Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-18 16:51:29    
Russia yaharakisha hatua za kurudi tena Mashariki ya Kati

cri

Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 17 alimaliza ziara yake ya siku mbili nchini Libya. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Russia kuitembelea nchi hiyo na pia ni ziara muhimu kabla ya Putin kuondoka madarakani mwanzoni mwa mwezi Mei. Ziara hiyo inamaanisha kuwa Russia itaharakisha hatua zake za kurudi tena kwenye mambo ya siasa na uchumi ya Mashariki ya Kati.

Kwanza, ziara ya Rais Putin inaonesha nia yake ya kuwa Russia ikiwa ni nchi kubwa itashiriki kwenye mambo ya Mashariki ya Kati. Ingawa Rais Putin ataondoka madarakani, lakini siku moja kabla ya kuanza ziara yake alikubali kuwa mwenyekiti wa chama tawala kikubwa nchini Russia, United Russia, na kuwa waziri mkuu wa serikali ya Russia. Hii inamaanisha kuwa Bw. Putin ataendelea kuwa kiongozi mkuu atakayeshika usukani katika mambo ya ndani na ya nchi za nje. Mbali na hayo, hali ya kisasa kwenye sehemu ya Mashariki ya Kati imebadilika, Marekani imekwama kwenye matope kutokana na vita vya Iraq na uwezo wake wa kujaribu kuongoza mambo ya Mashariki ya Kati umefifia.

Kuanzia mwaka jana Russia imechangamka kidiplomasia kwenye Mashariki ya Kati. Mwanzoni mwa mwaka jana Rais Putin alitembelea Saudi Arabia, Qatar na Jordan ili kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kinishati. Kutokana na suala la nyuklia, mgogoro kati ya Iran na nchi za magharibi ulipokuwa mkali, mwezi Oktoba Rais Putin aliitembelea Iran na kuonesha kuwa Russia ikiwa ni nchi kubwa inarudi tena kwenye eneo la Mashariki ya Kati. Mwishoni wa mwaka jana waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov aliitembelea Libya, hii ni hatua muhimu kwa ajili ya kufufua uhusiano wa pande zote na Libya. Mwezi Machi mwaka huu Bw. Sergey Lavrov kwa mara nyingine tena aliitembelea Mashariki ya Kati na kusisitiza uhusiano wa jadi wa kiwenzi na Syria, na kusema kwamba Russia itafanya jitihada kusukuma mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Yote hayo yamedhihirisha kuwa Russia ikiwa ni nchi kubwa iko tayari kurudi tena kwenye mambo ya Mashariki ya Kati.

Pili, ziara ya Putin nchini Libya itaimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Russia na Libya. Tarehe 16 rais wa Libya Muammar al-Qadhafi alipozungumza na Rais Putin walijadiliana masuala muhimu ya pande mbili. Kabla ya kuondoka nchini Libya Rais Putin alisema Russia na Libya zimekubaliana kwamba zitapiga hatua katika mambo ya siasa na ya uchumi, na kuamini kuwa nchi hizo mbili zitainua ushirikiano wa pande mbili kwenye kiwango kipya, katika siku hiyo pande mbili zilisaini taarifa ya pamoja ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Taarifa inasema pande mbili zitajitahidi kuifanya Mashariki ya Kati iwe sehemu isiyo silaha kali, kupunguza operesheni za kijeshi katika sehemu ya bahari ya Mediterranean na kuifanya sehemu hiyo iwe ya amani, utulivu na ya ushirikiano.

Tatu, kuhusu ushirikiano wa kiuchumi, Russia na Libya zimesaini makubaliano kuhusu miradi 10 ya ushirikiano. Licha ya kumbukumbu ya ushirikiano wa gesi ya asili, pande mbili zimesaini makubaliano kuhusu Russia kuisaidia Libya kujenga reli yenye urefu wa kilomita 500 yenye thamani ya Euro bilioni 2.2. Baada ya kusaini miradi hiyo naibu waziri mkuu na waziri wa fedha wa Russia Bw. Alexei Kudrin alisema kwa mujibu wa mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kifedha, Russia itaisamehe Libya deni la dola za Kimarekani bilioni 4.6 ikiwa kama ni fadhila kwa kusaini mikataba.

Ya mwisho, hivi karibuni Russia imekuwa inatilia nguvu ushirikiano wa kutumia nishati ya nyuklia kwa ajili ya amani na nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati. Rais Putin alipokuwa ziarani nchini Libya nchi hizo mbili zimekubali kusaini makubaliano ya kimsingi kuhusu matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia na mpango wa kutekeleza makubaliano hayo. Kabla ya hapo, mwezi Machi Rais wa Misri alipotembelea Russia nchi hizo mbili zilisaini makubaliano ya kutumia nishani ya nyuklia kwa amani, na hivi karibuni Syria imetangaza kuwa inapenda kushirikiana na Russia katika matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.

Tarehe 17 Rais Putin alimaliza ziara yake nchini Libya, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas alitangaza kuwa mwezi Juni mkutano wa duru jipya utafanyika mjini Moscow, na tarehe 18 atafanya mazungumzo na Rais Putin kuhusu mkutano huo. Vyombo vya habari vinaona kuwa kwa kufanya juhudi za kidiplomasia, Russia imekuwa inarudi tena kwenye mambo ya Mashariki ya Kati.