Tarehe 29 Mei ni siku ya kutimiza mwaka mmoja tangu rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria ashike madaraka ya utawala. Ili kusherehekea siku hiyo pamoja na wananchi wa nchi nzima, rais Umaru Yar'adua ametangaza kuwa tarehe ya 29 Mei ni siku ya mapumziko ya umma. Mtaalamu wa Nigeria ameona kuwa, katika mchakato wa mwaka wa kwanza wa utawala wa nchi hiyo, rais Yar'adua amefuata wazo la kufanya utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria, na kuweka msingi mzuri kwa ajili ya kutatua masuala mbalimbali yanayoikabili Nigeria.
Rais Umaru Yar'Adua alipoapishwa kuwa rais aliahidi kufanya juhudi zote katika ujenzi wa miundo mbinu nchini Nigeria, kukamilisha mfumo wa sheria wa kidemokrasia, kuboresha mazingira ya usalama wa umma na kuongeza nguvu ya kupambana na ufisadi. Profesa wa Chuo kikuu cha uhusiano wa Kimataifa cha Nigeria Bw. Bola Akinterinwa anaona kuwa, kazi za rais Umaru Yar'Adua zimepata ufanisi wa kiasi fulani, na wanaweza kusema kuwa, mpaka sasa kazi za rais Umaru Yar'Adua zimefanyika vizuri. Katika mwaka mmoja uliopita, rais Umaru Yar'Adua ameweka msingi mpya kwa ajili ya kuijenga Nigeria, msingi huo ni kuitawala nchi kwa mujibu wa sheria. Mpaka sasa wakuu kadha wa kadha wa majimbo waliondolewa madarakani kutokana na vitendo vyao vya ufisadi na kufanya udanganifu kwenye uchaguzi. Mwezi Machi mwaka huu, waziri wa afya na waziri wa taifa anayeshughulikia mambo ya afya waliondolewa madarakani kwa sababu ya kutuhumiwa kuiba mali ya taifa. Kesi kama hizo za kupambana na ufisadi zieonesha kazi za rais Yar'Adua za kufanya utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria.
Hivi sasa Nigeria inakabiliwa na matatizo mengi, tatizo moja ni upungufu mkubwa wa umeme. Mahitaji ya matumizi ya umeme ya nchi nzima ya Nigeria ni kilowati laki 2 kwa siku, lakini uwezo wa nchi hiyo ya kuzalisha umeme ni kilowati elfu 3 tu kwa siku. Ukosefu mkubwa wa umeme si kama tu umeathiri vibaya maendeleo ya uchumi, bali pia umeleta matatizo kwa maisha ya wananchi. Tatizo lingine ni shughuli zinazozidi kufanywa na wapinzani wenye silaha kwenye delta ya Niger, kuanzia mwaka 2006, watu hao wenye silaha wanaharibu majengo ya mafuta na kuwateka nyara wageni mara kwa mara. Hivi sasa watu zaidi ya 200 walikuwa wametekwa nyara, na uzalishaji wa mafuta ghafi nchini Nigeria pia umepungua kuwa mapipa milioni 2.1 kwa siku kutoka milioni 2.6 kwa siku. Baada ya kushika madaraka, rais Umaru Yar'Adua ametetea kufanya mazungumzo na wapinzani wenye silaha badala ya kuwaangamiza kwa njia ya kijeshi iliyochukuliwa zamani, lakini ufanisi wa utetezi wake bado ni mdogo. Profesa Akinterinwa alisema, hayo ni masuala yaliyobaki kwenye historia, ambayo hayawezekani kutatuliwa katika muda wa mwaka mmoja, na rais Umaru Yar'Adua ametunga mpango mzuri ambao utatekelezwa katika siku zijazo. Profesa huyo ameeleza imani yake kuwa, Mkutano wa Delta ya Niger utakaofanyika baada ya miezi miwili ijayo ni hatua kubwa anayochukua rais Umaru Yar'Adua, Mkutano huo hakika utapata matokeo yanayoweza kuhimiza zaidi juhudi za watu.
Baadhi ya wanasiasa wa Nigeria pia wametia mashaka yao juu ya uwezo wa utawala wa rais Umaru Yar'Adua, walisema Yar'Adua hana uwezo wa kutoa maamuzi. Shirikisho la vyama vya upinzani la Nigeria hata limemtaka Yar'Adua ajiuzulu wakati wa kutimiza mwaka mmoja tangu ashike madaraka. Profesa Akinterinwa alidhihirisha kuwa, namna ya kupata uelewa na uungaji mkono kutoka kwa wananchi wa Nigeria, hii itakuwa changamoto kubwa inayomkabili rais Umaru Yar'Adua. Profesa huyo alisema, changamoto hiyo imeletwa na wananchi wa Nigeria, ambao wanataka rais Umaru Yar'Adua aongoze mwelekeo wa njia yao ya kusonga mbele, na kupata uungaji mkono wa lazima. Wakati pengo la mawasiliano kati ya serikali na wananchi litakapoondolewa, ndipo nchi hiyo itakapopata maendeleo.
|