Mazungumzo ya siku 5 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kufanyika huko Bangkok, Thailand, wajumbe 1200 kutoka nchi 163 wanahudhuria Mkutano huo. Mkutano huo unajadili hasa namna ya kutekeleza "mpango wa Bali" uliopitishwa mwaka jana kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Tarehe 2 kwenye Mkutano huo wa siku ya tatu, wajumbe wa jumuiya mbalimbali zisizo za kiserikali walieleza kuwa watahimiza serikali za nchi zao kuchukua hatua, ili kuhimiza mazungumzo hayo yenye taabu yapate maendeleo. Mjumbe wa "Mtandao wa utekelezaji wa hali ya hewa duniani" Bw. Chris Henschel alisema:
"Mimi natoka Canada, kuongezeka kwa joto duniani kunatishia mfumo wa viumbe kwenye nchi kavu na bahari nchini Canada, barafu za ncha ya kaskazini zinayeyuka, na maliasili yetu ya nishati ya gesi inabadilika kuwa carbon dioxide, lakini tukilinganishwa na nchi nyingine nyingi za visiwa na nchi zilizoko nyuma kimaendeleo, nchi hizo zinakabiliwa na tishio kubwa zaidi. Ili kuhudhuria Mkutano huo, nilitembelea nchi nyingi, matembezi yangu yamenifanya nijisikie zaidi kuwa Canada ni nchi tajiri. Tuna matumaini kuwa nchi zilizoendelea zitabeba wajibu wa dunia nzima, na kutambua hali mbaya ya hivi sana. Mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia nchi zilizoendelea, vilevile yanatishia nchi nyingi wenzi wao.
Habari zinasema kuwa, wajumbe 229 wa jumuiya 65 zisizo za kiserikali wote wakiwa wachunguzi wamehudhuria Mkutano huo. Wajumbe hao wa jumuiya zisizo za kiserikali wanafanya mawasiliano ya karibu sana, walitoa hotuba kila mara kwenye Mkutano, wakati wa mapumziko ya Mkutano huo, walitawanya data mbalimbali zinazohusika, ili kueleza matumaini yao ya kuhimiza mazungumzo hayo ya Umoja wa Mataifa yaweze kupata matokeo mapema iwezekanavyo.
Mjumbe wa Mfuko wa mazingira ya maumbile duniani ambayo ni jumuiya maarufu isiyo ya kiserikali duniani inayoshughulikia uhifadhi wa mazingira Bibi Kathrin Gutmann, alipohojiwa na waandishi wa habari aliikosoa vikali nchi fulani iliyoendelea kurudi nyuma katika suala la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema ili kufikia makubaliano mapya kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, nchi zilizoendelea zinapaswa kufuatilia zaidi maslahi ya dunia nzima. Alisema:
"Naona tunafanya kazi muhimu, kwani kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa tunafuatilia zaidi tunatakiwa kufanya nini, na hali ya namna gani itatokea; lakini serikali za nchi mbalimbali zinazingatia zaidi maslahi ya nchi zao, na kufuatilia zingeweza kufanya nini, na zinafuatilia masuala halisi ya kisiasa. Lakini kwa kawaida, upeo wa serikali huwa ni mfupi. Hivyo kazi tunayofanya ni kuzihimiza zipanue upeo wao, na kuzisaidia kutambua zinatakiwa kufanya nini, na zinaweza kufanya nini".
Bibi Gutmann kwenye mazungumzo hayo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, alisema nchi zilizoendelea kama vile Japan na New Zealand zilieleza maoni yao ya ajabu au kusisitiza zaidi mambo madogomadogo, msimamo huo hausaidii dunia nzima kukabiliana pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa. Nchi zilizoendelea zinapaswa kufuatilia namna ya kupunguza kihalisi utoaji wa hewa zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa joto duniani, na wakati huo huo zitoe misaada halisi ya kiteknolojia na kifedha kwa nchi zinazoendelea. Kuhusu umuhimu wa jumuiya zisizo za kiserikali katika suala la dunia nzima kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, naibu Mkurugenzi wa kitivo cha mazingira katika chuo kikuu cha umma cha China Bw. Zou Ji alisema:
"Katika mfumo wa usimamizi wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa, jumuiya zisizo za kiserikali zinaweza kuonesha umuhimu wake ambao hauwezi kuchukuliwa na jumuiya nyingine. Jumuiya hizo zinaweza kufanya kazi nyingi za kuhimiza juhudi za nchi na watu, hasa kueleza sauti ya wananchi, kueleza ufuatiliaji wa watu kwa maslahi ya umma. Kwani masuala ya mazingira na hali ya hewa yanahusiana na mali za umma kote duniani, lazima kuwe na watu wanaotoa madai. Naona jumuiya zisizo za kiserikali zinaweza kufanya kazi nzuri kuhusu masuala hayo. Jumuiya kadha wa kadha zisizo za kiserikali zina uwezo mkubwa wa kuwashirikisha watu, kiwango chao cha taaluma ni cha juu, zinaweza kusaidia utatuzi wa masuala".
|