Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-24 16:28:06    
Hekalu la Dazhao lililoko kaskazini mwa ukuta mkuu

cri

Hekalu la Dazhao liko kwenye mji wa zamani wa mji wa Huhehaote, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani. Hekalu la Dazhao lilijengwa mwaka 1580 katika enzi ya Ming ya China. Majengo ya hekalu la Dazhao yalijengwa kwa ufundi mkubwa, kwenye ukumbi mkubwa wa hekalu kuna sanamu ya Sakyamuni iliyotengenezwa kwa fedha, kwa hiyo hekalu hilo pia linaitwa "hekalu la buddha wa fedha". Kuna vitu vingi vya kiutamaduni vilivyohifadhiwa katika hekalu la Dazhao, ambavyo vina thamani kubwa kwa utafiti kuhusu historia na utamaduni wa dini ya kabila la wamongolia.

Majengo yaliyoko kwenye hekalu la Dazhao yalipangwa kama ya mtindo wa mahekalu ya kabila la wahan, hekalu hilo lina eneo la zaidi ya mita za mraba elfu 30, kati yake majengo yanachukua nafasi ya mita za mraba zaidi ya 8,000, majengo muhimu ya hekalu ni pamoja na mlango mkubwa, ukumbi wa mfalme wa peponi, ukumbi wa pili wa pipal, jengo lenye vyumba tisa, ukumbi wa kusomea vitabu vya dini, na ukumbi wenye sanamu za mabudha, kati yake, ukumbi wa kusomea vitabu vya dini unaungana na ukumbi wenye sanamu za mabudha, ambapo panaitwa "Ukumbi Mkubwa", "Ukumbi Mkubwa" ni jengo pekee lenye mtindo unaounganisha jadi za watu wa kabila la wahan na watu wa kabila la watibet, kwenye sehemu ya katikati ya ukumbi wenye mabudha, imewekwa sanamu ya fedha ya Sakyamuni yenye kimo cha zaidi ya mita mbili, mbele ya sanamu ya buddha kuna nguzo kubwa zenye nakshi za dragon, na kwenye kando mbili za sanamu ya buddha ya fedha kuna sanamu za shaba za Zonggeba, Dalai wa tatu na wa nne; mbali na hayo ndani ya hekalu la Dazhao kuna vitu vingi vya zamani vya utamaduni wa dini, hususan sanamu za budhaa za fedha, nakshi za dragon na picha kubwa ziliyochorwa kwenye kuta za hekalu, ambavyo vinaitwa kuwa ni "vitu vitatu maarufu vya hekalu la Dazhao".

Kuhusu umuhimu wa hekalu la Dazhao katika shughuli za utalii za mkoa huo wa Mongolia ya ndani, profesa wa taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Mongolia ya chuo kikuu cha Mongolia ya ndani, Bw. Burenbat alisema,

"Baada ya kuona maelfu kwa makumi ya wanamji wanashiriki kwenye shughuli za dini na gulio la hekalu lenye michezo mingi, nimeona hali ya jamii yenye amani na neema. Hekalu la Dazhao linafanya kazi muhimu katika kurithshai utamaduni wa dini na jadi ya kabila la wamongolia, na ni kivutio kikubwa katika sekta ya utalii ya Mongolia ya ndani."

Mchezo wa ngoma ya "Cha Ma", ambayo ni ngoma ya watu wanaovaa vinyago ya kufukuza mashetani, kusherehekea mavuno mazuri ya kilimo na kuomba baraka katika mwaka unaokuja katika mwezi Januari na Juni ya kalenda ya kilimo ya China kila mwaka, ni mchezo mkubwa wa ngoma za vinyago ambao unachezwa kwenye hekalu la Dazhao. Wakati ule, watawa wanavaa mavazi maalumu na kuvaa vinyago wakijifanya kuwa ni miungu wa aina mbalimbali na kucheza kwa kufuata muziki wa jadi wa dini. Mchezo wa ngoma ya "Cha Ma" ni adimu na wenye uchangamfu mkubwa. Mwondoko wa wachezaji ni wa ajabu na kupendeza.

Katika mchezo wa ngoma ya "Cha Ma", wahusika waliovaa vinyago vya vichwa vya mbawala, maksai na mungu mwenye nyusi nyeupe ni wa kuvutia zaidi, katika midundo mikali ya muziki, wachezaji wakicheza huku wakizungusha upanga na kuwakata washetani. Mtawa wa hekalu la Dazhao Jin Cheng alisema,

"Katika miaka ya karibuni, pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya hekalu la Dazhao, watalii wengi wa nchini na kutoka nchi za nje wanatembelea hekalu hilo wakiwa na shauku kubwa kuhusu mchezo wa ngoma ya "Cha Ma", na shughuli za dini ya kibudha."

Katika miaka michache iliyopita, serikali ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ilitenga fedha nyingi za kufanya ukarabati mkubwa kuhusu hekalu la Dazhao, kuondoa nyumba zenye hali duni wakazi zilizoko karibu na hekalu hilo ili kuonesha uadhimu wa hekalu la Dazhao la zamani. Upande wa magharibi mwa hekalu la Dazhao ni mtaa mmoja uliohifadhiwa vizuri wa enzi za Ming na Qing, nyumba zilizojengwa kwenye kando mbili za mtaa huo zilijengwa kwa matofali na kuezekwa kwa vigae vya rangi ya kijivu, ambazo pembe nne za mapaa ya nyumba ni zenye mtindo wa kuchongoka kwa juu. Katika miaka ya hivi karibuni, filamu za sinema nyingi za kale zilipigwa huko. Vitu vingi vya kiutamaduni vya enzi za zamani, maneno ya hati za mkono, michoro ya sanaa, vyombo vya jade pamoja na michoro iliyochorwa kwenye ngozi pamoja na vyombo vya shaba vilivyotengenezwa kwa kazi za mikono vya kabila la wamongolia ni maarufu zaidi.

Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya watalii wanaotembelea hekalu la Dazhao imekuwa inaongezeka kwa mfululizo. Mtalii Cui Jin anaona kuwa utamaduni wa dini ni moja ya sababu muhimu zinazowavutia watalii kwenda kutembelea huko, alisema,

"Kwani nilitembelea sehemu nyingine, kuhusu maendeleo ya dini ya kibudha, wamechapisha vitabu vingi, na wametoa mchango halisi wa kuendeleza dini ya kibudha. Wameeneza utamaduni wa huko kwa sehemu nyingine na kufanya watu wafahamu zaidi utamaduni wao, wamekusanya maandishi yote kuhusu historia za mahekalu ya huko ili kuwafahamisha watu kuwa huu ndio utamaduni, ni mabaki ya utamaduni."

Idhaa ya kiswahili 2008-03-24