Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-25 20:25:02    
China na Afrika ni marafiki wazuri wa kutegemeana

cri

China na Afrika ni marafiki mazuri wa kutegemeana, zinaelewana, kuheshimiana, na kuungana mkono katika mambo ya kimataifa, ambazo ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya kusini na kusini katika uhusiano wa kimataifa. Baada ya kuingia katika karne mpya, mawasiliano kati ya viongozi wa China na nchi za Afrika na ushirikiano katika mambo ya kimataifa unaendelea kuimarishwa, utaratibu wa mazungumzo ya kisiasa ya pande mbilimbili kati ya China na nchi za Afrika ulianzishwa, na baada ya kuaizishwa kwa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2000, utaratibu wa mazungumzo ya pande mbalimbali kati ya China na nchi za Afrika umeanzishwa, na kutia nguvu mpya kwa uhusiano kati ya China na Afrika.

China inaihitaji Afrika, maneno hayo si matupu, bali ni ya halisi. Baada ya vita vya baridi, hadhi ya kisiasa ya Afrika ingawa ilielekea kushuka chini, lakini hadhi na umuhimu wake katika mikakati ya kidiplomasia ya China havikubadilika. Ingawa nchi nyingi za Afrika bado ziko nyuma kimaendeleo, lakini nchi nyingi za Afrika zina hali sawasawa na misimamo inayofanana, katika mambo ya diplomasia ya pande mbalimbali, moyo wa uungaji mkono ni muhimu sana. China inahitaji uungaji mkono wa nchi za Afrika, na imepata uungaji mkono wa nchi za Afrika katika masuala ya Taiwan, Tibet, kujiunga na WTO, kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki, kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa maonesho ya kimataifa na kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Afrika siku zote ni sehemu muhimu ya kufanya shughuli za kidiplomasia kwa China. Nchi 53 za Afrika, hasa nchi 47 zilizoanzisha uhusiano wa kibalozi na China zimepanua maeneo ya kufanya shughuli kwa China katika jukwaa la kimataifa. Historia na uzoefu vimethibitisha kuwa, nchi za Afrika ni rafiki mtiifu wa China, kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika kuna umuhimu wa kimkakati katika kuinua athari ya China duniani na kuimarisha msimamo wa kidiplomasia wa China.

Hivi sasa katika hali ya utandawazi wa uchumi duniani, na hali ya kisiasa ya kimataifa yenye mabadiliko mengi na utatanishi, nchi za Afrika zinatilia maanani hadhi na umuhimu wa China, ili kujitoa kutoka hali ya taabu ya umaskini na kuwekwa ukingoni, nchi za Afrika zinataka kupata msaada na uungaji mkono wa China. China ikiwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, siku zote inasimama kwenye upande wa nchi za Afrika na kuunga mkono maombi na mapendekezo yao halali. Katika miaka ya hivi karibuni, uaminifu wa kisiasa na ushirikiano kati ya China na Afrika unaendelea kuimarishwa, katika masuala makubwa ya kimataifa, China huitikia maombi ya nchi za Afrika na kudai mageuzi ya Umoja wa Mataifa ya maanani zaidi suala la maendeleo, kuongeza uwakilishi wa Afrika katika mageuzi hayo na kuunga mkono pendekezo la Afrika kuhusu pande mbalimbali. Aidha China inaunga mkono juhudi za nchi za Afrika za kutafuta ushirikiano ili kujiendeleza, China inaunga mkono Umoja wa Afrika kwa pendekezo lake la kutatua masuala ya Afrika kwa kujiamulia, na China imefanya juhudi kushiriki kwenye kampeni ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa barani Afrika na kwenye majadiliano ya Umoja wa Mataifa yanayohusu mambo ya Afrika. Tokea mwaka 1990, China imetuma askari 3,000 kwa ujumla kwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Liberia na nchi nyingine za Afrika kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa. Na ili kuzisaidia nchi za Afrika kutekeleza mpango wa NEPAD, China iliongeza msaada wa kiuchumi kwa Afrika na kupunguza au kusamehe madeni ya nchi za Afrika, na kuzisaidia nchi za Afrika kutatua matatizo yanayozikabili katika kufungua soko, kutoa mafunzo kwa watu, kinga na tiba ya magonjwa na uhifadhi wa mazingira.

China na Afrika zote zinatafuta nia ya kujiendeleza kwa amani, pande hizo mbili ni nguvu imara ya kulinda amani na utulivu wa dunia. Hivi sasa ushirikiano na uhusiano kati ya China na Afrika katika mambo ya kimataifa unaendelezwa kwa kuelekea kufanya juhudi za kufuata hali halisi, kufanya ushirikiano wa pande mbalimbali na kuweka utaratibu husika. Waraka wa sera za China kwa Afrika uliotolewa na serikali ya China mwezi Januari mwaka jana ulipanga mwelekeo wa kuendeleza ushirikiano wa kirafiki kati yao kwenye sekta muhimu katika kipindi kipya na kutangaza China inapenda kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa aina mpya wenye uaminifu wa kisiasa na kuwa na usawa, uhusiano huo unalingana na matakwa ya amani na maendeleo katika zama za hivi sasa, na pia unalingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa China na Afrika na watu wa dunia, na utasaidia kujenga utaratibu wa kimataifa ulio wa uwiano, utulivu na masikilizano.

Habari nyingine zinasema mwenyekiti wa chama cha umma cha Togo Bw. Solitoki Esso ambaye alimaliza ziara yake nchini China hivi karibuni, alisifu sana mafanikio yaliyopatikana nchini China katika ujenzi wa uchumi, hasa mradi wa magenge matatu ya Mto Changjiang na mabadiliko makubwa ya miji ya Beijing na Shanghai. Bw. Esso alisema kuna uhusiano mzuri kati ya chama cha kikomunisti cha China na chama cha umma cha Togo na kati ya nchi hizo mbili. Ujumbe wa Togo ulioongozwa naye ulikaribishwa kindugu na kirafiki nchini China. Alisema kabla ya miaka kumi iliyopita aliwahi kuzuru China, lakini safari hii alitembelea tena China ambapo hata alishindwa kutambua sehemu alizotembelea zamani kwa sababu maendeleo na mabadiliko ya China ni makubwa sana.