Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-14 15:21:33    
Vikundi vya Maonesho ya michezo ya sanaa vya Wulanmuqi mkoani Mongolia ya Ndani

cri

Vikundi vya maonesho ya michezo ya sanaa vinavyotoa huduma kwa watu kwenye mbuga ya Sunit katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani. Wafugaji wa mbuga hiyo wanaviita Vikundi vya Wulanmuqi maana yake ya kichina ni Machipukizi Mekundu.

Mwanzilishi mmoja wa vikundi vya Wulanmuqi Bw. Batu Suhe ambaye alianza kufanya kazi kwenye vikundi hivyo tangu miaka ya 50 ya karne iliyopita alisema,

"Mwishoni mwa miaka 50 ya karne iliyopita, kwenye sehemu kubwa ya mbuga ya ufugaji hakukuwa na watu wengi, na uchumi ulikuwa nyuma kimaendeleo. Haikuwa rahisi kwa wafugaji kupata habari za nje kutokana na mawasiliano magumu, walikuwa wanafanya kazi mchana na kulala usiku, na hakukuwa na burudani. Wakati huo kwenye mbuga ya Sunit ya wilaya ya Xilinguole alikuwepo mwanamume mmoja wa kabila la Wamongolia aitwaye Chaoge Badalahu, ambaye alitoa alishauri kuanzisha kikundi cha maonesho ya michezo ya sanaa cha kuhama hama, ili kutoa huduma ya nyimbo na ngoma kwa wafugaji mbugani."

Bw. Batu Suhe alijulisha kuwa wakati huo kutokana na upungufu wa pesa, hawakuwa na uwezo wa kuwaajiri maonesho ya michezo ya sanaa wa kulipwa, hivyo walikusanya wafugaji ambao walikuwa hodari katika kuimba nyimbo na kucheza ngoma ili kuanzisha kikundi cha maonesho ya michezo ya sanaa, na hicho kilikuwa ni kikundi cha kwanza cha Wulanmuqi. Mwanzoni kikundi hicho kilikuwa na wachezaji 11 na ala tano za muziki, na wachezaji hao wote walikuwa hodari katika kuimba nyimbo, kucheza ngoma na kupiga ala za muziki. Walifanywa maonesho ya michezo ya sanaa kwa wafugaji wa hapa na pale, na kuwaleta furaha kubwa.

Kikundi cha kwanza cha Wulanmuqi kilitoa mchango mkubwa kwa kuwaburudisha wafugaji mbugani. Kuanzia mwishoni mwa miaka 50 ya karne iliyopita, serikali ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani ilieneza kwa nguvu kubwa shughuli za Vikundi vya Wulanmuqi, vikundi hivyo vilistawi kwa haraka na kuenea kwenye sehemu zote za wafugaji mkoani humo, na hadi kufikia miaka ya 60 ya karne iliyopita, wilaya zote za mkoa wa Mongolia ya Ndani zilianzisha Vikundi vya Wulanmuqi. Wasanii wa vikundi hivyo si kama tu walikuwa wanafanya maonesho ya michezo ya sanaa kwa wafugaji, bali pia walikuwa wanatoa huduma nyingine mbalimbali za kutoa vitabu vya kusoma, kueneza elimu ya sayansi na teknolojia, kutengeneza mashine za kilimo na kunyoa nywele. Huduma hizo ziliwafurahisha sana wafugaji, hata wakisikia kikundi cha Wulanmuqi kitawatembelea, wanaweza kutembea umbali mrefu ili kukikaribisha. Bw. Ala Ta ni mfugaji wa wilaya ya Xilinguole ,alisema,

"Kila mara Kikundi cha Wulanmuqi kinapotoa maonesha michezo ya sanaa kwetu, sisi wafugaji tunafurahi sana, hata hatutaki kuondoka baada ya maonesho hayo, tunapenda kuongea na wasanii wa kikundi hicho."

Wapendwa wasikilizaji, mnaosikia ni muziki wa ngoma ya Kukamua Ng'ombe iliyochezwa na Kikundi cha Wulanmuqi. Zamani ngoma hiyo ambayo ilitungwa kutokana na hali halisi ya maisha ya wafugaji wa Mongolia ya Ndani ilichezwa na Vikundi vyote ya Wulanmuqi. Ngoma nyingine kama vile Ngoma ya Kukata Manyoya ya Kondoo na Ngoma ya Wafugaji pia zilikaribishwa sana na wafugaji, kwa kuwa maonesho ya ngoma hizo yaliwafanya wafugaji wafurahie hali ya maisha yao mbugani.

Mkoa wa Mongolia ya Ndani ya China ina eneo kubwa, licha ya watu wa kabila la Wamongolia, pia kuna watu wa makabila mengine madogo madogo yakiwemo makabila ya Wadawoer, Waewenke, Waelunchun, Wahui na Waman. Ili kukidhi matakwa ya watu wa makabila tofauti, Vikundi vya Wulanmuqi vilikuwa vinapanga maonesho kutokana na umaalumu wa makabila hayo. Juhudi hizo zilileta mafanikio makubwa, vikundi hivyo viliendeleza utamaduni na michezo ya sanaa ya makabila mkoani Mongolia ya Ndani, hali hii ilikuwa na athari kote nchini China.

Katikati ya miaka ya 60 ya karne iliyopita, mkoa wa Mongolia ya Ndani ulituma Kikundi kimoja cha Wulanmuqi kilichokuwa na wasanii 12 mji Beijing kufanya maonesho. Nyimbo na ngoma zilizochezwa na wasanii hao waliotoka sehemu za wafugaji ziliwafurahisha watazamaji wa mji wa Beijing, baadaye Vikundi vitatu vya Wulanmuqi vilipelekwa kufanya maonesho ya mzunguko kote nchini China, maonesho yao mazuri yaliwafurahisha sana watazamaji.

Vikundi vya Wulanmuqi si kama tu ninafanya maonesho ya michezo ya sanaa kwa watazamaji nchini China, bali pia vimewahi kufanya maonesho kwenye nchi za nje. Bw. Jiri Mutu ambaye amefanya maonesho ya michezo ya sanaa kwa miaka zaidi ya 40 kwenye Kikundi cha Wulanmuqi alisema,

"Katika miaka 40 iliyopita, tulifanya maonesho ya michezo ya sanaa zaidi ya 5,000 kwa wafugaji wa mkoa wa Mongolia ya Ndani, pia tuliwahudumia watazamaji wengine kote nchini China. Aidha tuliwahi kufanya maonesho kwa watu wa nchi nyingine zaidi ya 20 za Asia, Ulaya na Afrika, maonesho yetu yaliwafurahisha sana."

Sasa miaka zaidi ya 50 imepita, hali imebadilika sana mkoani Mongolia ya Ndani. Familia za wafugaji zina redio na televisheni, na wanaweza kupata burudani kwa njia mbalimbali, lakini kupenda kwa maonesho ya michezo ya sanaa ya Vikundi vya Wulanmuqi hakujapungua hata kidogo. Ingawa wachezaji wa Vikundi vya Wulanmuqi wamebadilika kwa mara nyingi, lakini vikundi hivyo havitabadilisha madhubuni ya kuwahudumia wafugaji, Vikundi vya Wulanmuqi vitakuwa jukwaa la kuhama hama linazotoa burudani kwa wafugaji mbugani.

Idhaa ya kiswahili 2008-04-14