Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-22 20:44:26    
Utamaduni wa Tibet wapata maendeleo kutokana na juhudi za serikali ya China za kurithisha na kuhifadhi utamaduni

cri

Opera ya kitibet ni sanaa inayoelezea hadithi kwa kuimba na kucheza inayofahamika sana kwenye sehemu wanakoishi watu wa kabila la Watibet hasa mkoani Tibet .

Kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii na hatua ya kufungua mlango kwenye mkoa wa Tibet katika miaka ya hivi karibuni, utamaduni wa Tibet kama vile opera ya kitibet umekuwa unastawi tena. Maonesho mengi ya opera hiyo ambayo iko kwenye hatari ya kutoweka sasa yanaendelezwa. Bibi Chi Jia ni mchezaji wa opera wa kitibet. Ameimba opera hiyo kwa miaka karibu 30, lakini sasa anafurahi zaidi, alisema,

"Nilianza kupenda kuimba opera ya kitibet tangu nilipokuwa na umri mdogo, lakini wakati huo ilikuwa ni kwa ajili ya kjiburudisha tu. Baada ya kujiunga na kikundi cha maonesho ya michezo ya sanaa, mimi pamoja na wachezaji wenzagu tulifanya maonesho kwa watu kwenye sehemu mbalimbali na hata nchi za nje. Sasa wachezaji wa kikundi chetu wanaongezeka, na tuna mapato mazuri. Naona hali hii inatokana na sera nzuri ya serikali ya kuhimiza kustawi kwa vikundi vya maonesho ya michezo ya sanaa za jadi."

Kwa kupitia kuchimba, kuratibu na kuendeleza maliasili ya utamaduni wa kale wa Tibet, wasanii wa Tibet kama vile bibi Chi Jia si kama tu wanaweza kushughulikia usanii wa jadi wanaopenda, bali pia wanahifadhiwa na serikali.

Mzee Sam Drup mwenye wa miaka 85 ni msanii wa kabila la Watibet ambaye ni hodari katika kuimba shairi maarufu la kabila hilo "Utenzi wa Mfalme Gesar". Ili kuliwezesha shairi hilo la historia liweze kurithishwa kizazi baada ya kizazi, serikali ya mkoa wa Tibet inamwalika Bw. Sam Drup mara kwa mara kutoa hotuba kuhusu sanaa ya kuimba mashairi kwenye Chuo Kikuu cha Tibet, taasisi ya sayansi ya jamii ya mkoa wa Tibet na kwenye idara nyingine. Idara inayohusika ya serikali ya mkoa huo pia ilitoa nyumba na ruzuku ya maisha kwa wasanii wa utamaduni wa jadi wa Tibet akiwemo Bw. Sam Drup.

Kuanzia mwaka 1980, kila mwaka idara ya utamaduni ya serikali ya mkoa wa Tibet imechapisha kitabu kimoja au viwili kuhusu hadithi za Mfalme Gesar, na hadi sasa imechapisha vitabu 30. "Utenzi wa Mfalme Gesar" ni shairi linalorithiwa kwa kupitia wasanii wa kuimba mashairi. Kutokana na kuwa wasanii hao wengi wana umri mkubwa, na hata baadhi yao wamefariki dunia, juhudi za kuokoa shairi hilo zinakabiliwa na changamoto kubwa. Mtaalamu wa ofisi ya utafiti wa makabila ya taasisi ya sayansi ya jamii ya mkoa wa Tibet Bw. Rig Zin alisema,

"Hivi sasa kazi yetu ya dharura zaidi ni kurekodi hadithi zinazoimbwa na wasanii wazee akiwemo Bw. Sam Drup, na kuchapisha vitabu vya hadhithi hizo. Tunapanga kuchapicha vitabu vya hadithi zaidi ya 60 zinazoelezwa na Bw. Sam Drup katika miaka kati ya mitano na nane. Katika miaka mitano iliyopita tumechapisha vitabu 27 vya hadithi 25 zlizosimulia."

Katika maendeleo ya historia ya miaka mingi, watu wa kabila la Watibet walivumbua utamaduni wa aina mbalimbali. Licha ya usanii wa kuimba mashairi iliyotajwa, vitu vingine vya sanaa zikiwemo ngoma, methali na nyimbo za jadi pia vina historia ndefu. Hivi sasa watu wengi zaidi na zaidi wanajishughulisha na kazi za kukusanya, kuhariri na kuchapisha vitabu kuhusu utamaduni wa jadi na michezo ya sanaa ya Tibet, na kutoa mchango kwa ajili ya kuhifadhi na kurithi utamaduni na michezo hiyo ya sanaa.

Mtafiti wa ofisi ya utafiti wa mila na desturi za jadi ya taasisi ya sayansi ya jamii ya mkoa wa Tibet Bw. Tsering Phuntsok amefanya kazi ya kuokoa fasihi za sanaa za umma za Tibet kwa miaka zaidi ya 20. Anaona kuwa serikali ya China inatilia maanani sana kuokoa na kuhifadhi michezo ya sanaa na utamaduni wa Tibet. Alisema,

"Kuanzia mwishoni mwa miaka 80 ya karne iliyopita, China ilifanya juhudi kubwa za kuokoa na kuhifadhi utamaduni wa Tibet, na ilianzisha idara maalumu za kuokoa, kukusanya na kutafiti utamaduni wa kabila la Watibet kwenye sehemu mbalimbali mkoani Tibet, na kupata mafanikio makubwa."

Kwenye mkoa wa Tibet, mabaki yanayoweza kuonesha utamaduni wa jadi na uaminfu wa dini kama vile Kasri la Potala, Hekalu la Norbu Lingka na Hekalu la Sagya ni mengi sana. Naibu mkurugenzi wa idara ya utamaduni ya mkoa wa Tibet Bw. Xin Gaosuo alisema, katika miaka mingi iliyopita serikali ya China imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kukarabati na kuhifadhi mahekalu. Alisema,

"Tangu China ilipokombolewa mwaka 1949 hadi mwaka 2005, China ilitenga renminbi yuan zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya kazi za kuhifadhi na kukarabati mabaki ya utamaduni mkoani Tibet, na kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2010, China imepanga kutenga yuan milioni 600 ili kuendelea na kazi hizo. Mbali na hayo serikali inatoa fedha kwa ajili ya kuhifadhi mabaki ya utamaduni wa Tibet."

Katika miaka ya hivi karibuni kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii na hatua kubwa ya kufungua mlango kwenye mkoa wa Tibet, athari ya utamaduni wa Tibet duniani inaongezeka siku hadi siku, na watu wengi kutoka nchi mbalimbali wanatalii mkoani humo. Wakati huo huo shughuli za mawasiliano ya utamaduni wa Tibet pia zinaongezeka siku hadi siku, na kuleta athari kubwa. Katika miaka kadhaa iliyopita, Tibet imetuma vikundi zaidi ya 20 kwenda nchi za nje kufanya mawasiliano ya utamaduni, kwa mfano kuandaa maonesho ya mabaki ya utamaduni ya kale ya Tibet nchini Ujerumani na Marekani.

Idhaa ya kiswahili 2008-04-21