|
Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bwana Li Changchun tarehe 23 mchana alikagua kiwanja cha ujenzi wa barabara ya kasi inayoanzia mashariki hadi magharibi nchini Algeria ambayo inajengwa na kampuni ya China.
Bw. Li Changchun alizumgumza na wafanyakazi wa China akieleza matumaini yake kuwa watakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati na kuhakikisha sifa ya barabara hiyo, alisema,
"Barabara hiyo ni daraja la urafiki kati ya China na Algeria. Si kama tu mnatakiwa kukamilisha mradi huo kwa wakati na kuhakikisha sifa ya barabara hiyo, bali pia mnatakiwa kuisadia Algeria kuandaa mafundi, ili serikali ya Algeria isiwe na wasiwasi kuhusu mradi uliojengwa na wafanyakazi wa China."
Barabara ya kasi kutoka mashariki hadi magharibi ya Algeria ni barabara ya kwanza ya kasi ya kisasa nchini humo. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1216 itaunganisha Tunis iliyoko mashariki ya nchi hiyo na Morocco iliyoko magharibi ya nchi hiyo. Si kama tu itakuwa barabara muhimu inayoanzia mashariki hadi magharibi nchini Algeria, bali pia itakuwa barabara ya kimkakati ya nchi za Afrika zilizoko kando ya Bahari ya Mediterranean.
Mwezi Mei mwaka 2006, umoja wa makampuni unaoundwa na kampuni kuu ya ujenzi wa reli ya China na Kampuni ya Zhongxin ulipata zabuni ya kujenga sehemu za magharibi na kati za barabara hiyo. Mwezi Septemba mwaka 2006, mradi huo ulianza rasmi, na inakadiriwa kuwa utamalizika mwezi Januari mwaka 2010. Meneja mkuu wa kampuni ya ujenzi wa reli ya China Bw. Jin Puqing alisema ujenzi wa barabara hiyo una athari mkubwa kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika siku za usoni, alisema,
"Wafanyakazi wanaoshiriki kwenye ujenzi wa barabara hiyo ni wafanyakazi hodari wenye maarifa mengi. Mradi huo unasaidia kuongeza mawasiliano ya kiufundi na kuwaanda wafanyakazi wa nchi hizo mbili, na jambo muhimu zaidi ni kuwa mradi huo utahimiza ushirikiano na urafiki kati ya nchi hizo mbili katika muda mrefu ujao."
China inapojenga mradi huo ambao unasaidia nchi hizo mbili kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja, inafuatilia maisha ya wenyeji wa huko na shughuli za kuhudumia jamii, kwa mfano inawanufaisha wenyeji wanaoishi karibu na barabara hiyo kwa kuchimba visima na kukarabati barabara. Waziri wa habari wa Algeria Bw. Abderrachid Boukerzaza alifurahia hatua za China, alisema,
"Kama barabara hiyo itakuwa na sifa nzuri, itatumiwa kwa miaka mingi, watu wa Algeria wataitumia mara kwa mara, na wataishukuru zaidi na kuwatakia heri na baraka watu wa China."
|