Hivi karibuni kutokana na bei ya nafaka kupanda kwa kasi, jumuyia ya kimataifa imeshikwa na wasiwasi, "msukosuko wa nafaka" limekuwa ni jambo linazumgumzwa miongoni mwa watu, bei ya nafaka na mafuta limekuwa suala linalofuatiliwa sana na jumuyia ya kimataifa, na baadhi ya mashirika ya kimataifa yanaona kuwa msukosuko wa nafaka umeikumba dunia nzima. Lakini mkurugenzi wa kitengo cha soko na biashara katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa Bw. Abdolreza Abbassian anaona vingine. Alisema,
"Ni kweli msukosuko wa chakula umeikumba dunia nzima? Kama ilinganishwe na hali ya maafa ya njaa mwaka 1973 iliyotapakaa dunia nzima, hali ya sasa haiwezi kuitwa msukosuko wa chakula duniani. Kwa sababu mwaka 1973 hata ukiwa na pesa hikuwa rahisi kupata chakula. Kutokana na huduma ya chakula, hivi sasa tuna nafaka za kutosha."
Kuhusu sababu za kupanda kwa bei ya nafaka Bw. Abdolreza alieleza,
"Sababu kubwa ni kuwa hali ya hewa mbaya imesababisha uzalishaji wa nafaka kupungua katika nchi zinazouza nafaka kwa nchi za nje na akiba ya nafaka duniani haikuwa ya kutosha. Zaidi ya sababu hizo bei kubwa ya mafuta imesababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji wa nafaka. Hali ya vurugu sokoni inasababishwa na sababu nyingi toka hali ya hewa mbaya hadi kushuka kwa thamani ya dola ya Marekani, na bei kubwa ya mafuta na hali ya kuyumbayumba ya soko la fedha. Ingawa sababu hizo hazihusiani na kupanda kwa bei ya nafaka moja kwa moja lakini zinaleta hali ya utatanishi na kusababisha bei ya nafaka kutokuwa tulivu."
Baadhi ya vyombo vya habari vinaona kuwa kupanda mimea kwa ajili ya kutengeneza mafuta ni sababu kubwa inayosababisha kupanda sana kwa bei ya nafaka. Bw. Abbassian pia anaona vingine, yeye anaona kuwa hii kweli ni sababu muhimu lakini sio ya kimsingi. Pia alikanusha kuwa kupanda kwa bei ya nafaka kunatokana na China na India kununua nafaka kutoka nchi za nje. Alisema,
"China na India, kwanza nchi hizo zimehakikisha kujitosheleza mahitaji yao wenyewe, na zaidi ya hayo zinauza nafaka kiasi fulani katika nchi za nje. Shirika la chakula na kilimo halina haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maendeleo yao ya haraka ya kiuchumi yatasababisha msukosuko wa nafaka duniani, huu ni upuuzi. Ongezeko la mahitaji ya nchi hizo linatokana na sababu mbili, moja ni ongezeko la idadi ya watu na lingine ni ongezeko la mapato. Lakini maongezeko hayo yameleta ongezeko la uwekezaji katika kilimo na kuchochea uzalishaji wa nafaka, kwa hiyo hili ni jambo zuri." Kadhalika, Bw. Abbassian alisifu sera zilizochukuliwa na China katika kuhakikisha usalama wa chakula. Alisema kutokana na sera nzuri China imepata maendeleo makubwa katika uzalishaji wa nafaka na mboga, mwaka huu serikali ya China imepandisha bei ya kununua mazao kutoka kwa wakulima ili kuhamasisha uzalishaji wao.
Hivi sasa suala wanalolifuatiliwa ni lini bei ya nafaka itapungua. Bw. Abbassian alisema, kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Chakula duniani, mwaka huu uzalishaji wa nafaka utaongezeka, kama hali ya dharura haitatokea bei ya nafaka ingeweza kupungua katika majira ya siku za joto, lakini kiasi cha kupungua kwa bei hakitakuwa kikubwa, bei ya nafaka itaendelea kuyumbayumba mpaka mwaka kesho. Bw. Abbassian alisema, ingawa hivi sasa bado hatujakumbwa na msukosuko wa nafaka, haimaanishi kuwa tunaweza kuuacha bila kushughulikia suala la sasa. Alisema hali ya hivi sasa haijawahi kutokea tangu mwaka 1973, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa yanapaswa kujifunza kutoka mambo ya zamani na kujaribu kuyatatua masuala ya sasa, tusipoyashughulikia tutakumbwa na msukosuko wa kweli.
Idhaa ya kiswahili 2008-04-25
|