Mkutano wa mara ya sita wa mawaziri wa mambo ya nje wa "nchi tatu kubwa za Ulaya na nchi za Asia ya Kati" ulimalizika tarehe 10 katika mji mkuu wa Turkmenistan, Ashgabat. Kwenye mkutano huo pande mbili zilikubaliana kuanza kufanya ushirikiano kwenye mambo ya nishati. Imefahamika kwamba hivi karibuni Umoja wa Ulaya utasaini kumbukumbu na Turkmenistan na Uzbekistan kuhusu kuunganisha mabomba ya kusafirisha nishati kati ya nchi hizo mbili na Umoja wa Ulaya, ushirikiano wa sekta mbalimbali ulioanzia nishati kati ya Umoja wa Ulaya na Asia ya Kati umeanza kuwa dhahiri.
Sehemu ya Asia ya Kati ni muhimu kimkakati kutokana na mahali ilipo. Sehemu hiyo licha ya kupakana na Russia, China, na pia inapakana na Iran na Afghanistan. Kwa hiyo imekuwa ni sehemu ambayo nchi zenye nguvu zinaigombea, na kila upande unajitahidi kustawisha uhusiano na nchi za Asia ya Kati. Umoja wa Ulaya ukiwa kundi kubwa la kisiasa na kiuchumi umeikaribia zaidi Asia ya Kati baada ya kupokea nchi 27 kuwa nchi wanachama wake. Hali hiyo ya kijiografia inaufanya Umoja wa Ulaya uwe na mkakati mpya na kupanua ushawishi wake.
Kutokana na hali hiyo, mwezi Juni mwaka jana Umoja wa Ulaya ulipitisha "mkakati wa Asia ya Kati tokea mwaka 2007 hadi 2013", lengo kuu la mkakati huo ni pamoja na kuhakikisha usalama na utulivu wa Asia ya Kati, kutoa misaada ya kiuchumi, kukomesha umaskini na kuanzisha ushirikiano mkubwa. Kwa mujibu wa mkakati huo mpya, hadi kufikia mwaka 2013 Umoja wa Ulaya utaisaidia nchi tano za Asia ya Kati kwa Euro laki 7.5. kuhusu ushirikiano wa kiuchumi, Umoja wa Ulaya utahimiza nchi hizo ziwe na uchumi wa aina nyingi na kuongeza mitaji katika nchi hizo. Kadhalika Umoja wa Ulaya una matumaini kuwa nchi nyingine zitakuwa nchi wanachama wa WTO licha ya Kyrgyzstan ambayo imekwisha kuwa nchi mwanachama.
Ushirikiano wa nishati na mawasiliano ya usafiri ni ushirikiano mkuu kati ya Umoja wa Ulaya na Asia ya Kati. Asia ya Kati ikiwa ni sehemu mpya inayotoa huduma ya nishati pia ni sehemu yenye utajiri mkubwa nishati, ni sehemu muhimu katika masoko ya nishati kwenye Bahari nyeusi na Bahari ya Caspian. Hivi sasa gesi ya asili ya nchi za Asia ya Kati inayouzwa kwa Umoja wa Ulaya yote inapitia Russia, lakini kadiri Umoja wa Ulaya unavyozidi kutegemea nishati ya Asia ya Kati, Umoja wa Ulaya hauna budi kuzingatia usalama wa mabomba ya kusafirisha nishati hiyo, na mgogoro wa gesi ya asili kati ya Russia na Ukraine uliutia wasiwasi Umoja wa Ulaya. Kutokana na kuwa Russia inatumia udhibiti wa nishati kama ni njia muhimu ya kudhibiti uhusiano na nchi kubwa, Umoja wa Ulaya unahitaji kupata njia nyingine ya kusafirisha mafuta bila kupitia Russia, kwa hiyo mpango wa kupitisha nishati chini ya bahari ya Caspian umeandaliwa. Hivi sasa nchi za Umoja wa Ulaya zinahitaji kukubaliana kuhusu mpango huo na kuwekeza. Kuhusu mawasiliano ya usafiri, Umoja wa Ulaya unaona kuwa kushiriki kwenye juhudi za nchi za Asia ya Kati kujenga usafiri wa "Bahari ya Caspian ?Bahari Nyeusi?Ulaya" kunalingana na maslahi ya Ulaya.
Licha ya yote hayo, kiwango cha viwanda vyepesi katika nchi tano za Asia ya Kati ni duni, ni fursa nzuri ya kibiashara kuwekeza kwenye soko lenye watu milioni 55, na nchi hizo tano zina matumaini ya kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika mapambano dhidi ya ugaidi, magendo ya dawa za kulevya na uhalifu wa vikundi.
Idhaa ya kiswahili 2008-04-11
|