Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-26 20:50:50    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na pilipili mboga

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 200, pilipili mboga gramu 50, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, sosi ya chaza kijio kimoja, wanga vijiko viwili, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja

Njia

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, koroga pamoja na mchuzi wa sosi, sukari, na wanga. Kata pilipili mboga iwe vipande.

2. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya nyama ya ng'ombe korogakoroga halafu vipakue.

3. washa moto tena, halafu tia vipande vya nyama na pilipili mboga korogakoroga, tia mvinyo wa kupikia, sosi ya chaza, chembechembe za kukoleza ladha korogakoroga halafu mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga na ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.