Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-30 20:56:02    
China, Afrika na Ulaya zajadili ushirikiano kwa Afrika kwenye hali ya utandawazi wa dunia

cri

Kongamano la kimataifa kuhusu ushirikiano na Afrika kwenye hali ya utandawazi wa uchumi duniani lilifanyika hapa Beijing hivi karibuni. Kongamano hilo liliendeshwa na shirika la mawasiliano ya kimataifa la China na Mfuko wa Friedrich Ebert Foundation wa Ujerumani, ambapo wataalamu, wasomi, wajumbe karibu 100 wa mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni kutoka China, Afrika na Ulaya walihudhuria kongamano hilo na kujadili namna ya kuanzisha kihalisi ushirikiano na Afrika chini ya hali ya utandawazi wa uchumi duniani.

Mshauri wa shirika la mawasialiano ya kimataifa la China ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa idara ya mawasiliano na nje ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Li Jinjun aliona kuwa kongamano hilo lina umuhimu mkubwa kwa ushirikiano kati ya China, Afrika na Ulaya na kusaidia nchi za Afrika kukabiliana na mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani. Alisema:

"Kongamano hilo lilijenga jukwaa la mawasiliano, wajumbe wa China, Afrika na Ulaya waliohudhuria kongamano hilo, walifanya mazungumzo ya kiujenzi kwa moyo wa usawa, urafiki na kuheshimiana kuhusu jinsi watakavyozidisha ushirikiano na Afrika na kuhimiza maendeleo ya Afrika, na kutoa mapendekezo mengi kwa maendeleo ya Afrika, kongamano hiyo lina umuhimu mkubwa."

Hivi sasa maendeleo ya mambo ya siasa, uchumi na jamii ya Afrika yameingia katika kipindi kipya, namna ya kukabiliana na hali ya kuendelezwa kwa kina kwa utandawazi wa uchumi duniani na kuharakisha maendeleo yake inafuatiliwa na nchi za Afrika na pia inafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa zikiwemo China na Ulaya katika mchakato wa kuimarisha na kuboresha ushirikiano na Afrika.

China ikiwa wenzi muhimu wa Afrika katika ushirikiano, inashikilia kanuni ya usawa na kunufaishana, na siku zote inashikilia kutohusisha misaada ya kiuchumi na mambo ya ndani ya Afrika, vitendo vya China vimekaribishwa na nchi za Afrika katika miaka zaidi 50 iliyopita.

Mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2006 hapa Beijing una umuhimu mkubwa katika historia ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika. Katika miaka miwili iliyopita, serikali ya China ilikuwa inatekeleza ahadi zake kwa Afrika hatua kwa hatua. Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Guijin katika kongamano hilo alieleza hali ya utekelezaji wa miradi kadhaa ya ushirikiano kati ya China na Afrika, akisema :

"hatua nane ziliyotolewa katika mwezi Novemba mwaka 2006 zinatekelezwa. Mfuko wa maendeleo ya China na Afrika umeanzishwa, na mikopo ya dola za kimarekani bilioni 5 umemaliza kupangwa. Aidha tumesaini makubaliano na nchi nyingi za Afrika kuhusu China kuzidi kufungua soko lake kwa nchi za Afrika zilizoko nyuma kimaendeleo."

Mjumbe kutoka Taasisi ya utafiti wa maendeleo ya chuo kikuu cha Dar es Salaam cha Tanzania Dr.Cosmas Aloys Kamugisha alisema:

"China na Tanzania zimeanzisha ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali. Hasa kwenye hali ya utandawazi wa uchumi duniani, China imetoa misaada mingi kwa Tanzania. Kwa mfano katika sekta ya kilimo, China inatusaidia kufanya utafiti wa tekenolojia na sayansi ya kisasa ya kuendeleza kilimo; China imetusaidia kuwaaandaa watu wenye ujuzi wa usimamizi wa viwanda na makampuni, China imefanya juhudi nyingi za kihalisi katika sekta mbalimbali."

Ofisa kutoka taasisi ya utafiti wa mambo ya uchumi ya Kenya Bw. Kwame Owino pia alieleza hali ya ushirikiano kati ya China na Kenya, akisema:

"Ushirikiano kati ya China na Kenya hasa kati ya China na Afrika unaimarishwa siku hadi siku. Rais Mwai Kibeki wa Kenya mwaka 2006 alihudhuria mkutano wa wakuu wa baraza la ushirkiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing. Kwenye mkutano huo, serikali ya China ilitoa sera kuhusu kuhamasisha makampuni ya China kwenda kuwekeza barani Afrika, na pia kuendelea kuhimiza kazi ya kubadilishana wanafunzi wa China na Afrika. Katika sekta za matibabu, China ilianzisha mradi wa utafiti wa kutibu ugonjwa wa malaria unaoenea barani Afrika. Katika mambo ya elimu, China ilianzisha chuo cha kwanza cha Confucius huko Nairobi nchini Kenya na kuongeza zaidi mawasiliano na urafiki kati ya China na Kenya na kati ya China na Afrika. Aidha China pia imetoa msaada mkubwa katika ujenzi wa miundo mbinu kwa Afrika."

Habari zinasema, ili kuendeleza vizuri zaidi uhusiano kati ya China na Afrika, China pia ilianzisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika miaka ya karibuni, kongamano hilo kati ya China, Afrika na Ulaya ni sehemu moja ya ushirikiano huo. Bw. Liu Guijin alisema:

"China, Afrika na Ulaya ni wanachama muhimu wa jumuiya ya kimataifa, sisi ni wenzi wakubwa wa ushirikiano na tunafanya juhudi kuhimiza amani na ustawi wa kudumu wa dunia. Hivi sasa uhusiano kati ya China na Afrika, kati ya China na Ulaya na kati ya Ulaya na Afrika ziko katika kipindi kipya muhimu. Maslahi ya pamoja ya pande hizo tatu yanapanua siku hadi siku, na zitatimiza mawasiliano mazuri na ushirikiano wa kunufaishana kwenye msingi wa kuheshimiana na kujadiliana kwa usawa."

Mjumbe wa Mfuko wa Friedrich Ebert wa Ujerumani nchini China Bw. Roland Feicht aliona kuwa, ushirikiano kati ya China, Ulaya na Afrika kwenye msingi wa kuaminiana na uhusiano wa kiwenzi pia ni mwelekeo wa ushirikiano wa kimataifa kwa hivi sasa. Akisema:

"kutokana na kuongezeka kwa umuhimu wa Afrika, kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika na Ulaya na Afrika ni mwelekeo wa alama katika uhusiano wa kimataifa. Kongamano hilo ni hatua mpya ya China na mfuko huo katika ushirikiano wa kimataifa pia ni uhusiano wa kiwenzi ulioanzishwa kwenye msingi wa uaminifu na kirafiki katikia miaka 20 iliyopita."

Profesa wa Chuo kikuu cha Nairobi Bw. Federick Quaye Gravenir katika mkutano huo alisema ana imani kubwa kwa ushirikiano kati ya China, Afrika na Ulaya. Akisema:

"Ushirikiano kati ya China, Afrika na Ulaya utakuwa na mustakabali mzuri, kwani ushirikiano kati ya pande hizo tatu utakuwa na ufanisi halisi zaidi kuliko ushirikiano kati ya Afrika na Ulaya na ushirikiano kati ya Afrika na America ya kaskazini, kwa sababu China na Afrika zina maslahi ya pamoja, China na Afrika zinasaidiana na kunufaishana."