Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-14 15:37:23    
Sanya ni mahali pazuri pa kupumzika kwenye sehemu ya Joto

cri

Sanya ni mji ulioko sehemu ya kusini kabisa mwa China, na pia ni mji pekee wenye shughuli za utalii ulioko kwenye pwani ya sehemu ya joto nchini China. Wakati sehemu ya kaskazini ya dunia ikiwa katika majira ya baridi, ambapo hali ya hewa ni baridi sana, theluji inaanguka, upepo wa baridi unavuma na maji ya mito kuganda kuwa barafu, lakini sehemu ya Sanya inakuwa na siku yenye anga ya buluu na mwangaza mzuri wa jua, watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanajiburudisha kwenye fukwe za bahari. Hali ya hewa ya Sanya katika majira ya baridi ni sawa ya ile ya visiwa vya Hawaii vya Marekani na kisiwa cha Puji cha Thailand. Watalii mbalimbali walisema,

"Ni mwaka wa tatu kwa sisi kufika hapa. Tunafika hapa ni kwa ajili ya kupunga upepo, na kutembea katika vipindi vya asubuhi na jioni."

"Hewa ya hapa ni safi sana, ninapenda kucheza baadhi michezo ya kuimarisha mwili na michezo ya burudani, ninapenda sana hekalu la Nanshan, ambalo ni zuri ajabu."

"Nilifika Hainan miezi miwili iliyopita, ninapenda sana hali ya hapa. Hali ya hewa nzuri, wakazi wa hapa ni wakarimu pia. Kuna mambo mengi yanayoniburudisha na kunifurahisha, ninaona hapa ni mahali pazuri sana."

Katika Sanya kuna mambo mengi ya kufurahisha. Tunaweza kwenda kuangalia hekalu la Nanshan lililoko kwenye sehemu ya kusini kabisa ya China, na kusikiliza sauti nene ya kengele ya hekalu hilo. Pia tunaweza kusikiliza hadithi kwenye mawe makubwa yaliyoko kwenye sehemu inayoitwa "Tianyahaijiao", maana yake ni "ukingo wa mbingu na pembe ya mwisho ya bahari". Vilevile tunaweza kucheza mchezo wa kupiga mbizi kuona mandhari ya sehemu ya chini ya bahari. Mbali na hayo, tunaweza kununua vitu vya sanaa vilivyotengenezwa kwa mikono vya watu wa kabila la Wali, ambalo ni kabila la asili la huko. Wakati giza linapoingia, watu hujaa kwenye baa zilizoko karibu na fukwe za bahari.

Ni hali ya kawaida kwa watu kula kaa wa baharini waliowakamata wao wenyewe huku wakinywa bia, kupunga upepo wa baharini na kuzungumza na marafiki. Lakini tofauti na miji mingi ya pwani ya China, watu wakiwa Sanya, wanajisikia kama wako katika nchi ya nje. Ndani ya baa kuna watu wengi kutoka nchi za magharibi wakizungumza kwa lugha tofauti. Wahudumu wa baa, pia wanaweza kuzungumza lugha za Kirusi na Kiingereza. Msichana Ivoch Chikova Nadegda Valezevha anaifahamu sana China, na ametembelea miji mingi ya China. Katika miaka ya hivi karibuni, karibu kila mwaka anafika kwenye mji wa Sanya, na akilinganisha na miji ya sehemu ya joto ya nchi nyingine, anaona kuwa huko ni salama zaidi, watu wanaweza kutembea wakati wa usiku bila tatizo lolote, alisema,

"Usiku sisi pia tunatembea nje, kwenda katika baa na kwenye fukwe. Kwa kawaida tunarudi saa 6 usiku, baadhi ya nyakati tulirudi saa 9 alfajiri. Usafiri wa hapa ni mzuri kuliko wa Russia, najiona salama sana kuishi hapa."

