Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-02 22:11:10    
Mapishi ya miguu ya nguruwe

cri

Mahitaji: Miguu ya nguruwe gramu 500, sukari vijiko viwili, pilipili manga kijiko kimoja, vitunguu maji na tangawizi kila gramu 5, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mafuta ya ufuta vijiko vinne.

Njia:

1. chemsha maji, weka miguu ya nguruwe kwenye maji, baada ya kubadilika rangi, ipakue.

2. kata vitunguu maji na tangawizi viwe vipande vipande.

3. mimina mafuta ya ufuta kwenye sufuria, halafu tia sukari, korogakoroga, tia miguu ya nguruwe korogakoroga kwa haraka, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, pilipili manga korogakoroga,mimina mchuzi wa sosi , mvinyo wa kupikia, korogakoroga, halafu mimina maji, baada ya kuchemka, punguza moto, endelea kuchemsha mpaka maji yaondoke, yapakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.