Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bi. Melissa Fleming tarehe 23 amethibitisha kuwa Iran imekubaliana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kuwa, mwezi Mei itaeleza wazi mpango wake wa nyuklia unaoshukiwa kuendeleza utafiti wa kutengeneza silaha za nyuklia kwa Shirika hilo. Imefahamika kwamba kitendo hicho kinahusiana na ziara ya naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Olli Heinonen nchini Iran.
Bw. Olli Heinonen aliwasili Teheran tarehe 21 na kisha alifanya mazungumzo ya faragha na pande husika. Vyombo vya habari vinasema lengo la ziara ya Bw. Hainonen lilikuwa ni kuihimiza Iran ieleze wazi mpango wake unaoshukiwa kuendeleza utafiti wa kutengeneza silaha za nyuklia kisirisiri kwa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki. Habari kutoka serikali ya Iran zinasema ziara ya Bw. Heinonen nchini Iran ni ya kawaida katika msingi wa ushirikiano kati ya Iran na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, pande mbili zitazungumzia ushirikiano huo kwa kina zaidi. Tarehe 23 Bi. Melissa Fleming alipozungumza na waandishi wa habari alisema katika siku mbili nchini Iran ujumbe ulioongozwa na Bw. Heinonen umekubaliana na serikali ya Iran kwamba Iran itashirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kufanya uchunguzi kuhusu shutuma ya kuwa Iran inatengeneza silaha za nyuklia. Amesema ana matumaini kuwa mwezi Mei Iran itatoa ushahidi unaotakiwa kwa Shirika la Kimataifa ili kuondoa shutuma hizo. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Mohamed el Baradei alisifu kitendo hicho cha Iran na kusema kwamba hii ni kumbukumbu ya kihistoria na kusema kwamba lengo la jumuyia ya kimataifa ni kutaka kuelewa vilivyo shughuli za nyuklia zilizofanywa zamani na sasa, na ana matumai kuwa atapata maelezo wazi kutoka kwa Iran kabla ya yeye kutoa ripoti kwa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki mwishoni mwa Mei.
Lakini je Iran inatakiwa kueleza wazi masuala gani kwa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki? Wachambuzi wanasema hivi sasa masuala yanayotaka kuchunguzwa na Shirika hilo, ni pamoja na hali ya kuendeleza makombora ya "Shabab-3", sababu ya kufanya jaribio la bomu kali linaloripuka chini ya ardhi kwa kudhibitiwa mbali na shughuli za kusafisha uranium. Baadhi ya nchi za Magharibi zina wasiwasi kuwa utafiti huo pengine unahusiana na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia na kusema kwamba Iran pengine inajenga maabara chini ya ardhi kwa ajili ya kufahamu ukali wa mlipuko wa bomu la nyuklia. Lakini mara kadhaa Iran inakataza shughuli za utafiti wa matengenezo ya silaha za nyuklia na kusisitiza kwamba mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya kuendeleza viwanda na kuongeza mafuta na gesi ya asili kuuzwa nchi za nje. Kutokana na kuwa Iran inakataa kusimamisha shughuli za kusafisha uranium Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara tatu lilifanya uamuzi wa kuiwekea vikwazo Iran.
Ingawa Iran inasisitiza mara kwa mara kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani, nchi za Maghariki zinazongozwa na Marekani zinaendelea kuishuku Iran kujaribu kuwa na silaha za nyuklia na kuiwekea shinikizo siku hadi siku. Tarehe 22 Februari mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohamed el Baradei kwenye ripoti yake kuhusu suala la nyuklia la Iran alisema, uwazi wa mpango wa nyuklia wa Iran umekuwa mkubwa kwa kiasi kikubwa, hata hivyo mpango huo unatakiwa uelezwe wazi zaidi kuhusu masuala yanayotiwa wasiwasi. Mwishoni mwa mwezi Mei Bw. Baradei atatoa ripoti nyingine kuhusu suala la nyuklia la Iran. Vyombo vya habari vinaona kuwa kukubaliana huku na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kueleza wazi "mpango wa nyuklia" kumeonesha kwamba kwa kiasi fulani msimamo mgumu wa Iran umebadilika. Shirika la Habari la Iran limesema kwamba ofisa mmoja wa Iran aliyeshiriki kwenye mazungumzo alisema mlango wa Iran kwa ajili ya kufanya mazungumzo uko wazi, na Iran itaendelea kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kwa kina zaidi.
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 23 alisema, Iran iko tayari kufanya mazungumzo na pande mbalimbali kuhusu suala la nyuklia, na inakaribisha kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo na kwa msingi wa kuheshimiana, lakini haitasimamisha shughuli zake za kusafisha uranium kutokana na shinikizo la jumuyia ya kimataifa.
|