Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-09 16:14:42    
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan kutembelea China

cri

Kutokana na mwaliko wa rais wa China Hu Jintao, rais Pervez Musharraf wa Pakistan atafanya ziara ya siku 6 nchini China kuanzia tarehe 10. Tarehe 8 alizungumza na waandishi wa China kuhusu ziara yake. Rais Pervez Musharraf tarehe 10 Aprili atafika mjini Sanya mkoani Hainan kisha atahudhuria mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Boao la Asia mwaka 2008 na kufanya mazungumzo na rais wa China Bw. Hu Jintao. Alipozungumzia lengo la ziara yake alisema,

"Lengo la ziara yangu ni kuimarisha uhusiano kati ya Pakistan na China na kuimarisha maingiliano kati ya viongozi wa nchi hizi mbili. Zaidi ya hayo tutazungumza kuhusu mambo ya ulinzi wa taifa, uchumi na mambo mengine, na vile vile nitazungumza nao kuhusu miradi ya ushirikiano inayotekelezwa na itakayoanzishwa".

Kwenye mazungumzo Bw. Pervez Musharraf alifurahia urafiki mkubwa wa miaka mingi uliopo kati ya nchi yake na China na kuwa na matumaini kuwa urafiki huo utazidi kuimarika. Alisema,

"Uhusiano mzuri kati ya Pakistan na China ni wa miaka mingi na urafiki una msingi imara. Uhusiano wa nchi hizi mbili kisiasa na kwenye sera za kidiplomasia ni mzuri, kuhusu masuala ya kimataifa zina mitazamo inayolingana, na uhusiano wa kibiashara unachukua nafasi muhimu katika uhusiano wa pande mbili."

Kutokana na maingiliano makubwa ya kibiashara yaliyopo kati ya nchi hizo mbili, makampuni yanayowekeza nchini Pakistan yamekuwa yanaongezeka. Bw. Pervez Musharraf alisema, Pakistan inakaribisha wawekezaji wa nje kuanzisha shughuli zao na imewawekea mazingira mazuri ya uwekezaji. Alisema Pakistan inathamani sana uhusiano wa kiuchumi na China na imetoa sera za kipaumbele kwa wawekezaji wa China. Alisema,

"Pakistan imewawekea miundombinu wawekezaji wa China, tumeanzisha sehemu za viwanda katika miji ya Gwadar na Lahore. Wawekezaji wa China wanakaribishwa sana nchini Pakistan na wananufaika na sera nyingi za kipaumbele."

Licha ya nyanja za uchumi, Bw. Musharraf alisema nchini hizo mbili pia zinaweza kushirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi. Alisema,

"Njia nzuri ya kukomesha ugaidi ni kutatua migongano ya kisiasa ya kimataifa, na China inaweza kutoa mchango mkubwa kwenye suala hilo. Zaidi ya hayo umaskini na ujinga pia vinachangia kuendeleza ugaidi na siasa kali, kwa hiyo Pakistan inahitaji msaada wa China katika kuendeleza elimu, kuondoa umaskini na kustawisha uchumi wa jamii."

Alisema Pakistan na China zina maslahi ya pamoja katika mapambano dhidi ya ugaidi, na Pakistan itaunga mkono kwa pande zote mapambano ya China dhidi ya magaidi wa kundi a Turkemenstan ya mashariki.

Rais Musharraf pia aliwaambia waandishi wa habari kuwa, nchi mbili zitasukuma mbele kwa pamoja elimu nchini Pakistan kwa kuanzisha vyuo vikuu, na katika ushirikiano wa miradi mikubwa ya barabara inayosifiwa kama ni miradi ya ajabu duniani imekuwa njia ya kuunganisha nchi hizo mbili, na hivi sasa barabara hiyo imekuwa ikipanuliwa, mradi mwingine ni ujenzi wa bandari wa Gwadar ambao utazinufaisha pande zote mbili. Na kuhusu mustakbali wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili Bw. Musharraf alisema urafiki wa nchi hizo mbili ni mkubwa na utarithishwa kizazi kwa kizazi. Alisema uhusiano huo licha ya kutokana na maingiliano makubwa kati ya viongozi, pia unatokana na urafiki uliopo miongoni mwa watu wa nchi hizo mbili. Alisema,

"Licha ya serikali, watu wa Pakistan wanaipenda sana China, na wana urafiki mkubwa kwa watu wa China, kwa hiyo bila kujali nani au serikali gani itaongoza China, Pakistan itakuwa na rafiki mkubwa wa China."

Bw. Musharraf alipofahamu kuwa CRI inakusanya habari kuhusu miji ya kirafiki ya China. Alisema,

"Hii ni hatua muhimu sana kwani inaweza kuimarisha maingiliano ya kiraia, kwa sababu maingiliano kati ya viongozi ni mengi lakini maingiliano kati ya watu wa kawaida pia yanahitaji kuimarishwa."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-09