Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-23 20:41:34    
Mapishi ya doufu na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Doufu gramu 200, kamba-mwakaje gramu 150, sosi ya pilipili hoho vijiko vitatu, chembechembe za pilipili manga, kijiko kimoja, chembechembe za pilipili hoho kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, maji ya wanga vijiko vitatu

Njia

1. kata doufu iwe vipande, halafu weka kwenye maji ya moto, tia chumvi .

2. koroga kamba-mwakaje pamoja na chumvi, maji ya wanga, halafu weka kwenye sufuria yenye mafuta ikaange halafu ipakue.

3. washa moto na mimina mafuta kwenye sufuria, tia sosi ya pilipili hoho, tia chembechembe za pilipili hoho, mimina supu, tia vipande vya doufu na kamba-mwakaje, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa sosi, tia chembechembe za kukoleza ladha, baada ya dakika 1, mimina maji ya wanga, korogakoroga, halafu tia chembechembe za pilipili manga. Ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.