Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-07 20:58:24    
Mapishi ya kukaanga bilinganya

cri

Mahitaji

Bilinganya moja, maji ya limao vijiko vitano, chembechembe za jibini, vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, wanga vijiko vitano, sukari kijiko kimoja, maji ya wanga vijiko viwili.

Njia

1. menya maganda ya bilinganya, likateliwa vipande vidogo vya mraba, halafu choronga kipande cha bilinganya, koroga pamoja na chumvi. Halafu tia wanga kwenye bilinganya.

2. washa moto, halafu tia bilinganya kwenye sufuria, kaanga mpaka iwe rangi ya hudhurungi. Ipakue.

3. washa moto tena, tia maji ya limao, chembechembe za jibini, sukari, chumvi, maji ya wanga korogakoroga halafu mimina kwenye bilinganya. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.