Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-02 22:02:52    
Majadiliano kuhusu mada maalumu kuhusu kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yafanyika

cri

Majadiliano ya siku mbili ya mada maalum kuhusu kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yanafanyika kuanzia tarehe 1 Aprili kwenye Baraza kuu la 62 la Umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wanajadili hasa namna ya kuhimiza malengo ya maendeleo ya milenia yatimizwe mapema iwezekanavyo.

Mwezi Septemba mwaka 2000, kwenye Mkutano wa wakuu uliofanyika kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi mbalimbali duniani walipitisha "Tangazo la milenia", wakiahidi kwa makini kwamba, malengo halisi manane ya maendeleo kama vile kutokomeza hali mbaya kabisa ya umaskini na njaa, kueneza elimu ya msingi, na kuhakikisha maendeleo endelevu yatatimizwa ndani ya miaka 15. Aidha kwa mara ya kwanza tangazo hilo pia limetambua wazi kuwa mambo ya maendeleo yanayohusiana moja kwa moja na amani na usalama wa dunia, na kuthibitisha kazi ya kufanya ushirikiano wa pande mbalimbali ili kuhimiza maendeleo ya pamoja kuwa ni jukumu kuu la nchi mbalimbali. Hivi sasa muda wa kutimizwa kwa malengo ya milenia umepita kwa nusu, nchi mbalimbali ziko katika hali mbalimbali tofauti ya utimizaji wa malengo ya milenia. Wakati huo huo masuala kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kupanda kwa bei ya vyakula na mambo ya uchumi wa dunia yanaendelezwa polepole yameleta changamoto mpya kwa juhudi za kutimiza malengo ya milenia. Katika hali hiyo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon aliamua kuendesha mwenyewe Mkutano wa ngazi ya juu mwezi Septemba mwaka huu wakati wa Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, ili kutia nguvu mpya ya uhai kwa ajili ya kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Majadiliano ya siku mbili yanayofanyika sasa yanalenga kukusanya maoni ya pamoja, kukumbusha mafanikio yaliyopatikana, na kutambua changamoto mbalimbali, na kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya Mkutano wa ngazi ya juu utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa majadiliano hayo alidhihirisha kuwa, hivi sasa maendeleo kadha wa kadha yamepatikana katika juhudi za jumuiya ya Kimataifa za kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, ambapo kila mwaka maisha ya watoto milioni 3 yanaokolewa, na idadi ya watu wanaopokea matibabu ya ugonjwa wa ukimwi pia imeongezeka kwa milioni 2. Lakini hivi sasa hali ya maendeleo ya dunia nzima bado si ya uwiano, hasa hali ya umaskini kwenye sehemu ya Afrika kusini mwa Sahara ni mbaya zaidi, kama hali ya hivi sasa inaendelea vivyo hivyo, sehemu hiyo haitaweza kutimiza lengo lolote kati ya malengo manane ya maendeleo ya milenia.

Ili kuisaidia Afrika iharakishe maendeleo, mwezi Septemba mwaka jana Bw. Ban Ki-moon aliendesha mwenyewe kazi ya kuanzisha kikundi cha kuelekeza Afrika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, na kutaka kupitia kazi hiyo kuhamasisha jumuiya ya Kimataifa iisaidie Afrika. Hivi sasa kikundi hicho kimependekeza kuanzisha "mapinduzi ya kijani ya Afrika" ili kuharakisha ongezeko la uchumi, na kutokomeza hali ya njaa, ambapo nchi mbalimbali za Afrika zingetumia vyakula vilivyotengenezwa kwenye sehemu mbalimbali za nchi za Afrika kutoa chakula kwa shule ili kuhakikisha hali ya uwiano ya virutubisho kwa watoto. Aidha kikundi hicho kinapendekeza kufanya uwekezaji kwenye miundo mbinu, ili kuinua tija na kuyafanya mambo ya uchumi wa Afrika yajiunge mapema iwezekanavyo na mambo ya uchumi wa dunia nzima. Bw. Ban Ki-moon ana matumaini kuwa, mwaka 2008 ungekuwa mwaka muhimu wa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, na kuwa mwaka wa kufuatilia maendeleo ya idadi ya watu wapatao bilioni moja ambao ni wenye hali ya umaskini zaidi kuliko wengine kote duniani.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, kutokana na migogoro ya kisehemu na shughuli za ugaidi zinazofanyika kwenye sehemu mbalimbali duniani, katika miaka mingi iliyopita, kwa ujumla jumuiya ya Kimataifa ilizingatia zaidi usalama na kupuuza maendeleo, hivi sasa Umoja wa Mataifa unajaribu kubadilisha hali hiyo. Mikutano mbalimbali iliyofanyika kwenye Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa, wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na jumuiya zinazohusika za Kimataifa walipohotubia wote walieleza maoni ya pamoja kuhusu mambo ya usalama na maendeleo yanahusiana, kama hakuna maendeleo, usalama wa dunia hautadumishwa.