Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-26 21:30:52    
"Taarifa ya Pamoja" yaimarisha msingi wa mkakati wa China na Russia

cri

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Dmitri Medvedev wa Russia alifanya ziara rasmi ya siku mbili nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kufanya ziara katika nchi za nje na pia ni mara ya kwanza kwake kutembelea nchi isio ya Jumuyia ya Nchi Huru za Russia. Ziara yake inamaanisha kwamba urafiki mzuri kati ya China na Russia unaendelea na matokeo ya ziara hiyo yameimarisha zaidi uhusiano huo. Cha muhimu zaidi katika ziara hiyo ni "Taarifa ya Pamoja kuhusu Masuala Makubwa ya Kimataifa".

Taarifa hiyo ina vifungu 11 ambavyo licha ya kuwa na kanuni zinazotakiwa kufuatwa katika kuendeleza uhusiano kati ya nchi mbili, pia kuna mitazamo na utetezi kuhusu masuala makubwa ya kimataifa. Kwenye taarifa hiyo kifungu cha kwanza kimesisitiza kanuni tano za "kuheshimu mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi, kutongiliana mambo ya ndani", na pande mbili pia zina msimamo wa pamoja kuhusu kuheshimu heshima ya Umoja wa Mataifa, kupinga upangaji wa mfumo wa kukinga makombora, kupinga kutumia vigezo viwili tofauti katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuheshimu tamaduni za aina tofauti na kupinga kuingilia kati kwa kisingizio cha kutetea haki za binadamu.

Ni wazi kwamba vifungu hivyo vinalenga wazi mambo yaliyopo sasa. Mazingira yake ni kuwa China na Russia zinakabiliwa na matatizo ya namna moja ya kimataifa baada ya kumalizika kwa vita baridi, matatizo hayo yanatokana na Marekeni kujichukulia uamuzi, msimamo unaofuatwa na nchi za magharibi katika mambo ya diplomasia, vigezo tofauti vianvyotumika katika haki za biandamu n.k.. Hisia ya namna moja na matakwa kutokana na hisia hizo zimekuwa mhimili wa kuendeleza uhusiano kati ya China na Russia.

Tuangalie upande wa Russia, ingawa baada ya tukio la "Septemba 11" uhusiano kati ya Russia na Marekani ulikuwa mzuri katika mapambano dhidi ya ugaidi, lakini baadaye Marekani ilishutumu kwamba mchakato wa demokrasia "unarudi nyuma", na kuunga mkono wazi nchi za Jumuyia ya Nchi Huru za Russia zianzishe "mapinduzi ya rangi", uhusiano kati ya nchi mbili ukawa mbaya na uhusiano huo umekuwa mbaya zaidi kutokana na Upanuzi wa NATO kwenye mashariki na Marekani kujaribu kuanzisha mfumo wa kukinga makombora katika Ulaya ya Mashariki. Kutokana na hali hiyo ni haja kwa Russia kurekebisha sera zake kuhusu Mashariki na Magharibi. Tuangalie upande wa China, mashinikizo kwa China katika mambo ya uchumi, siasa, diplomasia na uuzaji wa silaha pia ni makubwa. Isitoshe, China imepata hisia nyingi kutokana na kuwa katika muda mfupi uliopita nchi za magharibi zilifanya matatam kwa kutumia fursa za michezo ya Olimpiki, vurugu za Tibet na masuala ya Taiwan.

Kutokana na hali hiyo ni haja kabisa kwa China na Russia kuimarisha uhusiano wao kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa kimataifa wenye haki.

Baara ya Putin kushika madaraka mwaka 2000 alikuwa anatilia mkazo uhusiano kati ya China na Russia. Mwaka 2001 nchi mbili zilisaini "Mkataba wa Ushirikiano na Urafiki kati ya Russia na China". Mwaka 2004 baada ya marais wa nchi mbili kukutana, uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi mbili umepande kwenye ngazi ya juu zaidi kutokana na utatuzi wa masuala ya mpaka, kuanzishwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kibiashara na utekelezaji wa "Mkataba wa Ushirikiano na Urafiki kati ya Russia na China".