Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-23 16:12:32    
Maisha ya Bw. Sun Baohua barani Afrika

cri

Bw. Sun Baohua ni mwalimu wa Kiswahili wa Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, amewahi kwenda Afrika ya Mashariki kwa mara nyingi. Ziara zake barani Afrika zilimsaidia sana kuinua kiwango chake cha lugha ya Kiswahili, pia zilimsaidia kwenye kazi zake za kufundisha lugha ya Kiswahili. Katika kipindi hiki, tutazungumza na Bw. Sun kuhusu maisha yake barani Afrika.

Q: Bw. Sun, nimeambiwa kuwa umewahi kwenda Tanzania mara tatu, tafadhali nijulishe kuhusu maisha yako nchini Tanzania.

A: Mara ya kwanza nilipokwenda Afrika, nilikwenda nchini Tanzania ambako niliishi kisiwani pemba,Zanzibar, serikali yetu ilikuwa imewajengea kiwanda cha kupasulia mbao maisha ya huko yalikuwa magumu kwani tulikuwa tunaishi katika vibanda na sio nyumba, na pia hakukuwa na wingi wa vyakula kama nchini China, kwa mfano haikuwa rahisi kuchagua nyama yoyote kwani huko Pemba hakukuwa na nyama ya Nguruwe yaani mkubwa wa meza.

Nilifanya kazi huko kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitano na katika muda muda huo uwezo wangu wa kiswahili uliongezeka kwani hata mswahili mmoja aliniambia kuwa nilipofika huko kiswahili changu kilikuwa cha vitabuni lakini sasa unaongea kama waswahili.

Mwaka 1981 hadi 1982 nilijiunga na chuo kikuu cha dar es salaam kusoma kiswahili ili kuongeza ujuzi na baada ya miaka miwili 1984 hadi 19985 niliitwa zanzibar kufanya kazi katika kiwanda ch Mahonda, pale tulifanya kazi ya matengenezo kwani kiwanda kile kilikuwa kimeharibika kabisa, na baada ya matengenezo ya mwaka mmoja kiwanda kile kilianza kuzalisha sukari kwa tani 6000 hivi kwa mwaka na wenyeji wa huko walifurahi sana.

Q: Mwaka 1990 ulikwenda Kenya kwa mara ya kwanza, niliambiwa kuwa ulikwenda Kenya ukiwa na lengo fulani,ni kweli?

A: Mwaka 1990 nilikwenda Kenya kwa mara ya kwanza,, lengo la safari ya hiyo ni kujua kiswahili kinavyotumika nchini Kenya maana kabla ya hapo watu waliniambia kuwa Kiswahili hakitumiki Kenya,basi nilipofika uwanja wa Nairobi na kumaliza shughuri za forodha nilimuuliza mfanyakazi mmoja "nyinyi mnazungumza kiswahili" na alinijibu " sana,ndio tunazungumza" kwa kweli moyo wangu ulitulia. Na katika miaka yote miwili huko nilitumia kiswahili na sikupata shida yoyote.

Q: Baadaye ulikwenda Kenya kwa mara nyingine?

A: Mwaka 1998 hadi 2000 nilikwenda tena Nairobi kufanya kazi katika kampuni ya China Road and Bridge, lakini wakti huo sikwenda kama mkalimani. Nilifanya kazi ya uongozi na kazi hiyo ilinichosha sana. Maana ilimbidi kushukughulikia kila kitu isipokuwa ujenzi wa barabara kwa kweli nakumbuka kuwa sikuwahi kulala kabla ya saa sita usiku, nilikuwa nashugulikia wafanyakazi zaidi ya 500, nyumba zao, mishahara yao na matatizo yoyote yanayowahusu, kwa kweli nilijifunza mengi na kutoa mchango wangu katika ujenzi wa barabara.

Q: Tafadhali tueleze maoni yako kuhusu waafrika uliokutana barani Afrika.

A: Kwa maoni yangu naona waafrika ni wakarimu hasa kwa wachina kwani kuanzia miaka ya sitini ya karne iliyopita China iliwapekelea wataalam na imewajengea miradi mbalimbali iliyowasadia kuinua maisha yao, mahali popote walisalimiwa nin hao hata na watoto.

Hivyo tulifanya kazi pamoja kwa kushirikiana na kuheshimiana, kuheshimiana ni jambo la muhimu kabisa wakati unapowasiliana na waafrika. Maana wote tuna mikasa ya kutawaliwa na wageni.

Q: Bara la Afrika ni bara linalowavutia watu. Sasa wachina wengi zaidi na zaidi wamekwenda Afrika kutalii, ukiwa mtu aliyewahi kuishi barani Afrika, unaweza kutoa mapendekezo kadhaa kuhusu utalii nchini Tanzania na Kenya?

A: Kama ukitaka kusafikiri katika Afrika ya mashariki nakushauri uende kwanza Tanzania sehemu za kaskazini ambako kuna mlima Kilimanjaro ambao unafunikwa na barafu na theluji kwa mwaka mzima, halafu utaenda katika Bonde la Ngorongoro, ambalo ni maarufu barani Afrika, halafu katika mbuga ya Manyara ambapo kuna wanyama wengi na ndege aina ya Flamingo wengi. Halafu unaweza kwenda Serengeti ambayo ni mbuga kubwa kabisa duniani kuna wanyama wengi na wa kila aina tena kuna chimbuko la binadamu wa kale kabisa katika bonde la Olduvai.

Halafu nakushauri uende Kenya, plae masai mara unaweza kuona uhamiaji wa wanyama, halafu unaweza kuangalia Flamingo utawaona katika ziwa na Nakuru, pia unaweza kwenda Mlima Kenya ambapo kileleni unafunikwa na barafu. Ukitaka kuona mambo ya kale ni bora uende Mombasa ambapo utaona nyumba nyingi za kiarabu na waswahili wa huko ndio wataalamu kabisa wa kiswahili.

Q: Asante sana Bw. Sun.

Idhaa ya kiswahili 2008-05-23