Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-07 16:19:23    
Mtaalamu hodari wa jiolojia kutoka kabila la Watibet Bw. Duo Ji

cri

Bw. Duo Ji alizaliwa kwenye familia moja ya wakulima iliyoishi katika sehemu ya mbali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet. Mwaka 1974 Bw. Duo Ji alikwenda nje ya kijiji na wazazi wake hawajawahi kutoka nje ya kijiji hicho hata mara moja, na kuanza kusoma kozi ya jiolojia kwenye chuo kikuu kimoja cha mji wa Chengdu ulioko kusini magharibi mwa China. Mwaka 1978 alihitimu masomo yake na kuajiriwa na ofisi ya utafiti wa jiolojia na joto ardhini ya Tibet, na kuanza kazi ya utafiti wa jiolojia. Alipozungumzia sababu ya kuchagua kozi ya jiolojia, alisema,

"Nilipokuwa mdogo, niliwaona wanasayansi wengi waliokuja kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet kufanya kazi ya utafiti, nilianza kupenda sayansi ya jiolojia. Nilipokuwa kijana, nilidhani kuwa nilizaliwa kwenye mkoa wa Tibet wenye umaalumu mkubwa wa jiolojia, hivyo nilichagua kozi hiyo."

Katika miaka karibu 30 iliyopita tangu aanze kufanya kazi ya jiolojia, ili kutafuta maliasili ya joto chini ya ardhi, kutoka kwenye sehemu isiyo na watu iliyoko kaskazini mwa mkoa wa Tibet hadi kufikia milima mirefu pamoja na magenge yaliyoko kusini mwa mkoa huo, kutoka mabaki ya kale hadi kufikia misitu ya asili, Bw. Duo Ji alitembelea karibu sehemu yote mkoani Tibet, na kupata mafanikio makubwa katika kazi yake.

Sasa Bw. Duo Ji amekuwa mtaalumu maarufu wa jiolojia nchini China na duniani, pia ni mjumbe wa kwanza wa mkoa wa Tibet wa taasisi ya uhandisi ya China. Mwaka jana alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa 17 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Mafanikio makubwa aliyopata yanatokana na tabia yake nzuri, yaani kuwa hodari katika utafiti na udadisi, na kutoogopa matatizo.

Eneo lenye joto chini ya ardhi la Yangbajing lililoko kwenye wilaya ya Dangxiong mkoani Tibet, ni eneo kubwa zaidi lenye joto chini ya ardhi nchini China. Eneo hilo ni maarufu sana duniani, na wakati wa miaka ya 90 ya karne iliyopita, wataalamu kutoka nchini China na nchi za nje walialikwa kuchunguza malimbikizo ya joto chini ya ardhi kwenye eneo hilo, wengi wao waliona kuwa chini ya eneo la Yangbajing kuna joto tu, hakuna maji ya moto yanayoweza kuchimbwa na kutumiwa. Lakini Bw. Duo Ji kwa kutegemea uzoefu wake alichunguza vizuri umaalumu wa eneo hilo, na kuona kuwa eneo hilo lina maji ya moto ya kutosha. Utafiti ulithibitisha maoni ya Bw. Duo Ji, na kazi ya uchunguzi wa eneo hilo iliyoendeshwa naye ilipata mafanikio makubwa. Lakini wakati wa kuchimba kisima kirefu, Bw. DuoJi pamoja na wenzake walikumbwa na matatizo mengi. Alisema,

"Wakati huo China hakukuwa na uzoefu wa utafutaji na uchimbaji wa joto chini ya ardhi, kutokana na matendo makali ya miundo ya jiolojia chini ya eneo la Yangbajing, tulipochimba kisima tulikumbwa na matatizo mengi. Lakini sikuwa na mashaka juu ya maoni yangu kwamba kuna maji ya moto chini ya eneo hilo."

Kwa kukabiliwa na matatizo hayo yaliyodhaniwa kuwa hayawezi kutatuliwa, Bw. Duo Ji alifanya uchambuzi na utafiti kwa makini juu ya miundo ya kijiolojia ya eneo la Yangbajing, na kwa kutumia uzoefu aliopata kwa kupitia kufanya kazi kwa miaka mingi na teknolojia aliyojifunza kutoka nchi za nje, alitatua matatizo hayo moja baada ya lingine. Mwishoni kisima kirefu kilifanikiwa kuchimbwa, na kazi ya utafutaji wa joto chini ya ardhi ya China ilipiga hatua kubwa. Hivi sasa kisima hicho kimekuwa kisima chenye joto kubwa zaidi na kinachotoa maji ya moto mengi zaidi nchini China. Mafanikio ya eneo la Yangbajing pia ni muhimu sana kwa shughuli za utafutaji na matumizi ya joto chini ya ardhi nchini China. Bw. Duo Ji alisema,

"Mafanikio ya eneo la Yangbajing ni mfano mzuri kwa sehemu nyingine zenye maliasili ya joto chini ya ardhi ikiwemo mikoa ya Yunnan na Sichuan na sehemu kando ya bahari nchini China, na ni muhimu sana kwa juhudi za kueneza matumizi ya joto chini ya ardhi nchini China katika siku zijazo."

Mara kwa mara Bw. Duo Ji anafanya kazi nje ya miji, lakini anapenda sana kazi yake. Alisema,

"Watu wengi wanaona kuwa kazi ya jiolojia ni ngumu sana, lakini kwa kweli kazi hiyo pia imejaa furaha, na inawafanya watu waipende siku hadi siku. Ninapenda milima na uwanda wa juu, sitaki kufanya kazi kwenye ofisi yenye raha mjini."

Katika miaka mingi iliyopita, Bw. Duo Ji alifanya kazi nyingi katika utafiti wa joto chini ya ardhi, na kupata mafanikio makubwa. Alisifiwa na wataalamu wengine wa utafiti huo wa nchini na nchi za nje, na kwa nyakati tofauti alipewa heshima za Mfanyakazi Mzuri wa Shughuli za Jiolojia na Madini Nchini China na Mtu Hodari mwenye uwezo wa Teknolojia Nchini China. Lakini Bw. Duo Ji alisema,

"Mafanikio yangu yanatokana na mafunzo ya Chama cha Kikomunisti cha China na serikali, pia kuna watu wengi wema wamenisaidia. Kwa bahati nzuri nina wafanyakazi wenzangu hodari, mafaniko hayo yalipatikana kutokana na juhudi za sisi sote. Nitafanya bidii ili kutoa mchango mkubwa zaidi."

Bw. Duo Ji aliwahi kupata fursa nyingi ya kufanya kazi kwenye nchi za nje. Wakati alipokuwa anasoma nchini Marekani, wataalamu wengi wa nchi hiyo walimtaka afanye kazi nchini humo wakiahidi kumpa mshahara mkubwa, lakini alikataa, alisema,

"Sababu yangu ni rahisi, kwa kuwa mimi ninapenda taifa langu. Nilisaidiwa na Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa nchi hiyo. Ninapenda taifa la China na maskani yangu. Nilikwenda kusoma nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi wa mkoa wa Tibet, na baada ya kukamilisha masomo, lazima nirudi nyumbani."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-08