Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-08 15:55:03    
Kwa nini majeshi ya Marekani na Iraq yamelishambulia "jeshi la Mehdi"

cri

Hivi karibuni jeshi la Marekani na jeshi la usalama la Iraq yalifanya mashambulizi mfululizo dhidi ya jeshi la wanamgambo la "Mehdi" la madhehebu ya Shia katika sehemu ya Basra, sehemu ya kusini ya Iraq. Mashambulizi hayo yaliyoanza tarehe 25 Machi sasa yameingia katika wiki ya tatu. Baada ya wiki moja tokea mashambulizi hayo yalipoanzishwa tarehe 25 pande mbili ziliwahi kusimamisha mapambano. Waziri mkuu wa Iraq Bw Nouri al-Maliki alitoa onyo la mwisho akitaka wanamgambo wasalimishe silaha zao kabla ya tarehe 8 mwezi huu, na serikali itatoa fidia ya fedha. Lakini siku mbili kabla ya muda kufikia mwisho majeshi ya Marekani na Iraq kwa mara nyingine tena yalifanya mashambulizi, pande mbili zilipambana vikali mjini Sadr na kusababisha vifo vya watu 22 na kati yao watu 9 waliuawa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la anga la Marekani na watu 55 walijeruhiwa. Tarehe 7 majeshi hayo yalishambulia makazi ya wafuasi wa madhahebu ya Shia, kusini mwa Baghdad, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 10 na wengine 50 kujeruhiwa. Zaidi ya hayo askari kiasi cha 150 hivi wa Uingereza waliorudi kwenye mji muhimu wa Basra pia walishiriki kwenye mapambano hayo dhidi ya "jeshi la Mehdi".

Cha kuvutia zaidi ni kuwa tarehe 6 waziri mkuu wa Iraq alisema anataka kuvunja "jeshi la Mehdi" linaloongozwa na Moqtada al-Sadr, ama sivyo "harakati za Sadr" zinazoongozwa naye zitapigwa marufuku kushiriki kwenye mchakato wa kisiasa wa Iraq. Aidha alisema operesheni inayofanyika kote nchini dhidi ya vikosi haramu itaendelea mpaka mwisho. Wachambuzi wanaona kuwa mashambulizi hayo ya majeshi ya Marekani na Iraq yanatokana na sababu mbili. Kwanza uchaguzi wa serikali za mitaa umekaribia, serikali ya Nouri al-Maliki inataka kudhibiti ushawishi wa "hatakati za Sadr" ili sehemu ya kusini ya Iraq isiangukie mikononi mwa Sadr. Kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa kukaribia mapambano ya kugombea uongozi wa serikali za mitaa yamekuwa makali. Kundi la "Harakati za Sadr" lilitumia fursa ya majeshi ya Marekani na Iraq kupambana na vikosi vya Al-Qaida karibu na Baghdad na sehemu ya kaskazini ya Iraq, kueneza ushawishi wake katika sehemu ya kusini ya Iraq, na Bw. Muqtada al-Sadr alitaka kuwashawishi watu wa Iraq wafanye maandamano ya watu milioni moja katika tarehe 5, siku ya kuadhimisha miaka mitano tokea jeshi la Marekani liingie nchini Iraq. Pili, mashambulizi hayo yanalenga kuvunja jeshi la wanamgambo na kuleta nafasi ya usuluhishi wa kitaifa. Mwaka 2003 baada ya serikali ya Saddam kupinduliwa, jeshi la Marekani lilivunja jeshi la serikali ya Iraq, askari na maofisa laki kadhaa waliopoteza mapato walijiunga na vikosi vya kisehemu, vikundi vingi vya wanamgambo vimeimarika. "Jeshi la Mehdi" lenye askari elfu 60 limekuwa jeshi lenye nguvu kubwa kati ya vikosi vya wanamgambo nchini Iraq, na "harakati za Sadr" ni chama pekee kinachopinga kuvunjwa kwa vikosi vya wanamgambo. Kama "jeshi la Mehdi" likiweza kuvunjwa inamaanisha kuwa kikwazo kikuu kwenye mchakato wa upatanishi wa kitaifa kitaondolewa.

Lakini ukweli ni kwamba mashambulizi ya serikali ya Iraq dhidi ya "jeshi la Mehdi" yamempatia Bw. Nouri al-Maliki uungaji mkono mkubwa. Vikunvi vyote vya kisiasa licha ya "hatakari za Sadr" tarehe 5 Aprili vilitoa taarifa ya pamoja yenye vipengele 15 ikitaka vyama vyote vya kisiasa vivunje vikosi vyao kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Lakini vyombo vya habari vinaona kuwa kama majeshi ya Marekani na Iraq yakishindwa kudhibiti hali ya mapambano na kupunguza vifo vya watu wasio na hatia, hali ya usalama itazidi kuwa mbaya na yataharibu juhudi za usuluhishi wa kitaifa.

Idhaa ya kiswahili 2008-04-08