Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-09 20:37:02    
Mapishi ya maharagwe marefu na nyama ya kuku

cri

Mahitaji

Maharagwe marefu gramu 50, nyama ya kuku gramu 200, pilipili hoho gramu 5, chumvi gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 5, mvinyo wa kupikia gramu 2, maji ya wanga gramu 5.

Njia

1. osha nyama ya kuku, halafu kata iwe vipande, koroga pamoja na chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, na mvinyo wa kupikia .

2. kata maharagwe marefu yawe vipande, chemsha maji, halafu tia vipande vya maharagwe marefu kwenye maji ya moto, halafu vipakue.

3. mimina mafuta kwenye sufuria, tia pilipili hoho korogakoroga, tia vipande vya maharagwe marefu na nyama ya kuku, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mimina maji ya wanga korogakoroga, mimina mafuta kidogo, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.