Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-02 19:49:55    
"Mazungumzo ya Shangri-La" yatoa mapendekezo kuhusu usalama wa kikanda

cri

Mkutano wa 7 wa usalama wa Asia unaojulikana kama "Mazungumzo ya Shangri-La", ulifungwa tarehe 1 mwezi Juni huko Singapore. Katika muda wa siku tatu za mkutano huo, mawaziri wa ulinzi, wakuu wa majeshi, maofisa wa usalama na wataalamu kutoka nchi na sehemu 27 za Asia na Pasifiki walifanya mazungumzo kuhusu changamoto, mapambano dhidi ya ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa na mfumo wa usalama wa sehemu ya Asia na Pasifiki, na kutoa mapendekezo yao kuhusu usalama wa kikanda.

Walipojadili ajenda kuhusu "mustakabali wa usalama wa Asia ya mashariki", naibu mkuu wa jeshi la ukombozi wa umma la China luteni Jenerali Mao Xiaotian alisema, hali ya jumla ya usalama wa sehemu ya Asia na Pasifiki ya hivi sasa ni nzuri, lakini sehemu hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya usalama, hususan masuala ya upanuzi wa muungano wa kijeshi, ujenzi wa mfumo wa kupambana na makombora, kuweka silaha kwenye anga ya juu na kuenea kwa silaha za nyuklia, ambayo yameleta wasiwasi kwa usalama wa kikanda hata kwa usalama wa dunia, na kuathiri uwiano na ulingano wa nguvu ya kikanda. China inatetea kutimiza usalama wa jumuiya ya kimataifa, kupinga kuhakikisha usalama wa baadhi ya nchi kwa kuhatarisha usalama wa nchi nyingine, ikiwemo njia ya kupanua muungano wa kijeshi. Maslahi ya usalama ya nchi mbalimbali pamoja na mambo yanayofuatiliwa nazo yote yanatakiwa kuheshimiwa na kuzingatiwa ipasavyo. Kujenga na kuweka mfumo wa kupambana na makombora kunaathiri uhusiano na utulivu wa kimkakati. Anga ya juu inapaswa kutumiwa kwa amani na kuhimiza mchakato wa udhibiti wa silaha duniani.

Waziri wa ulinzi wa Japan Bw. Shigeru Ishiba akitoa hotuba alisema, iwe leo au katika siku za baadaye, Japan haina mpango wa kuwa taifa kubwa lenye silaha za nyukilia. Alisema baada ya kumalizika kwa vita baridi, baadhi ya matisho yaliyofichika katika kipindi cha vita baridi, sasa yanaanza kuibuka, hususan ugaidi. Alitoa mifano ya tukio la mashambulizi ya kigaidi ya "tarehe 11 Septemba" la Marekani pamoja na mauaji ya ovyo ya dhehebu ovu la Aum Shinrikyo ya Japan, na kusema Japan haiwezi kujisujudu kwa ugaidi. Kwa hiyo, Japan itaimarisha mazungumzo na nchi za jirani kuhusu mambo ya usalama, na kuendeleza uhusiano wa muungano wa usalama na Marekani.

Kuhusu suala la namna ya kubuni sera za ulinzi katika nyakati zenye mabadiliko mengi ya hali ya usalama, waziri wa ulinzi wa Korea ya Kusini Bw. Lee Sang Hee alisema, umaalumu wa hali ya usalama wa dunia katika karne ya 21 ni kutokuwa na uhakika. Hivyo, mwelekeo wa kubuni sera za ulinzi wa Korea ya Kusini ni kukuza kwa mfululizo nguvu za kijeshi ili kulingana na mabadiliko ya haraka ya hali ya usalama wa dunia katika karne ya 21. waziri wa ulinzi wa India, Bw. Palla Raju alisema India inapotunga sera za ulinzi, kwanza ni dhidi ya tishio kwa usalama wa nchini kutoka kwa watu wenye msimamo mkali wa kisiasa na ufarakanishaji; pia inazuia vitendo vya kigaidi vya pembezoni mwake visiathiri maendeleo na ustawi wa taifa; aidha, India itatunga sera za ulinzi kuhusu hali ya usalama wa dunia.

Kuhusu namna ya kurejesha amani katika hali ya dharura, naibu waziri mkuu wa Malaysia Bw. Najib Tun Razak alisema, hali ya dharura ni pamoja na matukio ya kimabavu ya nchini na kutoka nchi za nje, kupambana na maafa ya kimaumbile, kurejesha amani kunahitaji ushirikiano wa kikanda na kimataifa unaoongozwa na shirika moja maalumu. Alisema, "kituo cha kupunguza athari za maafa na utoaji misaada ya kibinadamu cha Umoja wa Asia kusini mashariki kilichoanzishwa Jakarta, Indonesia kitaanza kazi rasmi mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri wa ulinzi wa Singapore, Bw. Teo Chee Hean alisema, tunatakiwa kuanzisha ushirikiano wa usalama wa mitindo mbalimbali ili kuinua usalama wa kikanda, kwani matishio ya usalama yanayoikabili Asia ni ya aina mbalimbali.