Kutokana na mwaliko wa serikali ya Japan, rais Hu Jintao wa China alifanya ziara ya kiserikali nchini Japan kuanzia tarehe 6 hadi 10 May. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi aliyefuatana na rais Hu katika ziara yake hiyo alisema, ziara hiyo imepata mafanikio makubwa.
Wakati wa ziara hiyo, pande mbili zimetoa "Taarifa ya pamoja ya China na Japan kuhusu kuhimiza uhusiano wa kunufaishana wa kimkakati kwenye sekta mbalimbali". Katika taarifa hiyo ya pamoja, pande mbili zimedhihirisha kuwa, China na Japan ni wenzi wa ushirikiano, kila upande siyo tishio kwa upande mwingine, na kila upande unaunga mkono maendeleo ya amani ya upande mwingine, na pande hizo mbili zitashikilia kufanya mazungumzo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya nchi hizo mbili, kuongeza mawasiliano kati ya viongozi wakuu, na kuendelea na mazungumzo kuhusu ulinzi wa usalama.
Aidha, ziara hiyo ya rais Hu Jintao nchini China itazidisha ushirikiano wa kunufaishana kwenye sekta za uchumi na biashara. Rais Hu Jintao alisisitiza kuwa, pande mbili za China na Japan zinapaswa kusaidiana katika mambo ya uchumi, na kuinua sifa ya biashara kati ya nchi hizo mbili. Rais Hu Jintao amependekeza kuimarisha zaidi ushirikiano katika kazi za kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira, kufanya juhudi kubwa za kuhimiza ushirikiano kati ya makampuni ya nchi hizo mbili, na kuimaisha ushirikiano kati ya China na Japan katika mambo ya uchumi ya kikanda na Kimataifa.
Rais Hu Jintao alidhihirisha kuwa, kupanua mawasiliano ya utamaduni kati ya wananchi wa China na Japan ni njia yenye ufanisi na inayotegemewa zaidi kwa kuongeza maelewano na hisia za kirafiki kati ya wananchi wa China na Japan. Alipotoa hotuba kwenye Chuo kikuu cha Waseda cha Japan alisema, mustakabali mzuri wa urafiki kati ya China na Japan utawategemea vijana na chipukizi wa nchi hizo mbili, na watu wote wanatakiwa kufanya juhudi kwa pamoja ili urafiki kati ya China na Japan udumu kizazi baada ya kizazi. Maneno yake ya dhati yamewavutia watu wengi.
Rais Hu Jintao pia alidhihirisha kuwa, usitawi na neema za Bara la Asia haziwezekani kutengana na usawazishaji na ushirikiano kati ya China na Japan. Pande mbili za China na Japan zimeamua kufuata kanuni za ufunguaji mlango, uwazi na uvumilivu katika kuhimiza ushirikiano wa kanda ya Asia ya mashariki, na kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza kazi ya kuijenga Asia yenye amani, usitawi, utulivu na ufunguaji mlango.
|