Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-20 20:47:14    
China na nchi za Afrika zanufaika kutokana na uzoefu wa maendeleo ya uchumi

cri

Maofisa wa serikali za nchi 17 za Afrika pamoja na maofisa wa wizara husika za China na wasomi maarufu wa nchini na nchi za nje, tarehe 20 walikuwa na mkutano hapa Beijing kujadili namna ya kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China. Mkurugenzi wa ofisi ya baraza la serikali inayohusika na kuzisaidia sehemu maskini kujiendeleza Bw. Fan Xiaojian alisema, China inapenda kuimarisha maingiliano na ushirikiano na nchi za Afrika katika eneo la kuzisaidia sehemu maskini kujiendeleza.

Kongamano la siku 10 la maofisa wa ngazi ya juu wa China na nchi za Afrika kuhusu kunufaika kwa pamoja kutokana na uzoefu wa maendeleo limezinduliwa leo, Bw. Fan Xiaojian alisema, China ni nchi kubwa kabisa inayoendelea duniani, na Afrika ni bara lenye nchi zinaloendelea lenye idadi kubwa ya watu maskini duniani, China na nchi za Afrika zote zinakabiliwa na jukumu kubwa la kutokomeza umaskini na kuleta maendeleo ya usiano ya jamii. Alisema,

"Tunapenda kunufaika kwa pamoja na nchi za Afrika kutokana na uzoefu wa kupunguza idadi ya watu maskini na maendeleo ya jamii, na kutoa uungaji mkono wa kiufundi unaohusika."

Bw. Fan Xiaojian alisema, China inapenda kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika ubanifu na utekelezaji wa sera na miradi ya kupunguza idadi ya watu maskini, na kuinua ufanisi wa jitihada hizo. Katika miaka ya hivi karibuni, nguvu za uchumi na kiwango cha maisha ya watu wa China vimeinuka, idadi ya watu maskini kwenye sehemu za vijijini imepungua hadi kiasi cha milioni 14 mwaka 2007 kutoka milioni 250 mwaka 1978. Idadi ya watu maskini iliyopunguzwa kati ya mwaka 1990 na mwaka 2007 inachukua 70% ya jumla ya idadi ya watu maskini iliyopunguzwa duniani.

Naibu waziri wa mipango wa Angola anayeshiriki kwenye kongamalo hilo, Bw. Carlos Alberto Lopes alisema, uzoefu wa maendeleo wa China ni muhimu sana kwa nchi za Afrika hususan Angola katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo. Alisema,

"Ninaamini kuwa kongamano hilo na ziara yetu kwenye sehemu ya mashariki ya China vitakuwa na umuhimu sana katika ongezeko tulivu la uchumi kwa nchi zetu."

Bw. Carlos Alberto alisema, nchi za Afrika zimejitahidi katika miaka michache iliyopita kwa ajili ya kutokomeza umaskini, na zimepata maendeleo, lakini bado zinakabiliwa na changamoto nyingi. Alisema maendeleo ya uchumi ya China ni mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi za Afrika. Uzoefu wa China unaziambia nchi za Afrika, zisikae kusubiri misaada ya nchi za nje, bali zisimame kidete kuyakabili matatizo yanayotokea katika maendeleo.

Mwaka 2007, ongezeko la uchumi wa Afrika lilizidi 6%, maendeleo ya uchumi ya nchi nyingi za Afrika ni tulivu, na uwekezaji katika nchi za Afrika unaongezeka, sasa China imekuwa mwenzi muhimu wa ushirikiano wa nchi za Afrika. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2007, China ilitoa misaada ya aina mbalimbali kwa nchi 53 za Afrika, ambazo zinahusu sekta za viwanda, kilimo, utamaduni, elimu, mambo ya afya, mawasiliano ya habari, umeme, uchukuzi na zana za umma. Serikali ya China imetoa misaada mingi ya vitu na teknolojia pamoja na mikopo isiyo na riba, imeanzisha ushirikiano na maingiliano na nchi za Afrika kuhusu uendelezaji wa rasilimali za nguvukazi, tena imepunguza au kusamehe madeni ya nchi 32 Afrika zenye matatizo makubwa zaidi ya uchumi.