Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-21 18:38:45    
Wanafunzi wa Afrika kwenye shule ya sarakasi ya Wuqiao China

cri

Wanafunzi kutoka Afrika wanaojifunza sarakasi kwenye shule ya sarakasi ya Wuqiao, mjini Cangzhou mkoani Hebei, kaskazini mwa China, miongoni mwa wanafunzi hao, mdogo zaidi ni mwenye umri wa miaka 11 na mkubwa zaidi ni mwenye umri wa miaka 23. Kwa nini wanafunzi hao kutoka sehemu mbalimbali walikuja kujifunza sarakasi nchini China? Na maisha yao nchini China yakoje?

Wilaya ya Wuqiao iko katika mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China ambayo ni wilaya inayojulikana nchini na nchi za nje kwa michezo ya sarakasi. Shule ya sarakasi ya Wuqiao ya China iko kwenye wilaya hiyo. Mwaka 1999, shule hiyo ilipewa jina la kituo cha mafunzo ya sanaa ya sarakasi cha kimataifa cha Wuqiao cha China, halafu ilianza kuwafundisha wanasarakasi wa nchi za nje. Mwaka 2002, shule hiyo ilianza kutekeleza mpango wa wizara ya utamaduni ya China wa kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa wasanii wa sarakasi. Pia kwa sasa shule hiyo imefundisha vikundi vitano vya wanafunzi wa nchi za Afrika. Hivi sasa kikundi cha sita cha wanafunzi wa nchi za Afrika wanajifunza sarakasi kwenye shule hiyo. Naibu mkuu wa shule hiyo Bw. Qi Zhiyi alipozungumzia kuhusu wanafunzi hao wa Afrika alisema kwa fahari: "nchi yetu iliweka kazi ya kuwafundisha wanafunzi wa nchi za nje huko Wuqiao na kuweka kwenye shule yetu, kwa kuwa Wuqiao ni kama chimbuko la sarakasi lililojulikana sana duniani. Kama walivyosema wanafunzi hao wa Afrika kuwa, wanapenda kuja China kujifunza sarakasi ya asili. Wanaona wanajifunza sarakasi ni kutoka kwenye chimbuko la sarakasi la Wuqiao."

Bw. Qi Zhiyi alieleza, wanafunzi hao wa kigeni wanafanya mazoezi kwa makini, hata wakati wa Jumamosi wanaendelea kufanya mazoezi, na wanapumzika katika siku ya Jumapili tu. Mwandishi wetu wa habari alipoingia kwenye ukumbi wa kufanyia mazoezi, aliona wanafunzi zaidi 30 wa kigeni wakifanya mazoezi, baadhi yao walifanya mazoezi ya kuchezea kofia, wengine walifanya mazoezi ya kupanda baiskeli yenye gurudumu moja, na wengine walifanya mazoezi ya sarakasi. Mwandishi wetu wa habari alivutiwa na msichana anayefanya mazoezi ya kujiviringisha. Msichana huyo ana urefu wa mita 1.4. mwalimu wake alimwambia kuwa msichana huyo anaitwa Aileen na alitoka Kenya, na ana umri wa miaka 11, ambaye ni mdogo zaidi kuliko wanafunzi wengine wageni. Mwandishi wetu wa habari alipomwuliza kwa nini yeye alikuja China kujifunza sarakasi kutoka nchi ya mbali? Aileen alijibu bila ya kusitasita: "mimi mwenyewe, ninapenda sana sarakasi hivyo nilikuja China kujifunza sarakasi."

Kwa sababu Ailleen ana umri mdogo, wakati fulani hakuweza kueleza maoni yake kikamilifu, lakini kikwazo cha lugha hakipunguzi mawasiliano kati ya Ailleen na waalimu wake. Waalimu wengi walisema wanampenda sana Aillen, mwalimu Liang Wenjiang alisema: "ingawa msichana huyo ana umri mdogo, lakini anajua mambo mengi, anajua namna ya kufanya mazoezi kwa bidii nchini China, ni msichana hodari sana. Waalimu wanampenda sana. Sasa anamwambia mwalimu wake, anataka kujifunza kuviringika."

Mvulana Ronand kutoka Kenya ana umri wa miaka 14, alipohojiwa kwa nini alikuja China kujifunza sarakasi, jibu lake linaonesha kupevuka kwake. Alisema:"wachina wanajua sana sarakasi, nilikuja China kujifunza sarakasi kwa sababu ninataka kubadilisha maisha yangu na kubadilisha mustakabali yangu."

Ronand alisema walikuja China kujifunza sarakasi baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingi, kwa hivyo wanathamini sana fursa hiyo. Ronand alijifunza kubinuka na kuchezea baiskeli yenye gurudumu moja. Mwandishi wetu wa habari alimwuliza, mazoezi hayo ni magumu au la? Ronand alisema, si magumu. Alipoulizwa kama anakumbuka familia yake au la, alisema: "(sauti 5)

"ndiyo, nawakumbuka wazazi wangu na ndugu zangu. Kila mwezi nawapigia simu, na kuwasiliana nao kwa kupitia tovuti ya internet."

Ronand alisema waalimu wa shule hiyo ni wazuri sana na wanawasaidia katika mambo mengi, na wanashukuru sana. Mwalimu Ma Chao alieleza hali moja iliyotokea kati yake na Ronand, akisema: "Ronand ana uhusiano mwema na watu wengine, anapowakumbuka jamaa zake, aliniomba nimkumbatie, siku moja, hali ya hewa ilikuwa baridi sana, Ronand hakuweza kuzoea, nilimletea sweta, halafu alinikumbatia na kuniita: Baba, lakini umri wangu ni miaka 23 tu, niliona haya lakini nilitiwa moyo sana."

Naibu mkuu wa shule hiyo Bw. Qi Zhiyi pia alimwelezea Hibreate kutoka Ethiopia. Hibreate ana umri wa miaka 23 na yeye ni mkubwa miongoni mwa wanafunzi hao wa kikundi hicho, anaweza kuongea vizuri lugha ya Kiingereza. Yeye alikuja China kujifunza sarakasi kwa malipo yake mwenyewe. Mwandishi wa habari aliuliza: " "kwa nini ulikuja China kujifunza sarakasi."

"wakati nilipokuwa nchini Ethiopia, nilikuwa na ufahamu kidogo kuhusu utamaduni wa China kwa kupitia matangazo ya televisheni na magazeti, na marafiki zangu wanaipenda sana China. Ndani ya familia yangu, watoto wanne wanajifunza sarakasi, lakini tunajua sarakasi ya China ni nzuri sana. Baadaye mdogo wangu wa kike alikuja kwenye shule hiyo na kujifunza sarakasi. Aliona utamaduni wa China na ustadi wa sarakasi ni mzuri sana, hivyo mimi niliamua kuja China kujifunza sarakasi."

Hibreate alianza kujifunza sarakasi akiwa na umri wa miaka 11, na kuanza kucheza sarakasi jukwaani tangu akiwa na umri wa miaka 13, mpaka sasa alikuwa na uzoefu wa kuonesha sarakasi kwa miaka 10. Ingawa alikuja China si kwa muda mrefu, lakini anajua kusema kidogo lugha ya kichina, na matamshi yake ni sanifu. Hibreate alisema hajajua kueleza matarajio yake kwa kichina, hivyo anataka kueleza kwa Kingereza, akisema: "ninataka mwaka 2008 uwe ni mwaka wa mafanikio kwa watu wote, na ninawatakia wachina kila la heri!"