Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-24 16:52:55    
Wajumbe wa makabila madogo madogo wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China wazungumzia maendeleo ya sehemu ya magharibi mwa China

cri

Mkutano wa mwaka huu wa baraza la awamu mpya la mashauriano ya kisiasa la China umefungwa hivi karibuni hapa Beijing, kwenye mkutano huo baadhi ya wajumbe kutoka makabila madogo madogo waliisifu sana serikali kuu ya China kwa kuchukua hatua za kuhimiza maendeleo ya sehemu za makabila madogo madogo.

China ni nchi yenye makabila mengi, na idadi ya watu wa makabila madogo madogo imefikia zaidi ya milioni 100. Kutokana na sababu za historia, maumbile na jamii, sehemu za makabila hayo hazijaendelezwa vizuri. Watu wa makabila madogo madogo nchini China hasa wanaishi kwenye sehemu ya magharibi. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imekuwa inachukua hatua mbalimbali ili kuhimiza maendeleo ya sehemu hiyo. Bw. Daimik Diwana wa kabila la Watajik ni mjumbe wa baraza la awamu mpya la mashauriano ya kisiasa la China, na anatoka mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang. Alisema ingawa anaishi kwenye sehemu ya mbali, lakini sasa watu wa huko wamepata maisha mazuri kama watu wa sehemu nyingine nchini China, hasa tatizo la kupata matibabu limeondolewa. Alisema,

"Sasa serikali inalipa zaidi ya asilimia 70 ya gharama za matibabu kwa wakulima na wafugaji, na wao wanalipa asilimia ndogo tu."

Zamani wakulima na wafugaji wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur hawakuhudumiwa na mfumo wa huduma za matibabu, na walipopatwa na ugonjwa walilipa gharama zote za matibabu wao wenyewe. Kutokana na gharama hiyo ni kubwa, watu hao hawaendi hospitali hata wakipatwa na maradhi madogo wa kawaida. Lakini sasa serikali ya China imeanzisha mfumo mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini, na kuwapatia wakulima na wafugaji ruzuku ya matibabu. Hatua hiyo iliwapunguzia mzigo kwa kiasi kikubwa, na wakulima na wafugaji wengi siku hadi siku wamepata manufaa. Imefahamika kuwa mwaka huu mfumo wa aina mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini utawahudumia wakulima na wafugaji wote mkoani Xinjiang, ambapo mfumo huo utawanufaisha watu zaidi ya milioni 9 kwenye mkoa huo.

Mjumbe mwingine Bw. Qianjing alitoka kabila la Waluoba, na anaishi kwenye wilaya ya Milin ya mkoa unaojiendesha wa Tibet. Alijulisha kuwa, kiwango cha matibabu mkoani Tibet kimeinuka sana ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita. Serikali ya mkoa huo ilijenga hospitali kwenye sehemu za makazi ya watu, pia ilifanya juhudi kubwa ili kuhifadhi dawa na matibabu yenye umaalumu wa kabila la Watibet, na juhudi hizo pia zimeleta fursa mpya ya kujipatia maendeleo kwa wilaya ya Milin inayozalisha malighafi ya dawa. Bw. Qian Jin alisema,

"Kwenye wilaya yetu, kuna dawa nyingi za mitishamba. Sasa wilaya yetu inaendeleza shughuli za upandaji wa mitishamba. Viwanda vya kutengeneza dawa za kitibet, makampuni ya biashara ya dawa na hospitali ya matibabu ya kitibet zinakuja kununua malighafi ya dawa mara kwa mara.

Wakati mkutano wa kila mwaka wa baraza la mashauriano ya kisiasa unapofanyika nchini China, wajumbe wa baraza hilo wanatoa maoni na mapendekezo kuhusu sera za kitaifa na masuala yanayofuatiliwa na wananchi, na mashauri na mapendekezo kuhusu sehemu ya makabila madogo madogo yamesukuma mbele maendeleo ya sehemu hiyo. Bw. Luosang Danbainima ni budha mhai wa hekalu ya Lalu ambayo ni hekalu kubwa zaidi kwenye sehemu ya Linzhi mkoani Tibet, yeye amekuwa mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa kwa miaka mingi. Miaka kadhaa iliyopita Bw. Luosang kwenye mkutano wa baraza hilo alipendekeza kujengwa uwanja wa ndege kwenye sehemu ya Linzhi, na ujenzi wa uwanja huo ulikamilika mwaka jana. Alisema,

"Sasa uwanja wa ndege umejengwa kwenye sehemu ya Linzhi, wakati huohuo reli ya Qinghai-Tibet pia ilizinduliwa. Sasa ni rahisi kwa watu kusafiri kati ya Tibet na Beijing, Guangdong na Fujian. Watu wengi wanakuja kufanya utalii mkoani Tibet na kwenye sehemu ya Linzhi. Na biashara za watibet zinaendelezwa vizuri, na watu wa Tibet wanafurahi sana."

Serikali ya China pia inatilia maanani sana suala la elimu kwenye sehemu ya makabila madogo madogo. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kwenye mkutano wa mwaka huu wa baraza la mashauriano ya kisiasa alifanya majumuisho kuhusu kazi za serikali katika miaka mitano iliyopita akisema,

"Katika miaka hiyo mitano, China ilitenga yuan trilioni 2.43 kwa ajili ya shughuli za elimu, na pesa hizo zimeongezeka kwa asilimia 126. Lengo la kueneza elimu ya lazima ya miaka tisa na kuondoa kimsingi idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika limetimiza, na tumepiga hatua kubwa katika kutuimiza haki ya kupata elimu."

Mjumbe wa mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa Bw. Eyitai wa kabila la Wakorea ambaye ni mkuu wa Chuo Kikuu cha Makabila Cha China. Alisema kanuni ya chuo hicho kuwaandikisha wanafunzi inaonesha haki ya usawa kati ya watu wa makabila mbailmbail nchini China. Alisema,

"Wanafunzi wanaosoma kwenye Chuo Kikuu cha Makabila wanatoka makabila 56 nchini China, na wengi wao wanatoka kwenye sehemu za mbali za makabila madogo madogo ikiwemo mikoa ya Xinjiang na Tibet. Tumeandaa mazingira mazuri ya kutoa elimu na kuongeza uwezo kwa wanafunzi hao."

Mjumbe mwingine Bw. Zhou Mingfu aliyekuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya mambo ya makabila ya China aliwahi kufanya kazi kwa miaka minane kwenye sehemu ya makabila madogo madogo, ambapo alijionea mabadiliko makubwa yaliyotokea kwenye sehemu hiyo. Alisema,

"Hali ya wilaya maskini inabadilika siku hadi siku, majengo mengi yenye ghorofa na barabara nzuri zimejengwa kwenye wilaya hizo. Sasa ingawa umaskini bado haujaondolewa kabisa, lakini umepungua kwa kiasi kikubwa."

Idhaa ya kiswahili 2008-03-24