Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-12 16:20:12    
Kuna haja kubwa ya kuharakisha mchakato wa siasa wa Darfur

cri

Serikali ya Sudan tarehe 10 mwezi Mei ilitangaza kuwa ilivunja mashambulizi yaliyofanywa na kundi la watu wenye silaha wa Darfur wanaoipinga serikali ya nchi hiyo dhidi ya Khartoum, Mji mkuu wa nchi hiyo. Baadaye rais Omar al-Bashir wa nchi hiyo tarehe 11 mwezi huu alitangaza nchi yake kusimamisha uhusiano kati yake na Chad kwa kuwa mashambuzi hayo yaliungwa mkono na nchi hiyo. Hali hii imeonesha kuwa kazi ya dharura ya sasa ni kuharakisha kuhimiza kundi la upinzani la nchi hiyo kujiunga na mchakato wa utatuzi wa suala la Darfur.

Tarehe 10 alasiri, watu wenye silaha wa kundi la upinzani la Darfur JEM walijaribu kufanya mashambulizi na kupambana na jeshi la serikali ya nchi hiyo kwenye sehemu ya Omdurman iliyoko kaskazini magharibi mwa Khartoum. Baada ya mapambano yaliyodumu kwa saa 5, serikali ya Sudan ilifanikiwa kuzuia mashambulizi hayo na kuwaangamiza na kuwakamata baadhi ya washambuliaji. Tarehe 11 mwezi huu, rais al-Bashir alitangaza nchi yake kusimamisha uhusiano wa kibalozi na Chad, alisema ni lazima Chad iwajibike na tukio hilo. Siku hiyo serikali ya Chad ilitoa taarifa ikisema inasikitishwa na uamuzi wa Sudan. Siku moja kabla ya hapo, Chad ilikanusha lawama kuwa nchi hiyo inaunga mkono kundi la upinzani la Darfur kushambulia Khartoum.

Wachambuzi wanaona kuwa tukio hilo ni shambulizi la kwanza lililozushwa na kundi la upinzani dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo tangu mgogoro wa Darfur ulipozuka mwezi Februari mwaka 2003. Tukio hilo litatatanisha zaidi mgogoro kati ya kundi la upinzani na serikali ya nchi hiyo. Kwa upande mwingine hali hiyo pia imeonesha kuwa sasa kuna ulazima kuharakisha mchakato wa utatuzi wa suala la Darfur na kuhimiza kundi la upinzani la Darfur lirejee kwenye mazungumzo.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alilitaka kundi la upinzani la Darfur lijitahidi kutatua mgogoro huo kwa njia ya amani. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China pia alisema China inataka kundi hilo lishiriki mapema kwenye mchakato wa siasa na kurejesha mazungumzo na serikali ya Sudan ili kusaini mapema makubaliano ya amani ya Darfur na kutimiza amani, utulivu na maendeleo kwenye sehemu hiyo.

Jumuiya ya kimataifa inakubali mkakati wa "njia mbili" kuhusu suala la Darfur, yaani kufanya mchakato wa siasa na shughuli za kulinda amani kwenye sehemu ya Darfur ziende sambamba. Lakini hivi sasa mchakato wa siasa uko nyuma kidhahiri kuliko shughuli za kulinda amani. Jeshi la mseto la kulinda amani la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lilianza kutekeleza majukumu nchini Sudan kuanzia mwezi Januari mwaka huu. Kutokana na juhudi za pande husika, serikali ya Sudan na Umoja wa Mataifa zilisaini makubaliano kuhusu hadhi ya jeshi hilo, ambayo yatatoa mchango mkubwa kuboresha hali ya usalama wa sehemu ya Darfur. Lakini mchakato wa siasa umekwama kwa muda mrefu. Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Deng Alor alisema, hali hiyo inatokana na kuwa kuna vyama vingi vya upinzani na ni vigumu kwa vyama hivyo kufikia msimamo wa pamoja. Aidha nchi chache za magharibi zinazoliunga mkono kundi la upinzani la Darfur pia zimetoa athari kwa hali ya nchini humo. Kwa hivyo pande mbalimbali husika zinatakiwa kuondoa haraka vizuizi katika njia ya kusukuma mbele mchakato wa siasa na kuyahimiza makundi ya upinzani yashiriki mapema kwenye mchakato huo.