Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-23 21:02:48    
Kujikinga dhidi ya tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini kwa njia ya kisayansi

cri

Kutokana na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya watu na mabadiliko ya muundo wa chakula, sifa ya afya ya watu pia imeendelea kuboreka. Lakini pamoja na hali hiyo, tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini ambalo linahusiana kwa karibu na tabia za chakula limeanza kuwasumbua watu wengi, hata limeanza kutokea kwa watoto na vijana. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni zimeonesha kuwa nchini China hasa kwenye miji mikubwa, tatizo hilo hata limekuwa moja ya magonjwa makubwa kwa watoto na vijana.

Katika hospitali nchini China kuna watu wengi waliogunduliwa kuwa na tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini au waliokwenda kutafuta matibabu ya tatizo hilo. Tatizo hilo ni mabadiliko ya kipathaolojia yaliyosababishwa na kuwa na mafuta kupita kiasi kwenye chembechembe za maini. Hivi sasa tatizo hilo limekuwa ugonjwa wa pili wa maini nchini China baada ya homa ya manjano iliyosababishwa na virusi, na tatizo hilo linatambuliwa kuwa ni chanzo cha ugonjwa wa maini kuwa ngumu. Takwimu hizo zimeonesha kuwa, mwaka 2001 asilimia 19.3 ya watu wa China waligunduliwa kuwa na tatizo hilo, ilipofika mwaka 2003 idadi hiyo ilifikia asilimia 25.3. Kwa kuangalia hali ya jumla nchini China, tatizo hilo linaathiri watu wengi na idadi ya watu waliopatwa na tatizo hilo imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Je ni watu gani wanaweza kupatwa na tatizo hilo? Mkurugenzi wa idara ya maambukizi ya magonjwa katika hospitali ya 302 ya jeshi la ukombozi la China Bi. Zhang Hongfei alisema:

"tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini linasababishwa na sababu mbalimbali. Ya kwanza ni tabia mbaya za maisha, kama vile kula chakula kingi na kutofanya mazoezi; ya pili ni kutokana na maini yalidhuriwa na dawa. Aidha, kuna vyanzo vingine vya kibaiolojia, kama vile homa ya manjano iliyosababishwa na virusi pia inaweza kuleta madhara hayo."

Profesa Zhang Hongfei alisema, tabia mbaya za maisha ni sababu ya kwanza kwa tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini, na asilimia 80 ya wagonjwa wa tatizo hilo wanatokana na sababu hiyo. Hasa tabia ya kunywa pombe kwa kuwa pombe ni muuaji mkubwa wa maini. Tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini ni ugonjwa wa kawaida wa maini, kama linatibiwa ipasavyo tatizo hilo linaweza kuondolewa. Kwa hivyo ugunduzi mapema ni muhimu sana kwa kuzuia na kuboresha maendeleo ya tatizo hilo. Lakini uchunguzi unaonesha kuwa wagonjwa wengi hawatilii maanani tatizo hilo, hata baadhi yao hawakupata matibabu kwa wakati kwa visingizio mbalimbali. Mgonjwa mmoja alisema"

"nadhani hili si tatizo kubwa, linaweza kuondolewa kwa kudhibiti ulaji wa chakula, yaani kupunguza unywaji wa pombe."

Lakini kama tatizo hilo halidhibitiwi ipasavyo, linaweza kusababisha matokeo mabaya, hasa linaweza kuendelea kuwa homa ya manjano, ugonjwa wa maini kuwa ngumu na hata kuwa satarani ya maini. Profesa Zhang Feihong alisema:

"tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini ni msururu wa magonjwa wala si ugonjwa wa pekee. Tatizo hilo likiendelea, litakuwa homa ya manjano, halafu litakuwa ugonjwa wa maini kuwa ngumu, likiendelea zaidi litaweza kusababisha saratani ya maini."

Profesa Zhang pia alisema, tatizo hilo halina dalili maalumu wala vigezo vya upimaji, hivyo si rahisi kuligundua. Lakini kutokana na maendeleo ya teknolojia ya upimaji wa kimatibabu, hasa teknolojia za CT, upimaji kwa kutumia mionzi ya ultrasonic, imekuwa rahisi zaidi kwa watu kujikinga na kugundua mapema tatizo hilo. Na kama watu wakigunduliwa kupatwa ugonjwa huo, wanapaswa kufanya nini0?

Kwanza, wanapaswa kutafuta vyanzo vya tatizo hilo na kuchukua hatua kuviondoa. Kama vile wanywaji pombe wanapaswa kuacha kunywa pombe, wagonjwa wa kisukari wenye tatizo hilo wanapaswa kudhibiti ipasavyo kiwango cha sukari kwenye damu. Kuondolewa kwa vyanzo kama hivyo kutasaidia matibabu ya tatizo hilo.

Pili, wagonjwa wanapaswa kurekebisha muundo wa chakula na inafaa kula chakula chenye kiwango cha juu cha protini na vitamin, na kiwango cha chini cha sukari na mafuta. Profesa Zhang alisema:

"wagonjwa wa tatizo la kuwa na mafuta kwenye maini lililosababishwa na uzito kupita kiasi wanachukua asilimia kubwa kati ya wagonjwa wote wa tatizo hilo, uzito wa kupita kiasi unahusiana na tabia za kula chakula. Kwa hivyo wagonjwa hao wanapaswa kula chakula chenye kiwango cha chini cha sukari na mafuta. Pia wanapaswa kula chakula taratibu, na kula kiasi kinachohitajika na wala si kushiba kabisa."

Aidha, wagonjwa wa tatizo hilo pia wanapaswa kufanya mazoezi ili kuhimiza matumizi ya mafuta mwilini. Profesa Zhang akipendekeza alisema kuwa:

"wakati wa kufanya mazoezi, watu wanapaswa kuzingatia mambo matatu, yaani kiasi cha mazoezi, njia za mazoezi na muda wa kufanya mazoezi. Tunapaswa kufanya mazoezi mara mbili kila siku, na nusu saa kila mara mpaka jasho linatutoka. Kama tunaweza kushikilia kufanya mazoezi kama hayo mara 3 hadi 5 kila wiki, itatusaidia kujikinga dhidi ya tatizo hilo."

Mwishoni profesa Zhang alisema, wagonjwa wa tatizo hilo hawapaswi kutumia ovyo dawa za kujenga afya, kwa kuwa kama dawa hizo zitatumiwa kwa makosa, huenda zitaongeza shinikizo kwa maini na kulifanya tatizo hilo liwe kubwa zaidi.