Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-15 18:53:09    
Wachina wanaoishi katika sehemu mbalimbali duniani wachangia kazi ya uokoaji kwenye sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi

cri

Baada ya tetemeko la ardhi kutokea kwenye sehemu ya Wenchuan mkoani Sichuan, China, wachina wanaoishi katika nchi mbalimbali duniani na wanafunzi wa China wanaosoma kwenye sehemu mbalimbali duniani wametoa michango kuonesha ufuatiliaji wao kwa watu wa sehemu zilizokumbwa na maafa.

Tarehe 14 asubuhi, wachina wanaoishi nchini Qatar na wajumbe wa kampuni za China walikwenda kwenye ubalozi wa China nchini Qatar kutoa michango, walisema wanataka kutoa mchango wao kadiri wawezavyo ili kuwasaidia watu wa sehemu zilizokumbwa na maafa.

Mwenyekiti wa Shirikisho kuu la wafanyabiashara wa China wanaoishi nchini Thailand ambalo ni kundi kubwa zaidi la wachina wanaoishi Thailand Bw. Wu Hongfeng na wajumbe zaidi ya 20 wa shirikisho hilo tarehe 14 alikwenda kwenye ubalozi wa China nchini Thailand kutoa michango ya Yuan laki 4.5 kwa sehemu zilizokumbwa na maafa mkoani Sichuan. Bw. Wu alisema:

"Tarehe 12 tetemeko kubwa lenye nguvu ya 7.8 kwenye kipimo la Richter lilitokea kwenye wilaya ya Wenchuan mkoani Sichuan, China, tulipopata habari hiyo tulishtuka sana, ili kueleza ufuatiliaji wetu na kuwapa pole watu wa sehemu zilizoathirika na maafa, tumetoa michango na kutaka kuchangia kazi ya kuwaokoa watu na kupambana na maafa".

Bw. Zhao Zihao na msafara wake wenye watu wanane kutoka sehemu ya mashariki ya Thailand siku hiyo saa 12 na nusu ya asubuhi walifika kwenye ubalozi wa China nchini Thailand kutoa michango yao. Bw. Zhao alisema:

"Tunataka kutoa nguvu na fedha zetu kidogo ili kuwasaidia ndugu zetu wanaoathirika na maafa. Tuna matumaini kuwa vikundi vya wachina wanaoishi nchini Thailand na watu wengine wenye moyo wa upendo wote watatoa misaada ili ndugu zetu waliokumbwa na maafa waweze kupunguza taabu na huzuni, hili ni jukumu letu".

Bibi Fang Hong ambaye amefanya biashara nchini Qatar kwa miaka 6 siku hiyo alikwenda kwenye ubalozi wa China nchini Qatar pamoja na watoto wake kutoa michango, alisema:

"Tarehe 13 nilitazama televisheni kwa siku nzima nikifuatilia hali ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Sichuan, nilipoona ndugu zetu waliokufa kwenye tetemeko la ardhi, niliona huzuni sana. Sisi wachina tunaoishi katika nchi ya nje, hatuwezi kuwasaidia moja kwa moja, ila kutoa michango kwa kuonesha moyo wetu. Nimeona waziri mkuu Wen Jiabao mwenye umri mkubwa ambaye amefika kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa kuongoza kazi ya kuwaokoa watu na kupambana na maafa, na watu wengi wa huko walimzunguka na kumwambia hali mbalimbali, waziri mkuu Wen Jiabao aliwajibu mmoja baada ya mwingine, hali ambayo ilitutia moyo sana. Nina imani kuwa, ndugu zetu wachina hakika watashinda maafa na kujenga upya maskani yao".

Na kocha wa mchezo wa mpira wa wavu wa China Bw. Yu Chonghua ambaye amefanya kazi nchini Qatar kwa zaidi ya miaka 10 siku hiyo pia alifika kwenye ubalozi wa China nchini Qatar kutoa michango. Alisema:

"Wachina wote wanaoishi katika sehemu mbalimbali duniani wanaona huzuni baada ya kuona tetemeko kubwa la ardhi kutokea nchini China, tunataka kutoa michango ili kueleza nia yetu ya kuwasaidia ndugu zetu. Hii imeonesha kuwa, wakati taifa letu linapokumbwa na taabu yoyote, sisi sote tunataka kulisaidia. Nina imani kuwa, chini ya uongozi wa chama na serikali ya China, hakika tutashinda maafa ya kimaumbile".