Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-28 19:42:00    
Msitu wa mawe yenye maandiko ya maneno ya kumbukumbu

cri

Katika kipindi hiki cha leo, tunawafahamisha kuhusu msitu wa mawe yenye maandiko na michoro ya kumbukumbu ulioko mjini Xian, mkoa wa Shanxi, sehemu ya kaskazini magharibi ya China. Kundi hilo la mawe ya kumbukumbu linachukua nafasi ya kwanza kwa wingi wa mawe ya kumbukumbu yanayohifadhiwa nchini China, na kusifiwa kama ni jumba la makumbusho ya sanaa ya maandiko ya hati za mkono na sanaa ya uchongaji kwenye mawe.

Mawe yenye maandiko ya maneno ya kumbukumbu yalichukua nafasi muhimu katika utamaduni wa kale wa China. Zamani za kale, wachina walikuwa wanachukulia mawe yaliyochongwa maandiko ya maneno kama ni vitu vya kumbukumbu au alama fulani, wakati mwingine ilani pia zilichongwa kwenye mawe. Mawe hayo ni vitu muhimu vinavyoonesha mabadiliko ya historia na sanaa ya maandiko ya hati ya maneno ya kale.

Msitu wa mawe ya kumbukumbu ya mji wa Xian ni mahali yanapokusanywa mawe ya kumbukumbu ya zamani za kale ya China, sasa umebadilika kuwa jumba la makumbusho maalumu ya kuonesha mawe ya kumbukumbu ya zamani za kale ya China na "maktaba ya vitabu vya mawe". Mkuu wa jumba hilo la makumbusho, Bw. Zhao Liguang alisema, historia ya msitu wa mawe ya kumbukumbu wa Xian ukiwa mahali pa kukusanya mawe ya kumbukumbu ya kale, ilianza mwaka 1087, zaidi ya miaka 900 iliyopita, alisema,

"Katika mwaka wa pili wa Yuanyou ya enzi ya Song ya kaskazini, yaani mwaka 1087, kutokana na kusimamiwa na Lu Dazhong ambaye alikuwa ni kiongozi wa tume ya usimamizi wa uchukuzi wa majini, watu walisafirisha baadhi ya mawe maarufu ya kumbukumbu hadi kwenye sehemu ile ya sasa ya kuhifadhi mawe ya kumbukumbu, ambayo yaliweka msingi wa 'msitu wa mawe ya kumbukumbu'. Hapo baadaye mawe ya kumbukumbu yaliongezeka na kufanyiwa matengenezo katika enzi za Jin, Yuan, Ming na Qing, hatimaye yakafikia kiwango cha hivi sasa."

Sehemu hiyo ya Xian imehifadhi mawe ya kumbukumbu ya kale karibu elfu 4 ya enzi mbalimbali za zaidi ya miaka 2,000 iliyopita. Profesa wa chuo kikuu cha Hannan cha Japan, Bw. Yamamoto Kenji alivutiwa sana na mawe hayo ya kumbukumbu, alisema,

"Mawe ya kumbukumbu yanayohifadhiwa kwenye msitu wa mawe ya kumbukumbu ni vitu vya mabaki vya utamaduni vyenye thamani kubwa sana, mawe mengi ya kumbukumbu ya enzi mbalimbali yamekusanywa hapa, ni vitu vyenye thamani kubwa sana kwa watafiti wa maeneo mbalimbali."

Huko pia unaweza kuona mawe kadhaa ya kale ya China yaliyochongwa maneno ya lugha za nchi za kigeni, moja kati ya mawe hayo ni jiwe maarufu sana duniani la "Jiwe la China kuhusu kuenea kwa dini ya Jing ya Daqin" "Daqin" ni jina la nchi ya kifalme ya Rome ya mashariki lililoitwa na wachina katika zamani za kale, "dini ya Jing" ni tawi moja ya dini ya kikristo, jiwe hilo lilichongwa mwaka 781 likielezea kuenea wa dini ya Jing nchini China, fundi aliyechonga maneno kwenye jiwe hilo, alichonga majina ya watawa 72 wa dini ya Jing kwa maneno ya lugha ya Syria ya kale na lugha ya Kihan ya China, tena ilichongwa alama ya msalaba ya dini ya kikristo kwenye sehemu ya juu ya jiwe la kumbukumbu. Katika miaka ya hivi karibuni, maneno yaliyochongwa kwenye jiwe hilo yanafuatiliwa na watu wengi wa duniani, na yanachukuliwa kuwa ni dira muhimu katika utafiti kuhusu maingiliano ya kirafiki kati ya enzi za kale za China na Ulaya na Asia ya kati.

