Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-29 19:12:15    
Bw. Michel Perrin kutoka Ufaransa na magurudumu ya chapa ya Michellin

cri

Kampuni ya Michellin ni moja ya makampuni maarufu inayotengeneza magurudumu duniani. Wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, watu watakaokuja Beijing kutazama michezo hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani wataweza kupanda mabasi yanayotumia magurudumu ya chapa ya Michellin. Magurudumu hayo yanatengenezwa na kampuni ya magurudumu ya Michellin mjini Shenyang.

Bw. Michel Perrin mwenye umri wa miaka 61 amefanya kazi katika kampuni ya Michellin kwa miaka 35. Aliwahi kuwa meneja mkuu wa viwanda vya Michellin nchini Ufaransa na Hispania. Kampuni ya Michellin ya mjini Shenyang ilianzishwa mwaka 1995, na Bw. Perrin alikuwa meneja mkuu wa kampuni hiyo. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ameishi mjini Shenyang kwa miaka mitatu na miezi miwili. Alifika Shenyang,katika majira ya baridi, lakini hakuogopa baridi ya huko, alisema,

"Ingawa nje kulikuwa na badiri, lakini nilikuwa na kazi nyingi kiwandani, hivyo nilisikia joto."

Bw. Perrin alisema alikwenda Shenyang China kutokana na changamoto ya kazi sababu ni changamoto. Akiwa ni mtu kutoka Ulaya, kujionea utamaduni wa China na kushiriki kwenye ujenzi wa China ni mambo ambayo anapenda kufanya. Hasa katika miaka kadhaa ijayo, kampuni hiyo mjini Shenyang itakuwa moja ya kituo kikubwa zaidi cha kutengeneza magurudumu ya magari. Habari hiyo ilimfurahisha sana, alisema,

"Magurudumu yanayotumiwa na mabasi mjini Beijing yanatengenezwa na kampuni yetu. Naona fahari kuwa mabasi hayo yatatumiwa kwenye michezo ya Olimpiki."

Licha ya mabasi mjini Beijing, mabasi ya miji ya Tianjin, Zhengzhou, Xiamen na Hangzhou pia yanatumia magurudumu ya chapa ya Michellin. Wakati Bw. Perrin ni meneja mkuu wa kampuni ya Michellin mjini Shenyang, kampuni hiyo ilisifiwa kuwa ni moja ya makampuni kumi yenye mitaji ya nje ambayo yanalipa kodi nyingi mjini Shenyang, na ilipewa tuzo ya kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza wajibu wa kijamii. Mwaka 2006, Bw. Perrin alichaguliwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa wa kufanya kazi kwa bidii mjini Shenyang, alikuwa ni mgeni pekee kati ya watu waliochaguliwa.

Msaidizi wake Bw. Gao Ni alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ni kweli Bw. Perrin anafaa kupewa sifa ya mfano mzuri wa kuigwa wa kufanya kazi kwa bidii. Kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, Bw. Perrin anafika kazini mapema zaidi kuliko watu wengine, na anachelewa kuondoka. Kila siku anafanya kazi kwa karibu saa 12, alisema,

"Kila siku anakuja ofisini saa 1 asubuhi, lakini jambo analofanya kwanza si kufanya kazi ofisini tu, bali anakwenda kukagua sehemu mbalimbali kiwandani kwanza."

Bw. Perrin anapenda kusikiliza maoni tofauti, kuwasiliana na watu wengine kwa makini. Ingawa amefanya kazi na wenzake kwa miaka mitatu, lakini hawajawahi kubishana.

Bw. Perrin anajivunia wafanyakazi wote wa kampuni yake. Anaona kuwa, wafanyakazi ni muhimu zaidi kuliko mashine kiwandani. Wafanyakazi wa mji wa Shenyang wanafanya juhudi kwenye kazi zao ili kupata maendeleo. Bw. Perrin alisema maendeleo ya kampuni yake katika miaka kadhaa iliyopita yalitokana na juhudi za wafanyakazi wa China, alisema,

"Shughuli kadhaa zinaendelea kwenye kampuni yetu, tunahitaji msaada wa wataalamu wachache kutoka nchi za nje, lakini tunategemea zaidi wafanyakazi wa China."

Kampuni ya kutengeneza magurudumu ya Shenyang inatoa msaada kwa vyuo vikuu na idara za huduma za jamii mjini Shenyang mara kwa mara, na wakati fulani Bw. Perrin alikwenda kuwatembelea watoto yatima na kuwapatia zawadi. Bw. Perrin alisema,

"Lengo la kampuni ya Michelllin si kufanya biashara tu, bali pia inawasaidia watu wanaohitaji msaada. Tunatoa msaada wa masomo kwenye chuo kikuu cha Kaskazini Mashariki ili kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi. Aidha tunatoa msaada kwa idara ya watoto yatima ya Shenyang ili kuwasaidia kuondoa matatizo yao. Hatufanyi mambo hayo mjini Shenyang tu, hilo ni wazo la Kampuni ya Michellin.

Bw. Perrin anapenda kula chakula cha Kichina, na wakati wa mapumziko, anapenda kusafiri katika sehemu mbalimbali nchini China. Miongoni mwa miji ambayo aliwahi kutembelea, anapenda zaidi miji ya Xi'an na Beijing. Anaona kuwa miji hiyo miwili ina historia ndefu. Anaweza kujua habari kuhusu mabadiliko ya enzi kwenye historia ya China. Pia ana hamu kubwa ya kujua historia ya Enzi ya Qing, hivyo anaupenda mji wa Shenyang. Ametembelea mara nyingi vivutio vya kihistoria, na amewahi kutembelea kasri la kifalme mara tatu, alisema,

"Marafiki zangu kutoka Ufaransa walipokuja kunitembelea, tulikwenda kutembelea kasri la kifalme. Niliwaelezea kuhusu vitu na matumizi ya vyumba mbalimbali kwenye kasri hilo, na nilipokumbuka hadithi za kasri hilo, niliwaambia."

Bw. Perrin ana watoto wawili, ambao wanafanya kazi nchini Ufaransa. Hivi sasa yeye na mkewe wanaishi mjini Shenyang. Wanapenda kutembelea mitaa mbalimbali mjini humo. Baada ya kuishi huko kwa miaka mitatu, amejionea mabadiliko yaliyotokea mjini humo, alisema,

"Mabadiliko yametokea katika sehemu mbalimbali, kwa mfano mitaa na majengo. Subway imeanza kujengwa mjini Shenyang, hayo ni mabadiliko makubwa zaidi. Katika miaka mitatu iliyopita, uchumi wa mji huu umepata maendeleo makubwa."

Wakati Bw. Perrin anapofanya kazi mjini Shenyang, alipata wajukuu. Alisema anapenda kuwapeleka mjini Shenyang, ili waone kasri la kifalme mjini humo. Mwandishi wetu alipomwuliza kama atatazama michezo ya Olimpiki ya Beijing katika majira ya joto, alisema,

"Napenda kutazama michezo hiyo, lakini ni vigumu kununua tikiti, nitajaribu kupata tikiti."