Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-28 16:45:08    
Vyanzo vya tetemeko la ardhi

cri

Tarehe 12 mwezi huu tetemeTarehe 12 mwezi huu tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 8.0 kwenye kipimo cha Richter lilitokea kwenye wilaya ya Wenchuan mkoani Sichuan, na tetemeko hilo lilisikika kwenye miji na mikoa zaidi ya 10 nchini China na katika nchi za Vietnam na Thailand. je tetemeko la ardhi linatokea vipi? Kwa nini tetemeko hilo liliweza kuathiri eneo kubwa namna hii? ko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 8.0 kwenye kipimo cha Richter lilitokea kwenye wilaya ya Wenchuan mkoani Sichuan, na tetemeko hilo lilisikika kwenye miji na mikoa zaidi ya 10 nchini China na katika nchi za Vietnam na Thailand. je tetemeko la ardhi linatokea vipi? Kwa nini tetemeko hilo liliweza kuathiri eneo kubwa namna hii?

Kama upepo, mvua na umeme, tetemeko la ardhi pia ni hali ya kimaumbile inayotokea mara kwa mara duniani, tetemeko la ardhi husababishwa na kuvunjika au kugongana kwa miamba iliyoko kwenye sehemu zenye kina kikubwa chini ya ardhi, nishati kubwa iliyokimbikizika kwa muda mrefu ilitolewa ghafla na kusababisha kutetemeka kwa ardhi. Uchunguzi na ufuatiliaji wa muda mrefu umethibitisha kuwa tetemeko la ardhi hutokea kwenye sehemu yenye kina cha zaidi ya kilomita 10 hivi chini ya ardhi, yaani "chanzo cha tetemeko" kama tunavyoita.

Naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa fizikia ya dunia katika idara ya tetemeko la ardhi ya China Bw. Gao Mengtan alifanya utafiti kuhusu tetemeko la ardhi kwa miongo kadhaa. Bw. Gao Mengtan alisema, tetemeko la ardhi ni hali ya kimaumbile linalotokea mara kwa mara duniani, takriban linatokea kila siku, isipokuwa asilimia kubwa ya matetemeko hayasikiki, na yanasikika wakati yamekuwa na nguvu ya kiwango fulani. Bw. Gao Mengtan alisema:

"kama ukiwa kwenye sehemu ya katikati ya tetemeko la ardhi, yaani tetemeko likitokea kwenye mahali uliopo, kwa kawaida litasikika kama likifikia nguvu ya tatu kwenye kipimo cha Richter."

Kutokana na nguvu tofauti za tetemeko, wanasayansi waliyagawa matetemeko ya ardhi kuwa ya aina tofauti. Tetemeko lenye nguvu chini ya 3 huitwa tetemeko dogo, kwa kawaida, tetemeko kama hilo halisikiki; tetemeko lenye nguvu kati ya 3 hadi 4.5 linaitwa "tetemeko linalosikika", tetemeko la aina hiyo halileti uharibifu mkubwa; tetemeko kubwa lenye nguvu juu ya 8 litakuwa janga kubwa kwa binadamu, kwa mfano wa tetemeko la ardhi lililotokea huko Wenchuan mkoani Sichuan, hadi kufikia saa 6 mchana ya tarehe 27 limesababisha vifo vya watu 67183.

Bw. Gao Mengtan alisema, tetemeko la ardhi huenea kwa mawimbi yenye mielekeo miwili tofauti, wimbi kutoka chini ya ardhi linasababisha ardhi kutetemeka chini juu, wimbi jingine husababisha kuyumbayumba kwa ardhi. Njia hiyo ya kuenea kwa mawimbi ya tetemeko inasababisha maafa moja kwa moja, na inaenea kwa kasi zaidi kuliko ilivyofikiriwa. Bw. Gao Mengtan alisema:

"kwa kuwa wimbi la aina ya P na wimbi la aina ya S linaenea kwa kasi tofauti, lakini kwa wastani linaweza kuenea kwenye sehemu ya juu ya ardhi kwa kilomita kadhaa kila sekunde."

 

Kutokana na utafiti wa miaka mingi, wanasayansi wamegundua kuwa kutokea kwa tetemeko ni mchakato wa utatanishi, hata kama kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa, bado ni ngumu kuthibitisha kanuni zake.

Hivi sasa taarifa ya kimsingi tunayoijua kuhusu tetemeko la ardhi ni kuwa kuna ukanda mbili za tetemeko la ardhi duniani, yaani ukanda unaozunguka bahari ya Pasifiki na ukanda wa Mediterranean hadi mlima Himalayas. Sehemu za magharibi mwa China ziko kwenye ukanda wa pili, kwa hiyo China pia ni moja kati ya nchi duniani ambazo matetemeko mengi zaidi ya ardhi yanatokea.

Bw. Gao Mengtan alieleza kuwa dunia inaundwa na mabamba sita makubwa, kwenye sehemu ya juu ya ardhi mabamba hayo yanaungana, lakini kwenye sehemu ya kina zaidi kuna nyufa nyingi, nyufa hizo ni chanzo kikuu kinachosababisha tetemeko la ardhi. Kutokana na kusongamana kwa mabamba ya Ulaya na Asia, sehemu ya magharibi ya China ilivunjika kuwa vipande vidogo vidogo, sehemu hizo ndipo yanapotokea mara kwa mara tetemeko la ardhi. Bw. Gao Mengtan alisema:

"sehemu ya magharibi mwa China ina kanda zaidi ya 20 zenye nyufa, hasa sehemu zinazozunguka uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, kwa hivyo kutokana na hali ya kuenea kwa kanda za nyufa na ukali wao nchini China, matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea nchini China yalitokea kwenye sehemu ya magharibi."

 

Wilaya ya Wenchuan iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi iko kwenye ukanda mmoja mwenye nyufa. Matetemeko zaidi ya 10 ya ardhi yenye nguvu zaidi ya 6 kwenye kipimo cha Richter yalitokea kwenye sehemu hizo katika historia. Likilinganishwa na hali ya hao kabla, tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 12 mwezi huu liliathiri eneo kubwa zaidi na lilileta uharibifu mkubwa zaidi. Bw. Gao Mengtan alisema:

"kwa nini tetemeko hilo liliathiri eneo kubwa namna hii? Sababu ya kwanza ni kuwa tetemeko lenyewe ni kubwa hivyo lilitoa nguvu kubwa ya nishati, ndiyo maana liliathiri eneo kubwa sana, ya pili ni kuwa majengo ya sasa ni tofauti na yale ya zamani, miji mingi ina majengo marefu yenye ghorofa nyingi, mzunguko wa kutetemeka yenyewe kwa majenga hayo ni wa muda mrefu zaidi. Kwa hivyo majengo hayo yanaweza kutendeana na mawimbi ya tetemeko la ardhi."

Bw. Gao Mengtan alisema, tetemeko lolote la ardhi si tetemeko la peke yake, yaani tetemeko la ardhi huambatana na matetemeko mengi baadaye. Alisema kuwa baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, watu pia wanapaswa kuchukua tahadhari kuhusu uharibifu wa matetemeko yatakayofuata. Bw. Gao Mengtan alisema:

"baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea, ni kawaida kwamba linaambatana na matetemeko mengi ya baadaye. Tunapaswa kuepusha hasara katika matetemeko hayo yatakayofuata. La kwanza ni kutokaribia majengo yasiyo salama, halafu maafa ya kijiolojia hutokea baada ya tetemeko la ardhi, kama vile maporomoko ya ardhi, lazima tujiandae kwa ajili ya matukio kama hayo."