Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-16 21:50:33    
Napenda kujulisha hali ya China kwa watu wengi zaidi

cri

Baada ya tukio la uhalifu mkubwa wa mabavu kutokea tarehe 14 Machi huko Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Tibet, China, baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilitoa habari zisizolingana na hali halisi au kupotosha hali ya mambo hata kusema uwongo kuhusu tukio hilo, vitendo hivyo vimewaghadhabisha na kulaumiwa vikali na watu wengi wenye busara. Mtaalamu wa suala la China wa Brazil Bw. Carlos Tavares alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alisema, suala la Tibet ni mambo ya ndani ya China, habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi zilidanganya watu. Kuhusu mwenge wa Michezo ya Olimpiki ulipokimbizwa kwa kupokezana ulisumbuliwa na watu wachache waliotetea kuifanya Tibet ijitenge na China, Bw. Tavares alisena tukio kama hilo liliwahi kutokea hapo kabla, na watu waliopinga mbio za mwenge ni wachache tu, hakuna haja ya kuwajali. Alisema:

"Huko Paris kulikuwa na watu zaidi ya 20 ambao walifanya usumbufu na uharibifu kwa mbio za mwenge, hali hii ilionesha kuwa watu hao wachache ni waumini dini wenye msimamo mkali. Sababu nyingine ni kwamba baadhi ya watu hawapendi kuona kuwa Beijing itaandaa Michezo ya Olimpiki itakayopata mafanikio makubwa zaidi kwenye historia ya michezo hiyo, na kutokana na maendeleo ya siasa na uchumi ya China, baadhi ya watu hawapendi kuona China inayojiendeleza na kuwa na nguvu kubwa, hivyo watu hao walifanya usumbufu na upinzani huo ni kutaka kudhoofisha athari kubwa ya China duniani".

Kwa maoni ya Bw. Tavares, baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilipotoa habari kuhusu uharibifu uliofanywa na watu wanaotetea kuifanya Tibet ijitenge na China wakati wa mbio za mwenge wa Michezo ya Olimpiki vilitia chumvi . Alisema:

"Kihalisi, katika mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya Olimpiki, kulikuwa na mtu mmoja au wawili ambao walijaribu kunyang'anya mwenge, lakini vyombo vya habari vilitia chumvi na kupanua tukio lenyewe kuwa kubwa lisilo na kikomo. Kwa kweli, watu wengi si wabrazil ama wafaransa, wote wanaelewa kuwa ni wafuasi wa Kundi la Dalai wanaofanya usumbufu na uharibifu wa mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya Olimpiki".

Kabla ya hapo Dalai Lama aliwahi kujigamba kuwa yeye haungi mkono shughuli za mabavu, Bw. Tavares anaona kuwa maneno ya Dalai Lama na vitendo vyake vinagongana kabisa. Alisema:

"Kama Dalai Lama ni kiongozi wa dini, kama anaunga mkono harakati za amani na kupinga mabavu, basi hapaswi kuruhusu wafuasi wake wafanye shughuli za mabavu, na hakupaswa kuwachochea watawa wachache kuzusha tukio la mabavu huko Lhasa, bali anapaswa kujitokeza katika utatuzi wa suala au kutoa maombi yake kwa njia ya amani".

Bw. Tavares alisisitiza mara kwa mara kuwa, Tibet ni sehemu moja ya China, suala la Tibet lazima litatuliwa na wachina wenyewe, nchi nyingine hazipaswi kuingilia kati. Alisema:

"Tokea Tibet ilipokombolewa kwa njia ya amani mwaka 1950, watibet wote wanaweza kupata elimu ambayo zamani waliwapata watawa tu. Ndiyo maana, mambo ya utamaduni wa Tibet yanaendelezwa siku hadi siku. Hivi sasa mapato ya shughuli za utalii za huko yamechukua 15% ya thamani ya jumla ya uzalishaji mali wa mkoani Tibet. Mwaka 2007, watalii wa makabila mbalimbali wa China wapatao milioni 4 walikwenda Tibet kutalii, mapato ya shughuli za utalii za Tibet yalifikia dola za kimarekani milioni 668".

Bw. Tavares anashughulikia utafiti wa suala la China, hivyo siku zote anaona kuwa mambo mbalimbali ya Tibet yanaendelea kukua hivi sasa. Lakini kutokana na sababu mbalimbali watu wa nchi za magharibi hawajaelewa, hata wanaelewa kwa makosa kuhusu suala la Tibet. Yeye mwenyewe amefanya kazi nyingi kujulisha hali ya China na hali ya Tibet kwa watu wa Argentina, alisema hii ni kazi kubwa, lakini anapenda kujulisha hali ya China kwa watu wengi zaidi, na ameandika vitabu vitano kuhusu China. Kwa kuwa watu wengi wanashikilia maoni yao ya upande mmoja kutokana na sababu za kisiasa au kidini, bado hawajaweza kuielewa China kihalisi. Lakini mwaka jana wabrazil waliokwenda China kufanya utalii walifikia elfu 61, hili ni ongezeko la 40 % kuliko mwaka uliotangulia. Nina imani kuwa watu wengi watakuwa na matumaini mazuri ya kuifahamu China.