Watazamaji licha ya kuweza kusoma historia kutoka kwenye mawe hayo ya kumbukumbu, pia wanaweza kushuhudia sanaa ya maandiko ya hati ya mkono ya China. Maneno ya mawe mengi hayo ya kumbukumbu, yaliandikwa na mabingwa maarufu wa kuandika maandiko wa zamani za kale wa China, maandiko ya hati zao za mkono yanachukuliwa kuwa mfano wa kuiga katika sanaa ya kuandika hapa nchini China. Profesa wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Chaoyang, Taiwan, Bi. Geng Huiling anafurahia sana mawe hayo ya kumbukumbu, alisema,

"Ingawa msitu wa mawe ya kumbukumbu wa Xian una historia ya miaka 920, lakini utamaduni uliopo kwenye mawe hayo ya kumbukumbu ni utamaduni wa China wa miaka elfu 5 iliyopita. Sanaa ya maandiko ya maneno ya hati ya mkono ni sanaa maalumu katika utamaduni wa China, maneno yaliyochongwa kwenye mawe hayo yanaonesha uzuri wa sanaa na ukweli wa mambo halisi."

Moja ya mawe hayo ya kumbukumbu linaloitwa "Dibaji ya Dini Takatifu" linafuatiliwa na watu wengi. Watu wanaofahamu sanaa ya maandiko ya maneno ya hati ya mkono ya China, wanaweza kutambua mara moja kuwa maneno hayo ni hati ya Wang Xizhi, bingwa maarufu wa sanaa ya maandiko ya maneno ya hati ya mkono wa kale wa China, lakini mambo yaliyosimuliwa na maneno hayo ni ya makala iliyoandikwa na Xuan Zhuang, mtawa wa ngazi ya juu katika miaka 200 baada ya Wang Xizhi kufariki dunia. Hii inaonesha kuwa maandiko ya maneno yaliyochongwa kwenye jiwe hilo hayakuandikwa na Wang Xizhi mwenyewe, bali yalichukuliwa na kuchongwa na fundi mkubwa kutoka katika maandiko ya maneno yaliyoandikwa na Wang Xizhi kutokana na maelekezo ya mtawa mwingine wa ngazi ya juu. Mawe ya kumbukumbu yaliyoko kwenye msitu wa mawe ya kumbukumbu, yana umaalumu mkubwa wa kichina, ambao uliorodheshwa kuwa sehemu 50 zenye maana kubwa zaidi kwa watalii wa nchi za kigeni. Hivi sasa msitu huo wa mawe ya kumbukumbu unatembelewa na watalii wengi sana kila siku.

Jumba la makumbusho ya msitu wa mawe ya kumbukumbu wa Xian inatarajia kutumia Yuan milioni 300 kufanya ujenzi wa upanuzi, ili kufanya maeneo ya maonesho kupanuliwa maradufu kuliko ya hivi sasa. Ofisa wa jumba hilo la makumbusho hayo, Bw. Qiang Yue alisema, wana mpango wa kujenga "msitu wa mawe ya kumbukumbu ya teknolojia ya tarakimu".

"Tunatarajia kufanya majaribio ya kujenga 'msitu wa mawe ya kumbukumbu wa teknolojia ya tarakimu', na kufanya baadhi ya mawe ya kumbukumbu kusanifiwa kuwa video ya katuni, na kupeleka habari kuhusu mawe hayo ndani ya simu za mkononi za watazamaji kwa teknolojia ya Bluetooth, watazamaji wakizifungua kwenye simu zao, wanaweza kuona maneno, video, picha na alama za mawe hayo ya kumbukumbu, hatua ambayo inasogeza zaidi utamaduni ulioko kwenye mawe ya kumbukumbu na watazamaji"