zilizoendelea zinatakiwa kutoa fedha za kutosha kwa nchi zinazoendelea, na kuzisaidia kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
|