Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-19 16:50:42    
Mapishi ya nyama ya nguruwe na vipande vya pilipili mboga

cri

Mahitaji

Nyama ya nguruwe gramu 370, pilipili mboga gramu 70, mafuta gramu 25, sosi ya pilipili hoho gramu 10, mchuzi wa sosi gramu 10, mvinyo wa kupikia gramu 10, sukari gramu 5, vitunguu maji gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 3.

Njia

1. chemsha maji, halafu tia nyama ya nguruwe kwenye maji, baada ya dakika 20, ipakue. Halafu uikate iwe vipande vipande.

2. mimina mafuta kwenye sufuria, washa moto, tia vipande vya nyama kwenye sufuria, korogakoroga, halafu ipakue. Tia sosi ya pilipili hoho, korogakoroga, kasha tia pilipili mboga na vipande vya vitunguu maji korogakoroga, halafu mimina mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, korogakoroga, tia chembechembe za kukoleza ladha, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.