Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-21 15:14:43    
Serikali ya Uingereza ina matatizo ya kufanya uamuzi wa kuondoa jeshi lake kutoka nchi ya Iraq

cri

Tarehe 20 Machi ni siku ya kutimiza miaka mitano tokea Uingereza iifuate Marekani kutuma jeshi kuingia nchini Iraq. Siku hiyo waziri mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown alikutana na mbunge wa Baraza la Juu la Marekani Bw. John McCain na pande mbili zilijadiliana kuhusu suala la Iraq. Baada ya kukutana kwao, kwenye mkutano na waandishi wa habari Bw. John McCain alisema Marekani inalishukuru jeshi la Uingereza ambalo linaendelea kuwepo nchini Iraq na mchango wake. Alisema kutokana na kutopata maendeleo, wananchi wa Uingereza wamekuwa na hisia ya kuvunjika moyo, alisema hii inaeleweka. Vyombo vya habari vya Uingereza vilitangaza maneno hayo ya John McCain, lakini waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown hakusema lolote kuhusu suala hilo la Iraq, alichukua msimamo wa kuwa kimya.

Wachambuzi wanaona kuwa "ukimya" wa Bw. Gordon Brown umeonesha msimamo wake wa kuyumbayumba. Kimsingi sera za Tony Blair na Gordon Brown kuhusu suala la Iraq hazina tofauti kubwa. Kabla ya kuwa waziri mkuu Bw. Gordon Brown alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya Tony Blair, na miaka mitano iliyopita aliwahi kuunga mkono kwa uthabiti Uingereza kutuma jeshi nchini Iraq na kushughulikia mwenyewe mambo husika ya fedha. Lakini kuondoka madarakani kwa Tony Blair kulimfahamisha kwamba suala la Iraq ni kubwa na lisiloweza kupuuzwa katika mambo ya siasa, na pia ni jambo muhimu linalohitaji kupata uungaji mkono wa wananchi. Lakini baada ya Bw. Tony Blair kuondoka madarakani anashindwa kufanya uamuzi wa kuondoa jeshi kutoka Iraq. Kwa mujibu wa takwimu tokea vita vya Iraq ianze hadi leo, askari 175 wa Uingereza wamepoteza maisha yao nchini Iraq, na fedha zilizotumika pauni bilioni sita, au kwa maneno mengine, kwa wastani imemgharimu kila Mwingereza pauni zaidi ya 100. Lakini serikali ya Uingereza ilipoulizwa kuwa "tumepata nini kutoka vita vya Iraq?" Serikali hujibu kwa maneno yasiyoweza kuaminika. Uingereza ikiwa kama kibaraka mbele ya Marekani, inawaaibisha wananchi wa Uingereza. Vita vya Iraq vilivyosababisha vifo vya watu wa Iraq zaidi ya elfu 90 ni ukweli wa mambo usioweza kukubaliwa na watu wa Uingereza.

Hivi karibuni kadiri siku ya kutimia miaka mitano ya vita vya Iraq inavyokaribia, vyama vya upinzani na wananchi wa Uingereza wanazidi kuishinikiza serikali yao na wanataka uchunguzi kuhusu uamuzi wa kupeleka jeshi nchini Iraq na matokeo yake ufanyike. Kutokana na shinikizo hilo waziri mkuu Gordon Brown kwenye barua yake wazi ya tarehe 17 alisema serikali itafanya uchunguzi huo ili kupata mafunzo, lakini huku alisema hali ya Iraq bado ni dhaifu, kwa sasa haifai kufanya uchugnuzi huo. Wachambuzi wanaona kuwa hivi sasa serikali ya Bordon Brown inatatizwa na mambo mawili.

Kwanza tokea Bw. Brown alipopokea wadhifa wa waziri mkuu kutoka kwa Tony Blair mwezi Juni mwaka jana, makosa mengi yaliyotokea katika mambo ya ndani yameshusha heshima na pia Chama cha Leba, kiasi cha uungaji mkono wa wananchi kimeshuka kwa zaidi ya asilimia kumi chini ya chama cha wahifadhina. Kutokana na hali hiyo Bw. Gordon Brown na chama chake hawana uhakika wa kuweza kubadilisha hali hiyo kwa kushughulikia suala la Iraq.

Pili, kama Uingereza ikiondoa jeshi lake hivi sasa ni sawa kuondoa moto chini ya sufuria kwa Marekani, hii ni sababu mojawapo ya Rais George Bush kumtuma Bw. John McCain kwenda Uingereza wakati vita vya Iraq vinapotimia miaka mitano. Ingawa baada ya kukutana na Gordon Brown Bw. John McCain alisema muda wa kukaa kwa jeshi la Uingereza nchini Iraq unaamuliwa na wananchi wa Uingereza, laini pia alisema Marekani inazingatia sana suala hilo. Kama inavyojulikana, Bw. John McCain ni muungaji mkono thabiti wa sera ya Rais George Bush kuhusu suala la Iraq na pia ni mgombea urais wa chama cha Ripublican. Ziara ya John McCain kwa kiasi fulani inamkumbusha Gordon Brown asipuuze "uhusiano usio wa kawaida kati ya Marekani na Uingereza".