Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-16 16:05:37    
Maonesho ya kikundi cha nyimbo na ngoma cha Shenzhen cha China yaliyofanywa nchini Uganda

cri

Hivi karibuni maonesho ya michezo ya sanaa yenye mtindo wa kichina yalifanyika nchini Uganda, ambayo yametia uhai kwenye mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi hizo mbili. Alfajiri ya tarehe 30 mwezi Aprili, watu walijazana kwenye Jumba la maonesho ya michezo ya sanaa la taifa la Uganda huko Kampala. Mwendeshaji wa kikundi cha nyimbo na ngoma kutoka Shenzhen, China aliwajulisha watazamaji kuwa, tarehe 30 mwezi Aprili ilikuwa siku ya kubaki kwa siku 100 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, kuanza maonesho ya kikundi hicho kwenye nchi tano za Afrika kuna umuhimu mkubwa zaidi na anatarajia kuwa maonesho hayo yatawavutia wananchi wa Uganda na kuhimiza mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Maonesho hayo ya michezo ya sanaa yaliyofunguliwa, ngoma inayoitwa "kusherehekea sikukuu kwa furaha" iliwafurahisha mara moja watazamaji. Baadaye maonesho mazuri ya michezo ya sanaa iliifanya hali ya ukumbini ifikie kileleni. Ikilinganishwa na michezo mingine, michezo ya sarakasi ya China iliwavutia zaidi watazamaji wa Uganda. Sarakasi ya kuviringisha mwavuli kwa miguu ilichezwa kwa dakika chache tu, lakini iliwavutia sana watazamaji, na kupigiwa makofi kwa mara zaidi ya 10.

Katika maonesho ya saa mbili, wachezaji wa China walifanya maonesho ya ngoma zenye umaalum wa makabila madogomadogo ya China na michezo ya sarakasi na Wushu ya China, yaliwashangaza watazamaji wote na kupigiwa makofi na watu wengi. Waziri wa taifa wa Uganda anayeshughulikia mambo ya jinsia na utamaduni Bi. Rukia Isanga aliyetazama maonesho hayo, alishukuru sana kwa misaada inayotolewa na serikali ya China kwa nchi za Afrika katika sekta mbalimbali na akieleza matumaini kuwa Uganda inapenda kuzidisha mawasiliano na ushirikiano kwenye sekta ya utamaduni kwa kupitia juhudi za pamoja za idara za utamaduni za nchi hizo mbili.

Balozi wa China nchini Uganda Bw. Sun Heping alipotoa risala kwenye ufunguzi wa maonesho hayo, alijulisha maendeleo na mabadiliko ya eneo maalum la uchumi la Shenzhen na kusifu mawasiliano hayo ya utamaduni yanayosaidia kuhimiza maelewano ya wananchi wa nchi hizo mbili na kuzidisha urafiki kati yao. Kikundi cha nyimbo na ngoma cha Shenzhen kitakwenda Cameroon, Senegal, Cape Verde na Kenya na kufanya maonesho ya michezo ya sanaa na utamaduni wa jadi wa China kwa watazamaji wa huko.

Habari nyingine zinasema kampuni ya ujenzi wa mawasiliano ya China hivi karibuni ilitoa dola za kimarekani 20,000 kwa shule moja ya Nairobi nchini Kenya ili kuisaidia shule hiyo kujenga madarasa mapya mawili. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Meng Fengzhao alisema, tawi la kampuni ya ujenzi ya Luqiao nchini Kenya lilikamilisha ujenzi wa miradi mingi wenye sifa nzuri nchini Kenya tangu miaka ya 80 ya karne iliyopita na kutoa nafasi nyingi za ajira kwa ajiali wakazi wa huko. Kampuni hiyo inataka kutoa mchango ili kusaidia maendeleo ya mambo ya elimu ya Kenya na kusukuma mbele urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming alisema hii ni mara ya pili kwa kampuni ya China kutoa misaada ya elimu nchini Kenya na kuonesha urafiki wa jadi kati ya China na Kenya, na pia kuonesha moyo wa masikilizano na upendo wa Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Beijing. Shule ya Kenya iliyopewa msaada ilisema ili kuonesha shukurani zake kwa na msaada wa kampuni ya China, itayaita madarasa hayo mawili kuwa ni "madarasa ya Beijing".

Habari nyingine zinasema, kampuni ya miradi ya kijiolojia ya China na kampuni ya miradi ya kimataifa ya mafuta na kemikali ya China zilifanya sherehe ya kuunganisha mabomba ya kusafirisha maji kwenye jangwa la InSalah-Tamalasat nchini Algeria, na hii inamaanisha kuwa ujenzi wa mradi huo umeanza kwa pande zote. Kaimu wa balozi wa China nchini Algeria Bw. Ling Jun alitoa pongezi akieleza imani kuwa kutokana na juhudi za pamoja za makampuni hayo mawili, matatizo mbalimbali yataondolewa na sikuya kukamilika kwa ujenzi wa mradi na sifa ya mradi huo pia zitahakikishwa ili kuleta manufaa kwa serikali ya Algeria na wananchi wake. Watendaji wa makampuni hayo mawili pia walisema watafanya juhudi zote kukamilisha ujenzi wa mradi huo na kukidhi mahitaji ya wananchi wa huko, na kuufanya mradi huo uwe mradi mzuri kabisa na kutoa mchango kwa urafiki kati ya China na Algeria.

Mabomba hayo ya kusafirisha maji yana urefu wa kilomita 800 na yanagharimu dola za kimarekani zaidi ya milioni 800, na ujenzi wake unatazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2009. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo, tatizo la maji ya kunywa kwa watu wanaoishi kwenye sehemu ya jangwa ya kusini mwa Algeria litatatuliwa na maendeleo ya shughuli za utalii na ujenzi wa uchumi wa huko yatasukumwa mbele.

Mwezi Februari mwaka huu, rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria aliwahi kwenda kuhudhuria sherehe ya kuzinduliwa kwa mradi huo, na alisema mradi huo siyo tu ni mradi unaoonesha matumaini ya wananchi wa Algeria, bali pia ni mradi wa kisiasa, na mradi wa karne, hivyo ni muhimu sana kujenga vizuri mradi huo.

Idhaa ya kiswahili 2008-05-16