Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-20 16:40:08    
Shule ya msingi ya Chantang inayofuatilia watoto waliobaki vijijini ambao wazazi wao wanafanya kazi za vibarua mijini

cri

Kutokana na wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini wanaongezeka siku hadi siku, hivi sasa kuna watoto milioni 20 vijijini ambao wazazi wao wamekwenda mijini inawabidi waishi nyumbani kwa jamaa zao au waishi peke yao.

Shule ya msingi ya Chantang iliyoko wilaya ya Lingbi mkoani Anhui, ambayo inafuatilia sana watoto waliobaki vijijini, ambao wazazi wao wanafanya kazi za vibarua mijini . Mkuu wa shule hiyo Bw. Zhou Changbin alituelezana kwa nini miaka kadhaa iliyopita shule ya msingi ya kawaida ilibadilika kuwa shule ya bweni, akisema:

"Mwaka 2004, mwanafunzi mmoja wa shule yetu alianza kuonesha mabadiliko madogo, alianza kuchelewa shuleni, na hali yake ya masomo shuleni ilizidi kuwa mbaya. Baada ya uchunguzi kuhusu hali hiyo, tuliona kuwa wazazi wake wanafanya kazi za vibarua mijini, na mwanafunzi huyo aliishi pamoja na babu yake na bibi yake, lakini babu na bibi hawawezi kumtunza vizuri."

Mkuu wa shule hiyo aliona kuwa, ni kawaida kuwa wazazi wa wanafunzi wengi wa shule hiyo, kunafanya kazi za vibarua mijini, na wanafunzi hao walitunzwa na babu na bibi zao. Upungufu wa elimu ya familia unasababisha watoto wengi waliobaki vijijini ambao wazazi wao walifanya kazi za vibarua mijini kutokuwa na mwendo mzuri, wengi kati yao wanakuwa na hali ya kutopenda masomo na mara kwa mara wanatoroka shuleni au kuacha masomo.

Viongozi wa shule hiyo waliona kuwa ili kutatua suala hili, wanapaswa kubadilisha mtizamo wa kuendesha shule, kupata njia mpya na kuwafanya watoto wengi zaidi wapate elimu na usimamizi nje ya masomo wakiwa shuleni. Mwaka 2005, shule hiyo ilianzisha rasmi mradi wa kujenga bweni kwa ajili ya watoto hao. Kwenye shule za kawaida za kiserikali, muda wa kukaa shuleni kwa wanafunzi ni saa 6 hivi, lakini shule hiyo ilirefusha muda huo kuwa saa 24 ambapo wanafunzi wanaruhusiwa kusoma na kulala shuleni. Mkuu wa shule hiyo Bw. Zhou alisema,

"Tuliongeza vitu vingi kutokana na ukarabati wa shule yetu, hata nyumba za walimu zilichukuliwa kuwa ni mabweni ya wanafunzi, na madarasa kadhaa yalichukuliwa kuwa ni bwalo la wanafunzi, hivyo tatizo la bwalo na bweni la wanafunzi linatatuliwa. Aidha, tuna walimu watano maalumu wanaoshughulikia maisha ya wanafunzi hao ikiwa ni kusafisha nguo, kuwatunza wanafunzi hao wakati wanapolala, na kufuatilia afya ya kisaikolojia ya wanafunzi hao. Walimu hao wote ni wanawake, ambao ni kama mama wao shuleni."??

Bw. Zhou pia alieleza kuwa shule hiyo iliajiri wapishi kupika vyakula vya aina mbalimbali vinavyoweza kuleta virutubisho kwa wanafunzi.??

Aidha, shule hiyo pia ilianzisha utaratibu wa kuzungumza kwa simu na wazazi wa wanafunzi kila baada ya muda, watoto wanaweza kuzungumza na wazazi wao. Baba Mzazi wa mwanafunzi wa shule hiyo Bw. Zhang alisema, hatua hiyo inawafanya wazazi wanaofanya kazi za vibarua waweze kufanya kazi kwa utulivu zaidi. Alisema,

"hali ya maendeleo ya masomo shuleni ya mtoto wangu imeinuka sana kuliko ilivyokuwa kabla ya kuishi bwenini. Shule hiyo ilifuatilia sana masomo ya watoto hao, na mazingira ya bwenini pia ni mazuri. Watoto wetu wanatunzwa hapa, sisi wazazi wa watoto hatuna wasiwasi."??

??Wanafunzi hao waliobaki ambao wazazi wao wanafanya kazi za vibarua mijini wanapata ufuatiliaji wa shule, wanaona kuwa shule ni kama nyumbani kwao. Mwanafunzi mmoja Zhang Siwei alisema,

"Tunakua shuleni, na hapa ni kama nyumbani kwetu, tunaipenda sana!"

Idhaa ya kiswahili 2008-03-20