Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-05 20:22:25    
Tazama Tibet kutokana na historia yake

cri

Kwenye mkoa unaojiendesha wa Tibet, hivi sasa watu wanaishi maisha mazuri, wanapata elimu nzuri, wanapewa huduma za matibabu bure, na wengi wao wana nyumba za kudumu. Lakini miaka zaidi ya 50 iliyopita, Tibet ilitekeleza mfumo wa wakulima watumwa, na asilimia zaidi ya 95 ya watibet walikuwa wakulima watumwa.

Katika jumba la makumbusho ya historia la Tibet, kuna barua moja iliyoandikwa na kabaila mmoja kwa mwengine wakati wa mfumo wa wakulima watumwa. Kwenye barua hiyo kabaila huyo alisema alishindwa katika kucheza kamari na mwenzake, na atkampa farasi saba, kiasi fulani cha pesa na wakulima watumwa watatu. Kutokana na barua hiyo, tunaweza kujua kuwa kabla ya ukombozi wa Tibet, wakulima watumwa hawakuwa na haki za binadamau, na walichukuliwa kama ni bidhaa. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Tibet ya China Bw. Gelek aliyekuwa mtumwa wa kabaila alisema,

"Bibi yangu alikuwa mtumwa wa kabaila mmoja, lakini alitolewa kwa kabaila mwengine kama zawadi. Nilizaliwa kwenye zizi la ng'ombe. Nilizaliwa asubuhi, na alasiri ya siku hiyo mama yangu alikuwa lazima aende kufanya kazi kwani yeye alikuwa mkulima mtumwa."

Familia ya Bw. Gelek ilikuwa kwenye tabaka la chini kabisa wa ngazi ya wakulima watumwa wakati wa utekelezaji wa mfumo wa utawala wa ya kisiasa na kidini, hawakuwa na vyombo vya uzalishaji wala haki za binadamu, na walichukuliwa na makabaila kama ni mifugo walioweza kusema, waliishi kwenye mazizi ya ng'ombe, na kufanya kazi ngumu kila siku.

Kijiji cha Sesin kiko umbali wa kilomita zaidi ya 70 kutoka mji wa Lhasa. Chini ya mwangaza mzuri wa jua, watoto wanacheza kwa furaha. Lakini miongo kadhaa iliyopita, sehemu hiyo ilikuwa mashamba ya ukoo wa Dalai Lama. Kutokana na kutoweza kuvumilia mateso, baadhi ya wakulima watumwa waliwahi kutoroka kwa pamoja. Mzee Chos Phel na dada yake mkubwa Drolma Yuzhen walikuwa wawili kati yao. Bw. Chos Phel alisema watoto wa hivi sasa wanaishi maisha ya furaha, lakini zamani alipokuwa mtumwa mwenye umri mdogo, maisha yalimaanisha kuwa ni taabu kwake, alisema,

"Tulikuwa tunafanya kazi ngumu mchana kutwa na usiku kucha, tulichoka sana mpaka tulikuwa tunalala chini ya ardhi. Mbali na hayo hatukuwa na chakula cha kutosha, mara kwa mara tulikumbwa na njaa."

Bibi Zhuoma alisema wakati huo walikuwa wanateswa vibaya na makabaila, wakichelewa kufanya kazi walichapwa viboko na kupigwa kwa mawe, mwishoni baadhi ya wakulima watumwa hawakuweza kuvumilia na walitoroka.

Kabla ya ukombozi, watoto wengi walikuwa wakulima watumwa au watumwa mara baada ya kuzaliwa kwao. Walikua wakikumbwa na njaa, baridi na hofu. Kutokana na mazingira mabaya, watoto wengi walikufa kwa njaa, magongjwa au ajali. Wakiwa na bahati nzuri na kukua kuwa watu wazima, walilazimishwa kufanya kazi ngumu sana. Wakati huo wakulima watumwa walikuwa wanachukua zaidi ya asilimia 95 ya idadi ya watu wa Tibet, na wao walidhibitiwa na sufii wa ngazi ya juu, makabaila na maofisa, ambao hawakufikia asilimia 5 ya idadi ya watibet, lakini walimiliki karibu mali zote za Tibet. Mwaka 1959 kabla ya mageuzi ya kidemokrasia, mkoani Tibet kulikuwa na familia 197 za warithi wa makabaila na familia 25 za makabaila makubwa, na miongoni mwao familia kubwa zaidi zilimiliki mashamba ya malefu ya hekta.

Mtaalamu wa taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Tibet ya China Bw. Zhou Yuan alisema,

"Undani wa mfumo wa wakulima watumwa chini ya utawala wa kisiasa na kidini wa Tibet ni masufii wa ngazi ya juu na makabaila kuwatawala kidikteta wakulima watumwa. Walikuwa wakiritimba wa vyombo vya uzalishaji nawakulima watumwa wa Tibet, hivyo waliwakandamiza na kuwanyonya kikatili wakulima watumwa. Huu ni msingi wa mfumo wa zamani wa wakulima watumwa wa Tibet."

Zamani serikali ya mtaa ya Tibet ilikuwa na mamlaka ya kuanzisha mahakama na jela, hata baadhi ya masufii walikuwa na mamlaka hiyo, na adhabu dhidi ya wakulima watumwa zilikuwa za kinyama, adhabu hizo zilikuwa kama vile kukata mikono na miguu, kutoa macho au ulimi na kubandua ngozi. Zamani chini ya kasri la Potala kulikuwa na shimo lililojulikana kama shimo la nge. Shimo hilo lililowekwa nge wengi wenye sumu lilichimbwa kwa ajili ya kuwaua wakulima watumwa.

Mwingereza mmoja aitwaye Charles Bell alisifiwa kuwa ni mtu anayeijua Tibet. Alijionea hali halisi ya zamani ya Tibet. Kwenye kitabu chake cha "Dalai Lama" alisema kama mtu kutoka Ulaya au Marekani akienda Tibet, hali ya sehemu hiyo itamrudisha kwenye zama za miaka mia kadhaa iliyopita.

Mwaka 1959, kutokana na matakwa ya wakazi wa Tibet na baadhi ya watu wa ngazi ya juu wa sehemu hiyo, mfumo wa utumwa uliodumu kwa miaka zaidi ya mia moja ulitokomeza mkoani Tibet. Mageuzi ya kidemokrasia yalifanyika, serikali ya kujiendesha ilianzishwa, na mamilioni ya wakulima waliokuwa wakulima watumwa walianza kuwa na haki ya kujiamulia. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Tibet ya China Bw. Gelek alisema,

"Tuna uhakika kuwa mageuzi ya kidemokrasia ya mwaka 1959 ni mwanzo wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya Tibet, kwa kuwa mageuzi hayo yana maana tatu muhimu, kwanza, wakulima watumwa waliokombolewa walianza kuwa na haki ya kusema na kupiga kura za uchaguzi, pili wakulima watumwa hao walianza kutambua kwa mara ya kwanza kuwa, jamii ya zamani ilikuwa ni jamii isiyo na haki, tatu, kutokana na mageuzi hayo, ardhi iligawanywa kwa watu wote wa Tibet."

Tangu kuanzishwa kwa mkoa unaojiendesha wa Tibet mwaka 1965, watibet walianza kuwa na haki ya kupiga kura za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sheria za China kuhusu uchaguzi. Sasa asilimia 70 ya maofisa na watumishi wa serikali ya Tibet wanatoka kabila la Watibet na makabila mengine madogo madogo.