Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-18 16:28:25    
Moto mtakatifu wa michezo ya Olimpiki ya Beijing wakimbizwa huko Dar es Salaam

cri

Alasiri ya tarehe 13 Aprili, mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing zilifanyika kwa mafanikio mjini Dar es Salaam, ambao ni mji pekee uliopokea mwenge huo katika bara la Afrika. Uchangamfu mkubwa na urafiki ulioneshwa na watu wa Tanzania viliwavutia watu.

Saa 3 kabla ya uzinduzi wa mbio hizo, watu walikuwa wanamiminikia kwenye uwanja wa kituo cha reli ya TAZARA, ambapo ilikuwa ni sehemu ya kuanza kwa mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki. Wasanii wa Tanzania waliimba na kucheza ngoma uwanjani.

Kutokana na mpango uliowekwa, mbio hizo za umbali wa kilomita 5 zilianzia kwenye uwanja wa kituo cha reli ya TAZARA na kumalizika kwenye uwanja mpya wa taifa, ambapo mwenge wa michezo ya Olimpiki ulikimbizwa kwa kupokezana na wakimbizaji 80 kutoka Tanzania, China na nchi nyingine za Afrika. Mkimbiza mwenge wa kwanza alikuwa waziri wa Habari, michezo na Utamaduni wa Tanzania Bw Mohamed Seif Khatib alikabidhiwa mwenge na makamu wa rais Dk Shein, na kukimbiza kwa mita 60.

Miongoni mwa watu walikuwa wanasubiri kuuona mwenge huo kwenye kando za barabara, pia kulikuwa na vijana kadhaa wa Tanzania ambao walikuwa wanakimbia kuufuata mwenge huku wakishangilia.

Watoto waliovaa sare za shule walikuwa wamejipanga kwenye kando za barabara wakiimba.

Wengine walimwambia mwandishi wetu wa habari jinsi walivyofurahia mbio hizo za mwenge wa michezo ya Olimpiki.

Mkimbiza mwenge wa mwisho ambaye ni naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Anna Tibaijuka alipokimbiza mwenge huo kuingia uwanjani, watu walimkaribisha kwa shangwe. Kundi la vijana wa Kenya walishangilia kwa lugha ya Kichina kumtia moyo.

Saa 10 alasiri kilele cha mbio hizo kilifika wakati mwenge wa michezo ya Olimpiki ulipokimbizwa hadi kwenye uwanja mpya wa taifa. Naibu mwenyekiti mtendaji wa kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing Bw. Liu Jingmin aliukabidhi mwenge huo kwa meya wa Dar es Salaam. Bw. Liu alitoa shukrani kwa watu wa Tanzania, alisema mbio hizo za mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing mjini Dar es Slaam zilifanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na shauku kubwa na urafiki wa watu wa Tanzania, ambao walionesha jinsi wanavyopenda michezo na michezo ya Olimpiki.

Wasikilizaji wapendwa, mliosikia sasa hivi ni wimbo unaoitwa "shujaa", wimbo huo ulitungwa na mtungaji wa muziki wa China kutokana na hadithi ya mtanzania Bw. John Stephen Akhwari. Miaka 40 iliyopita, mchezaji wa Tanzania Bw. Akhwari aliposhiriki kwenye mbio za Marathon katika michezo ya Olimpiki ya Mexico aliumia mguu wake wa kulia,lakini Bw. Akhwari aliendelea mbio zake mpaka mwisho. Alisema "nchi yangu ilinituma Mexico City siyo kuanza michezo , bali ni kumaliza michezo"

Katika mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing, Bw. Akhwari alikimbiza mita 63 akiwa mkimbiza mwenge wa 12. Matumaini yake ya Olimpiki yaliendelea kwenye ardhi ya nchi yake baada ya miaka 40.

Nyumbani mwa Bw. Akhwari ziko sehemu yenye umbali na jiji la Dar es Salaam, kwa ajili ya mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing, Bw. Akhwari alikwenda Dar es Salaam kwa basi. Alisema mkimbiza mwenge anabeba majukumu ya kueneza moyo wa Olimpki. Michezo ya Olimpiki ni mashindano, pia ni mkutano wa michezo. Bila shaka ni muhimu kupata ushindi, lakini kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki pia ni muhimu sana. Mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki zinaonesha moyo wa kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki.

Bw. Akhwari aliwashukuru rafiki wa China kumpatia fursa ya kuwa mkimbiza mwenge. Watu husema, China na Tanzania si kama tu ni rafiki, bali pia ni ndugu wazuri.

Kati ya wakimbiza mwenge wa mbio huko Dar es Salaam, kuna wachina 14.

Mkimbizaji mwenge wa saba wa mbio hizo ni mchina Bw. Liu Yulin wenye umri wa miaka 56, ambaye aliwahi kushiriki kwenye ujenzi wa reli ya TAZARA. Mwaka 1975 Bw. Liu Yulin aliyejifunza masomo ya lugha ya Kiswahili alihitimu kutoka chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, halafu alitumwa kwenye kikundi cha utafiti wa kijiolojia nchini Tanzania kuwa mtafsiri. Sasa Bw. Liu Yulin amekuwa ni mjumbe mkuu wa ofisi ya uchumi na biashara ya ubalozi wa China nchini Tanzania.

Baada ya kukimbiza mwenge, Bw. Liu Yulin alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, anaona fahari sana kukimbiza mwenge huko sehemu alipowahi kufanya kazi.

Bw. Liu Yulin alisema, nchini Tanzania yeye na wenzake wanafuatilia habari kuhusu michezo ya Olimpiki ya Beijing. Wachezaji watatu wa Tanzania watashiriki kwenye michezo hiyo, ana matumaini kuwa wanaweza kuonesha uwezo wao kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing, pia ana matumaini kuwa michezo hiyo itafanyika kwa mafanikio.

Bw. Liu Yulin alisema zamani walikwenda Tanzania na kujenga urafiki kati ya China na Tanzania, hivi sasa wechezaji wa Tanzania watakwenda Beijing kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki, hii itahimiza zaidi urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Mkimbiza mwenge wa nane wa mbio za mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing nchini Tanzania ni mchina Bw. Jiang Senling. Bw. Jiang Senling ni dereva wa reli ya Qinghai-Tibet, Baba yake aliwahi kuwa ni mfanyakazi aliyeshiriki kwenye ujenzi wa reli ya TAZARA. Bw. Jiang Senling alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa alikuja nchini Tanzania pamoja na matumaini ya baba yake. Kabla ya kuja nchini Tanzania, baba yake alimtaka azingatie vizuri reli ya TAZARA, Bw. Jiang Senling alisema, wakati walipoona reli hiyo, aliona fahari sana.

Baada ya safari ya ndege ya muda mrefu, Bw. Jiang Senling aliwasili Tanzania. Mara alipofika nchini Tanzania, aliona urafiki kutoka waafrika. Alisema watanzania ni wa kirafiki, mtaani watanzania walinisalimia kwa lugha ya kichina "Ni hao", nilijibu kwa tabasamu.

Bw. Jiang Senling aliona kuwa kama China kuisaidia Tanzania kujenga reli ya TAZARA, mbio za mwenge pia zinaeneza urafiki. Alisema lengo lake kufika nchini Tanzania ni kueneza hisia za wachina kwa Tanzania, na kuoneshea amani na urafiki duniani.

Idhaa ya kiswahili 2008-04-18