Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-03 15:45:49    
Mji wa Taiyuan China wastawisha soko la utamaduni kwa michezo iliyo bora ya sanaa

cri

Mkoa wa Shanxi ni chimbuko la opera ya jadi nchini China. Opera maarufu ya "Msichana Mwenye Nywele Nyeupe" iliyotungwa katika miaka ya 40 ya karne iliyopita ndio iliyotungwa kwa msingi wa opera ya jadi ya mkoa huo. Katika miaka ya hivi karibuni, mji mkuu wa mkoa huo, Taiyuan, umeanza kustawisha soko la utamaduni kwa michezo iliyo bora na umepata mafanikio dhahiri.

Mliyosikia ni opera ya kimkoa ya Shanxi inayoitwa "Fu Shan Aingia Mjini Beijing". Mwaka 2007 michezo mingi iliyo bora ilitungwa mjini humo, makundi makubwa matano ya opera yalitunga opera zaidi ya 20 na kufanya michezo ya sanaa istawi sana. Kwa kutumia fursa ya kuadhimisha mwaka wa 400 wa kuzaliwa kwa Bw. Fu Shan aliyekuwa mwanautamaduni mkubwa wa mkoa wa Shanxi kundi moja la opera liliwaalika wahariri na waongoza opera wengi kutunga opera iitwayo "Fu Shan Aingia Mjini Beijing". Ofisa wa idara ya utamaduni ya mji wa Taiyuan Bw. Wang Hongwei alieleza,

"Tuliwaalika mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii la Mkoa wa Fujian, mhariri maarufu wa opera Bw. Zheng Huaixing na mwongoza opera mashuhuri Shi Yukun na kuunda jopo la utungaji wa opera hiyo, na muziki wa opera hiyo ulitungwa na mwanamuziki mkubwa wa opera ya Kishanxi, waigizaji ni wa kundi letu. Opera hiyo imekusanya watu wengi hodari wa nchini China."

Opera inayoitwa "Fu Shan Aingia Mjini Beijing" iliwahi kushiriki kwenye mashindano ya opera nchini China kwa mara nyingi na imepata tuzo ya Chuo cha Taaluma ya Opera ya China. Mwigizaji mkuu wa opera hiyo Bi. Xie Tao ni naibu mkuu wa Kundi la Opera la Taiyuan, anafahamu mchakato mzima wa kupatikana kwa opera hiyo. Alisema,

"Opera inayoitwa 'Fu Shan Aingia Mjini Beijing' ilianza kuoneshwa jukwaani mwezi Januari mwaka 2007, hadi sasa imeoneshwa kwa mwaka mzima. Katika muda huo wa mwaka mzima tulihariri na kurekebisha mara sita, na kila baada ya kuoneshwa tunaomba ushauri kutoka kwa wataalamu kisha tuliikamilisha ili kupata opera iliyo bora kabisa na kuwafanya watu wakumbuke zaidi mkoa wa Shanxi na wajue mji wa Taiyuan."

Bw. Fu Shan alikuwa ni mwanafikra, mwanafasihi, msanii wa kuandika maandishi ya Kichina kwa brashi ya wino na mganga mashuhuri katika karne ya 16, sasa mafanikio ya utafiti uliofanywa kuhusu Bw. Fu Shan yamekuwa aina moja ya utamaduni katika shughuli za biashara. Uchumi wa mambo ya utamaduni hauwezi kuendelezwa bila bidhaa za kiutamaduni. Naibu mkuu wa Idara ya Matangazo ya Redio na Televisheni Bw. Cao Yongming alisema, kwa kutegemea mabaki mengi ya kiutamaduni, hivi karibuni mji wa Taiyuan umetunga michezo mingi ya sanaa, kwa mfano opera ya dansi ya "Gao Moja la Tende", muziki wa simfoni wa "Ukoo wa Qiao" na matamasha ya nyimbo za mkoani Shanxi na kadhalika, yote hayo yanatokana na kuwa maliasili za kiutamaduni hazikutumika, sasa zimekuwa bidhaa zinazostawisha uchumi. Bw. Cao alisema,

"Katika muda wa miaka miwili tumeshiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya utamaduni mjini Beijing kwa miradi zaidi ya mia moja ya utamaduni, thamani ya mikataba imefikia Yuan bilioni moja. Tunaimarisha soko la utamaduni kwa kuwavutia wafanyabiashara na mitaji, na uchumi wa sekta ya kiutamaduni unaokua kwa 10% hadi 15% kila mwaka."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-03