Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-09 16:09:47    
Kampuni ya Tasly ya China yajiendeleza barani Afrika na kuenzi dawa za China zenye sifa nzuri

cri

Kampuni ya dawa ya Tasly ya Tianjin, China na Idara ya usalama wa afya ya umma ya serikali ya mji wa Johannesburg, Afrika kusini na Kamati ya utaalamu wa dawa za asili ya Afrika Kusini hivi karibuni ziliitisha kongamano la kwanza kuhusu "dawa za mitishamba za kichina zaingia barani Afrika", ambapo wajumbe wa wizara ya afya ya Afrika kusini, Kamati ya utaalamu wa dawa za asili ya Afrika kusini, maofisa wa Idara ya usalama wa afya ya umma ya serikali ya mji wa Johannesburg pamoja na wajumbe wa ubalozi mdogo wa China huko Johannesburg, ofisi ya uchumi na biashara ya China nchini Afrika kusini na wataalamu na wasomi wahusika wa China walihudhuria kongamano hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Kampuni ya dawa ya Tasly ya Tianjin inayoshughulikia biashara ya dawa za kichina ilikwenda barani Afrika kujulisha dawa za jadi za kichina ambazo zinatengenezwa kwa teknolojia za kisasa, baada ya kutoa mafunzo kuhusu utamaduni wa dawa za kichina na kutembeza bidhaa, dawa hizo zimekaribishwa na watu wa Afrika, ambapo zinatiliwa maanani na kutambuliwa na serikali za nchi mbalimbali za Afrika.

Baada ya kuingia kwa karne ya 21, wimbi la kupenda vyakula na dawa za asili na zisizo na uchafuzi limetokea kote duniani. Afrika kusini pia ina historia ndefu ya kutumia dawa za mitishamba za huko kwa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Kwenye kongamano hilo, konsela mkuu wa China huko Johannesburg Bw. Tang Qingheng alisema, dawa za mitishamba za kichina zilitokana na mfumo mkubwa wa ustaarabu na falsafa za China zenye taaluma, dawa hizo za kichina zitaendelea kuleta manufaa kwa watu. Kongamano la "dawa za mitishamba za kichina zaingia barani Afrika" litasaidia kuongeza urafiki kati ya wananchi wa China na Afrika Kusini, pia zitanufaisha afya za wananchi wa nchi hizo mbili. Alieleza matumaini yake kuwa Kampuni ya dawa ya Tasly na makampuni mengine ya China yatatumia mbinu za kisayansi na kiteknolojia, usimamizi wa kisasa na uzoefu wa Kimataifa katika kueneza dawa za mitishamba za kichina na kuendesha biashara ya dawa hizo, kushirikiana na Afrika kusini katika kuendeleza dawa za mitishamba za kichina na dawa za mitishamba za Afrika kusini, ili kusaidiana na kupata maendeleo ya pamoja, kufanya juhudi za kutafiti na kuendeleza dawa za mitishamba za kichina, kutoa mafunzo yanayohusika na kufanya mawasiliano ya Kimataifa, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kuendeleza dawa za mitishamba za kichina.

Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa umma ya serikali ya mji wa Johannesburg Bw. Thuliva Nderwath alisema kwenye kongamano hilo kuwa, baada ya dawa za mitishamba za kichina hasa dawa hizo zilizotengenezwa na Kampuni ya dawa ya Tasly kuingia nchini Afrika Kusini, dawa hizo zimeendelezwa kwa kasi kwenye msingi wa urafiki wa jadi kati ya China na Afrika, na kukaribishwa na watu wa Afrika kusini. Dawa za aina mbalimbali zimetiliwa maanani na kutambuliwa na serikali ya Afrika kusini. Na mwezi Agosti mwaka 2006 dawa za aina 7 zilizotengenezwa na Kampuni ya dawa ya Tasly zimepata zabuni kwenye mpango wa serikali ya mji wa Johannesburg kuhusu kuongeza uwezo wa kinga, Kampuni ya Tasly ya Afrika Kusini imekuwa kampuni ya kwanza ya kutoa dawa za mitishamba za kichina zenye uwezo wa kusaidia watu kuongeza uwezo wa kinga mwilini katika serikali ya mji wa Johannesburg.

Mwenyekiti wa Kamati ya utaalamu wa dawa za asili ya Afrika Kusini Dr. Issac Kekana alisema, utamaduni kuhusu dawa za mitishamba za kichina na elimu ya China kuhusu afya za watu zimeenezwa nchini Afrika kusini, na mafunzo ya kiwango cha juu kuhusu matibabu na elimu yanatambuliwa na Kamati ya utaalamu ya dawa za asili ya Afrika Kusini, Kampuni ya dawa ya Tasly imekubaliwa na kamati hiyo ya Afrika Kusini kuwa mjumbe wake. Ili kuishukuru Kampuni ya dawa ya Tasly kwa mchango wake mkubwa kwa ajili ya kuboresha kiwango cha matibabu ya Afrika Kusini, Dr. Issac Kekana kwa niaba ya Kamati ya utaalamu wa dawa za asili ya Afrika Kusini alitoa tuzo kwa meneja mkuu wa Kampuni ya dawa ya Tasly Bw. Yan Xijun.

Meneja mkuu wa Kampuni ya dawa ya Tasly Bw. Yan Xijun alitoa hotuba kuhusu "uvumbuzi na uendelezaji wa teknolojia ya dawa za mitishamba za kichina" kwenye kongamano hilo, akitoa mfano wa kutengeneza dawa ya kisasa ya mitishamba ya kichina ya matibabu ya ugonjwa wa moyo, alithibitisha kuwa kuendeleza dawa mpya za mitishamba za kichina kunapunguza muda, nguvu na gharama, na pia kunakidhi sana mahitaji ya huduma za afya barani Afrika.

Bw. Yan alisema, baada ya kuanzisha tawi lake nchini Afrika Kusini mwaka 2002, Kampuni ya dawa ya Tasly ikitegemea mafanikio yake ya kutengeneza dawa kwa njia ya kisayansi, imehimiza mchakato wa kutengeneza dawa za kisasa za mitishamba za kichina na kuziuza duniani. Baada ya kujiendeleza kwa miaka mitano, kampuni hiyo imeanzisha matawi 7 na ofisi 20 pamoja na maduka 200 nchini Afrika Kusini, Swaziland, London ya mashariki, Durban, na Msumbiji, na mfumo wa uuzaji wa dawa za mitishamba za kichina umeundwa kwenye ngazi mbalimbali. Hivi sasa thamani ya uuzaji wa bidhaa kwa mwaka wa Kampuni ya dawa ya Tasly imefikia dola za kimarekani milioni 80.

Idhaa ya kiswahili 2008-05-09