Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-14 17:27:03    
Mji wa Chongqing waweka mkazo katika kuingiza wataalamu wa hali ya juu kutoka sehemu nyingine

cri

Katika miaka ya hivi karibuni mji wa Chongqing ukiwa ni mji pekee unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu kwenye sehemu ya magharibu mwa China, umetilia maanani katika kuingiza wataalamu wa hali ya juu kutoka sehemu nyingine. Katika kipindi hiki, tutawaelezeni jinsi mji huo wenye mvuto mkubwa unaojistawisha kwa kuingiza wataalamu kutoka sehemu nyingine.

Mji wa Chongqing ukiwa ni mji mpya unatawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China, umedumisha ongezeko la kasi la uchumi kwa miaka 7 mfululizo. Katika mji huo wenye eneo la kilomita za mraba elfu 82.4 na wakazi milioni 32, nguvu kubwa ya msukumo wa maendeleo ya uchumi ni wataalamu hodari wanaotoka sehemu mbalimbali nchini China na kote duniani.

Bw. Chen Shu ni mmoja kati ya wataalamu hao. Yeye ni mkuu wa taasisi ya sayansi ya jamii ya mji wa Chongqing na naibu mkurugenzi wa kudumu wa kituo cha utafiti wa maendeleo ya serikali ya mji huo. Bw. Chen Shu pia ni mhariri mkuu wa jarida liitwalo "Mageuzi" linalofuatilia maendeleo ya mji wa Chongqing. Bw. Chen Shu alipozungumzia mabadiliko yaliyotokea mjini humo, alisema:

"mimi ni mmoja kati ya watu walioshuhudia maendeleo ya Chongqing. Katika miaka 10 iliyopita, nimeona mji huu ukibadilika kila mwezi, hata kila siku. Kwa kawaida ukikaa mjini Chongqing kwa muda mrefu, utazoea na hata kuchoshwa na mabadilikoa hayo, lakini mimi bado nafurahia mpaka sasa."

Tarehe 17 mwezi Julai mwaka 1997, muda mfupi tu baada ya mji wa Chongqing kuchaguliwa kuwa mji wa nne unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China, Bw. Chen Shu na madaktari wengine 38 walitumwa mjini Chongqing wakiwa ni kikundi cha kwanza cha wataalamu kushiriki kwenye ujenzi wa mji huo. Huo ni mpango ulioandaliwa na mji huo kuhusu kuingiza wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali kuu ya China. Baada ya mwaka mmoja, Bw. Chen Shu aliamua kubaki mjini humo. Bw. Shen Shu alisema, anapenda kufanya kazi mjini Chongqing hadi atakapostaafu, kwa kuwa mji huo umemfanya ajisikie nguvu ya uhai kwenye maisha. Bw. Shen Shu alisema:

"maendeleo ya mji wa Chongqing yamewapa watu matumaini, mji huo si wa kawaida, bali ni mji unaoonesha nguvu ya uhai ambayo inawapa watu wa China hata kote duniani matumami ya maendeleo, ndiyo maana wataalamu wengi wamekuja Chongqing."

Kama ilivyo kwa Bw. Chen Shu, mkuu wa chuo kikuu cha mawsiliano cha Chongqing Bw. Tang Boming pia ni mjenzi kutoka sehemu nyingine. Kabla ya kwenda kwenye mji huo, Bw. Tang Boming aliwahi kuwa profesa na mwalimu wa madaktari katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Nagaoka cha Japan. Ingawa maisha nchini Japan ni ya raha na starehe, lakini Bw. Tang Boming anataka nadharia alizojifunza nchini Japan ziweze kufanya kazi halisi na matokeo ya utafiti wake yaweze kutumika katika uzalishaji mali, kwa hivyo aliamua kurudi nchini China. Bw. Tang Boming alisema:

Kwa kuwa nilisomea mawasiliano, pamoja na shughuli za ujenzi wa madaraja, kutandika barabara na kuchimba mahandaki, masomo hayo yanahusiana na mambo mengi ya miradi halisi. Ingawa mambo ya nadharia yanaweza kutatuliwa kwenye maabara, lakini vipi utatatua masuala yanayotokea kwenye miradi halisi? Kazi hodari kabisa za maabara pia zinahitaji kufanywa na mafundi kwenye miradi halisi. Kwa hivyo nilikuwa na wazo la kurudi nchini China na kuchagua sehemu moja ambayo nitaweza kutoa mchango halisi na kuonesha ustadi wangu wa kitaaluma kuhusu ujenzi na miradi."