Hivi sasa kutalii na kupumzika kwenye mji wa Sanya ni jambo linalopendwa na watu wengi. Uchunguzi uliofanywa na jumuiya ya hifadhi ya mazingira ya dunia kuhusu miji 158 ya dunia, ubora wa hewa ya mji wa Sanya unachukua nafasi ya pili ukiufuata mji wa Havana. Huenda hii ni sababu kubwa inayovutia watu wanaotaka kuboresha afya zao. Mzee Zhou kutoka mji wa Shanghai, China amekaa Sanya kwa zaidi ya mwezi mmoja akiwa pamoja na mkewe, hata sikukuu ya Spring walisherekea wakiwa huko. Alisema,

"Tumekaa hapa kwa zaidi ya mwezi mmoja, ni kama siku 40 hivi. Mke wangu ana ugonjwa wa kuhema na mkandamizo mkubwa wa damu. Laini tangu alipofika hapa, mkandamizo wa damu umepungua. Hewa ya hapa ni nzuri, hali ya hewa ni ya sehemu ya joto, hapa hakuna majira ya baridi, panafaa sana kuishi kwa wazee wenye magonjwa ya muda mrefu."

Wageni wa nchi za nje waliofika na kupumzika kwenye mji wa Sanya, wanapenda sana matibatu ya jadi ya China, yanayotolewa kwenye nyumba ya mapumziko yenye matibabu ya jadi ya China ya mji wa Sanya. Bw. Evan amefika mara mbili kwenye mji wa Sanya, na sasa ugonjwa wake wa shingo umepata ahueni baada ya kutibiwa kwa matibabu ya jadi ya China. Alisema

"Nina nafasi katika majira ya joto, nimefika hapa kufuata matibatu katika majira ya baridi. Ninataka kutibu ugonjwa wangu wa shingo, ninaona matibabu hayo yana ufanisi mkubwa sana."

Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2007 idadi ya watalii kutoka nchi za nje waliokwenda kutembelea mji wa Sanya ilizidi laki 5, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 30% kuliko mwaka uliotangulia, kasi hiyo ya ongezeko inachukua nafasi ya kwanza kati ya miji ya China. Maendeleo ya sekta ya utalii yanastawisha shughuli za hoteli na soko la nyumba. Hadi sasa, mji wa Sanya umejenga hoteli 9 za nyota 5. Hivi sasa ujenzi wa hoteli ya nyota 7 na bandari moja ya kimataifa kwa ajili ya boti ulianza mwaka jana. Kiongozi wa jumuiya ya mahoteli ya Sanya, Bw. Liu Kaiqiang alisema, hata hivyo bado hatuwezi kukidhi mahitaji ya sekta ya utalii ya mji wa Sanya. Alisema,

"Shughuli za mahoteli za Sanya ziliendelezwa kwa nguvu katika nusu ya pili ya mwaka 2003, raslimali za kipekee za mji wa Sanya, maendeleo ya uchumi wa China na maendeleo ya kasi ya uchumi wa dunia, pato la watu wanaofanya utalii limeinuka na mahitaji yao yameinuka, serikali ya mji wa Sanya pamoja na mashirika ya utalii yanafanya juhudi za pamoja, maendeleo makubwa yalionekana baada ya mwezi Oktoba mwaka 2003, mahoteli makubwa yanaongezeka kwa mfululizo, na idadi ya watalii pia inaongezeka kwa haraka, hali hiyo inaendelea hadi hivi sasa."

Kutokana na sera nafuu zinazotolewa na serikali ya China kwa mji wa Sanya, hivi sasa watalii wa nchi na sehemu 21 hawahitaji visa ya kuingia Sanya. Mkurugenzi wa idara ya utalii ya mkoa wa Hainan, Bw. Zhang Qi alisema,

"Watalii wa nchi za kigeni wanaweza kuona kuwa hakuna vizuizi vyovyote kwao wakiwa katika kisiwa cha Hainan, Hainan ni mahali pazuri kabisa kwa mapumziko katika sehemu ya mashariki ya dunia, tunatoa mwaliko wa kudumu kwa watu wote wa dunia."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-14