Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-17 15:18:02    
Mabadiliko ya makazi ya watu

cri

Makazi siku zote ni jambo muhimu katika maisha ya watu wa China. Katika miaka ya hivi karibuni, kuboresha hali ya makazi pia ni jambo wanalozungumzia sana watu wa China. Baada ya China kufanya mageuzi na kufungua mlango, hali ya makazi ya Waislam nchini China imekuwa na mabadiliko ya kufurahisha. Bw. Bai Shangcheng ni mjumbe kutoka kijiji cha mkoa unaojiendesha wa Ningxia, alipomfahamisha mwandishi wetu wa habari hali ya makazi ya watu wa sehemu za magharibi za China kabla ya mageuzi na kufungua mlango alisema,

"Zamani sisi wanakijiji tuliishi mapangoni, tulikuwa na watoto wengi, watu sita waliishi kwenye pango moja, na iliponyesha mvua, maji ya mvua kuingia pangoni lilikuwa jambo la kawaida."

Mapango yanayotajwa na Bw. Bai Shangcheng ni makazi ya wanavijiji wa sehemu za magharibi za China, katika muda mrefu kabla ya mageuzi na kufungua mlango, mapango mengi waliyokuwa wakitumia watu yalikuw madogo, tena yalikuwa na hali duni. Wakati ule katika sehemu za magharibi, watu walioishi mjini wengi pia waliishi katika nyumba za matofali zisizo na ghorofa, kwa kawaida watu watatu au wanne, hata wa vizazi vitatu waliishi kwenye nyumba moja.

Mjini Beijing, hali ya makazi ilikuwa nzuri zaidi, watu wengi waliishi kwenye nyumba za chini, japokuwa baadhi ya watu waliishi kwenye nyumba za ghorofa, lakini nyumba hizo zenyewe zilikuwa na chumba moja moja cha kulala tu, jiko na choo zinatumiwa kwa familia zote, na shughuli zote za familia moja zilikuwa zinafanyika katika chumba kimoja tu. Mjumbe kutoka Beijing Bibi Wang Xiaoke aliwahi kuishi kwenye nyumba kama hiyo kwa muda mrefu, hakuweza kusahau hali ya siku moja ya kuwapokea wageni nyumbani kwake, alisema,

"Baba yangu ni mwalimu wa kichina, alikuwa na miradi kadhaa ya ushirikiano wa kimataifa. Siku moja wageni walikuja nyumbani kwetu, lakini hawakuwa na mahali pa kukaa, walikaa kitandani. Katika wazo lao chumba cha kulala ni sehemu binafsi, lakini wakati huo hatakuwa na sebule."

Bibi Wang Xiaoke alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ndoto yake kubwa kabisa ilikuwa ni kuwa na nyumba yenye jiko na choo. Lakini hivi leo, moja ya matokeo kutokana na mageuzi na ufunguaji mlango na maendeleo ya uchumi ni kuboresha kwa hali ya makazi. Bw. Bai Shangcheng alisema,

"Baada ya kuanza kufanya mageuzi na kufungua mlango, mkoa unaojiendesha wa Ningxia ulifanya ukarabati wa makazi ya mapango na nyumba kuku zenye hatari, ndipo watu walipohama kutoka kwenye mapango, na serikali iliipa kila familia Yuan 8,000, ili watu wawe na nyumba za kukaa."

Bw. Bai Shangcheng alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, miaka 30 iliyopita hata hakutarajia kuwa ataishi kwenye nyumba kubwa, na ataweza kuoga kwenye bafu la nyumba yake mwenyewe.

"Zamani nilikuwa nakwenda kituo cha kuogea, nilikuwa naoga kila baada ya siku 10 au nusu ya mwezi; sasa ninakaa kwenye nyumba yenye eneo la mita za mraba 130, tunatumia gesi nyumbani, na tunaweza kuoga wakati wowote tunapotaka, kwani nyumbani kuna bomba la maji moto."

Mjumbe wa kabila la Watatar Bw. Abdullah Abbas ni mwalimu wa idara ya sayansi ya maisha na teknolojia ya Chuo Kikuu cha Xinjiang, yeye ana kazi nyingi kila siku. Alisema kila akirudi nyumbani baada ya kazi, mazingira ya makazi ya starehe na ya kisasa yanamfanya asahau uchovu wake. Alisema,

"Sasa familia yangu ya watu wanne inakaa kwenye nyumba ya ghorofa yenye eneo la mita za mraba zaidi ya 150, kila mtu ana chumba cha kulala, pia kuna kompyuta na televisheni, mazingira ya maisha na kusoma ni mazuri sana. Nikichoka kazini, naona naweza kupumzika vizuri baada ya kurudi nyumbani, halafu pia nina msukumo wa kufanya kazi kwa bidii, ili kuweka mazingira mazuri zaidi kwa familia yangu."

Bibi Wang Xiaoke alipozungumzia mabadiliko ya miaka 30 hivi kwenye eneo wanalokaa watu wengi wa kabila la Wahui mjini Beijing?Niujie alisema,

"Zamani Niujie haikuwa na duka kubwa, maduka yote yalikuwa madogo, pia yalikuwa makongwe. Hakukuwa na nyumba za ghorofa, nyingi zilikuwa ni nyumba za chini. Sasa serikali inawapa wakazi waliorejea kwenye eneo la makazi yao ya zamani sera nyingi zenye unafuu, na kuzifanya nyumba za huko zidumishe upekee wa utamaduni wa kikabila."

Katika karne ya 21, watu wana machaguo mengi zaidi ya makazi, kuna makazi ya nyumba zenye ghorofa nyingi, nyumba zenye ghorofa, makazi yenye bustani, hata kuna makazi ya nyumba za kifahari(villa). Kadiri kiwango cha maisha ya watu kinavyoinuka, ndivyo kazi ya kupamba nyumba imekuwa inafuatiliwa zaidi na watu. Watu licha ya kutaka kupata nyumba kuwa kubwa, pia wanataka kupata mazingira ya kukaa na vifaa mbalimbali vikamilike zaidi, wanataka kukaa kwa starehe na kukaa kwa furaha. Kutokana na mabadiliko ya makazi, Waislam wa China pia wanaona mabadiliko makubwa na kasi yanayoletwa na mageuzi na ufunguaji mlango, pia wananufaika na matokeo hayo mazuri, wanaamini kuwa: katika siku za usoni watakaa kwa furaha zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2008-04-17