Mwaka 1999 ambao ulikuwa ni mwaka wa tatu baada ya mji wa Chongqing kuchaguliwa kuwa mji unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China, Bw. Tang Boming alipowatembelea jamaa zake mjini Chongqing, alisikia kwamba mji huo unahitaji sana wataalamu wa hali ya juu waliosoma ng'ambo, hivyo alikwenda kwenye idara ya usimamizi wa nguvukazi ya mji huo, Bw. Tang Boming alisema:

"nilipokewa kwa dhati. Katika siku ya pili iliyofuata, ofisa wa idara hii alikuja na kuzungumza nami. Kweli nilijisikia kwamba ujenzi wa mji huo unahitaji wataalamu. Kwenye mazingira ambayo hufahamu vizuri, idara hiyo inakupa misaada kadiri inavyoweza."

Baada ya kutafakari kwa miezi miwili, hatimaye Bw. Tang Boming aliamua kubaki mjini Chongqing. Bw. Tang Boming alisema:

"kwa upande wa kitaalumu, mji wa Chongqing ni mji mwenye milima na mabonde mengi, hasa una hali mbalimbali za madaraja, mahandaki, kijiolojia, msingi wa barabara n.k. ambazo zote zinahusishwa kwenye elimu ya mawasiliano kw njia ya barabara niliyoijifunza, hata unaweza kusema mji huo ni kama jumba kubwa la makumbusho ya mawasiliano nchini China, masuala yote yanayoweza kutokea yamewahi kutokea mjini humo."

Bw. Tang Boming alipokuwa naibu mkurugenzi wa idara ya barabara ya Chongqing, aliongoza na kushiriki kwenye utafiti wa miradi zaidi ya 20 na kutatua masuala halisi yaliyotokea katika mambo ya uzalishaji mali na usimamizi. Moja ya miradi aliyoshughulikia ni marekebisho ya usanifu wa barabara uliopunguza gharama za ujenzi kwa zaidi ya yuan milioni 60. kutokana na mchango huo, Bw. Tang Boming aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya barabara ya mji huo na kupewa tuzo ya mafanikio kwa wataalamu waliorudi nchini China baada ya kumaliza masomo ng'ambo.

Naibu mkurugenzi wa kudumu wa ofisi ya wataalamu ya kamati ya chama cha kikomunisti ya mji wa Chongqing Bw. Xie Xin alisema, katika miaka ziadi ya 10 tangu mji huo uanze kutawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China, Chongqing uliingiza wataalamu wengi wa hali ya juu. Bw. Xie Xin alisema:

"katika miaka hiyo, mji wa Chongqing umeweka mkazo katika kazi ya kuingiza wataalamu, hasa wataalamu wa hali ya juu na wenye moyo wa uvumbuzi ambao hawawezi kuandaliwa kwa muda mfupi. Kwa jumla tunaingiza wataalamu kutoka miji mingine au nchi za nje. Tumeingiza kwa njia mbalimbali wataalamu zaidi ya 800 wa hali ya juu na watu wenye shahada ya udaktari 290 wa taaluma zinazohitajika, pia mji huo ulisaini makubaliano na taasisi ya sayansi ya China kuwa taasisi ya utafiti wa software ya taasisi hiyo itahamishiwa rasmi kwenye eneo la viwanda vya elektroniki la Chongqing. Hatua hiyo imeziba pengo la kutokuwepo kwa taasisi ya viwanda hivyo kwenye sehemu ya kusini magharibi mwa China."