Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-16 16:44:54    
Mapishi ya pilipili hoho na majimbi

cri

Mahitaji

Majimbi 10, pilipili hoho 4, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, chumvi nusu ya kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja

Njia

1. kata pilipili hoho iwe vipande.

2. chemsha maji, halafu weka majimbi kwenye sufuria chemsha kwa dakika 20, halafu ipakue. Kata majimbi iwe vipande.

3. koroga vipande vya majimbi pamoja na pilipili hoho, chembechembe za kukoleza ladha, chumvi, halafu weka kwenye sufuria yenye maji chemsha kwa mvuke kwa dakika 30. Ipakue mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa